Nape, yameishia wapi??

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,134
2,000
Kwako ndugu yangu Nape, nilitaka kufahamu yale ya Mawziri Mizigo yaliishia wapi>

Nimeelezwa kwenye Kamati ya Chama wajieleze lakini ninyi wenyewe mlitofautiana na kama si busara za Mwenyekiti basi hali ingekuwa mabya kwako na Katibu Mkuu Mzee Kinana kwa kuwa mlionekana kukivuruga chama kwa kukosa kuelewa ni yepi mnapaswa kuyazungumza mbele ya Maadui zenu (wapinzani) na yepi hampaswi kuyazungumza (ubovu wa ndani ya chama). Nilisikia kuwa ninyi (Nape na Kinana) mlionekana kutojua hata mnafanya nini na kwa kiasi kikubwa mlilaumiwa kwa kushindwa kuwa na mawasiliano wala kujibidisha kufahamu Mawaziri na Wizara za Serikali ya CCM zinafanya nini....Kwa mfano kwa lile la kulalamikia wakulima wanapata bei ya chini ya mazao yao lakini wakati hiuo huo mnalalamikia kuwa vyakula vimepanda bei mara dufu (hili inadaiwa hamkuwa na utashi wa kisayansi kujua nguvu za soko au uchumi wa soko unavyocheza). Wenzenu waliwaona hamkuwa na agenda njema kwa chama kwenye Ziara ya mikoani iliyotumia fedha nyinyi za walipakodia ndani ya CCM.

LABDA UTUJUZE HATIMA YA ZILE KELELE ZA MAWAZIRI MIZIGO WANANCHI TUTARAJIE NINI??AU NDIO YAMEKWISHA??
 

peace2007

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
213
195
Wanasubiri Waziri Mkuu awajibishwe, ndio raha yao hao! Ngoma walianzisha wenyewe sasa inakula kwao!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom