Nape: Sikuwahi sema kuwa Mafisadi wataondolewa CCM baada ya siku 90

Status
Not open for further replies.
Mwisho watawahoji, na kama kawaida watakao sema sio watashinda.
Ndivyo zitakavyoisha siku 90;)
 
Anafanya kazi ya bure,anajitahidi wenzake wana mlet down,acha na wewe, maana wanakuchukulia kama toy tu.....unafanya kazi ambayo haina kichwa wala miguu,,wewe unasafisha wenzako wanachafua....
 
Utawasikia wenzake mjengoni wakisema 'ndiyoooooo'kusaport pumba zao na kugonga meza zetu kwa fujo,na hilo gamba kubwa livuliwe 2015 tumewachoka jaman mtatuuza mpaka wananchi nyie!
 
Hakuna cha kujivua Gamba wala hakuna cha siku 90, asiyesadiki maneno yangu basi soma habari hii, Nape Kwishney.

Serikali yamsafisha rasmi Chenge
• Yamwondoa kwenye wizi wa pesa za rada

na Hellen Ngoromera, Dodoma



amka2.gif

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa kimewaweka pabaya makada wake watatu kinaotaka kuwafukuza uongozi katika vikao vikuu vya chama katika dhana ya kukjivua gamba, serikali imemsafisha rasmi mmoja wao, Andrew Chenge, ikidai hauhusiki na kashfa anazotuhumiwa.
Chenge, ambaye amekuwa akihusishwa na ufisadi katika ununuzi wa rada nchini Uingereza, alisafishwa na serikali jana bungeni kwa kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu makadirio ya matumizi na mapato ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Alisema Chenge hahusiki na kashfa ya ununuzi wa rada. Badala yake, serikali imewataja waliohusika katika tuhuma hizo kuwa ni dalali Sailesh Vithlani na vigogo wawili wa Kampuni ya BAE System ya Uingereza, inayotengeneza zana za kivita.
Alisema kwa mujibu wa Shirika la Uchunguzi wa Makosa Makubwa la Uingereza (SFO) na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa nchini (TAKUKURU), Chenge hakuonekana sehemu yoyote kuhusika katika sakata hilo.
"Hakuna ushahidi kuhusu Chenge kuhusika na mchakato huo wa rada, hivyo hatuwezi kwenda mahakamani kwa hisia, ndiyo maana hadi leo tulikaa kimya," alisema Chikawe.
Alisema suala la rada limekuwa likizungumzwa kwa muda mrefu na kwa namna mbalimbali, ikiwamo kupotoshwa, hivyo ikiwa kuna mtu ana ushahidi dhidi ya Chenge aupeleke kwa serikali ili wamshitaki haraka iwezekavyo.
"Kama hakuna ushahidi, ndiyo maana tunatangaza kama kanisani kuwa kama kuna mtu ana ushahidi na yanayosemwa alete, tutaushughulikia hata leo," alisema Chikawe kwa kujiamini.
Hatua hiyo inachukuliwa wakati zikiwa zimebaki siku chache kwa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kukaa kujadili, pamoja na mambo mengine, kuwafukuza uongozi makada walioamuliwa kujiondoa wenyewe kwa tuhuma za ubadhirifu, ambao hadi sasa hawajajiondoa.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Bunge iliyotumwa kufuatilia fedha za rada imewasilisha ripoti yake kwa Spika jana mchana huku ikipendekeza waliohusika katika kashfa hiyo ya ununuzi wa rada wa Tanzania na Uingereza wachukuliwe hatua.
Mapendekezo hayo yalitolewa jana na mjumbe wa kamati iliyoundwa kufuatilia fedha hizo, Mussa Azzan Zungu, kwa niaba ya wenzake. Kwa niaba ya kamati, Naibu Spika Job Ndugai ndiye aliyemkabidhi Spika Anne Makinda ripoti hiyo.
Katika ziara ya Uingereza, mbali na Ndugai na Zungu, wajumbe wengine walikuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (CCM) na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP).
Kamati ilipendekeza pia kwamba ifikapo Septemba, kama BAE Systems itakuwa haijatekeleza matakwa ya kukabidhi pesa hizo serikalini, ishitakiwe.
Zungu alisema walipokuwa Uingereza walisisitiza kwamba pesa hizo si msaada bali ni haki ya Watanzania.
Alisema kwa sasa Bunge la Uingereza na serikali wanatambua mchezo mchafu uliofanywa na BAE kwa kutaka kulipa fedha zetu kwa kutumia asasi za kiraia. Alisema Serikali ya Uingreza imeona uonevu huo wa BAE Systems.
Awali Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Job Ndugai, alikiri kwamba walipokuwa Uingereza walikuwa wakihojiwa kama serikali imekwisha kuchukua hatua zozote dhidi ya watuhumiwa waliosababisha pesa hizo kuibwa. Alisema hii ndiyo ilikuwa changamoto kubwa waliyokumbana nayo.
Hata hivyo, alisema kuna ugumu katika kuwashughulikia wahusika, kwani BAE walikwisha kujiondoa katika kashfa hiyo na kesi ilikwishafungwa, wakajisafisha.
Kwa mujibu wa Ndugai, kamati za Kampuni ya BAE na SFO zinatarajiwa kubanwa na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza kujibu tuhuma za sakata hilo la rada.
Ndugai alisema kikao hicho cha wazi cha pamoja kinatarajiwa kufanyika Julai 19 mwaka huu kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria, Taasisi ya Rushwa ya Uingereza na wengine.
Kamati hiyo ilikwenda Uingereza Juni 17, 2011 na kurejea Juni 28, 2011 kushawishi BAE ilipe pauni milioni 29.9 na riba yake kupitia katika akaunti ya BAE zilikohifadhiwa.



h.sep3.gif



 
Swali (Mwandishi wa habari):

Lakini kwa kuwa kujivua gamba ilikuwa ni mkakati wa dharura, kwanini msifanye vikao vya dharura vya haraka mkawaondoa watuhumiwa hao ili wasiendelee kukichafua chama, badala yake msubiri ratiba ya vikao vya Halmashauri Kuu?

Jibu (Nape):

Hiyo ni dhana potofu kuamini kuwa kujivua gamba ni kufukuza watu kwenye chama. Tunafanya mabadiliko katika ngazi zote za chama. Kufukuza watu ni moja tu mikakati. Kuna watu wamesahau kabisa kuwa rushwa ni adui wa haki, sasa watu kama hao tunawaondoa.
Kwanza, tumeweka sekretarieti ya chama ambayo iko muda wote, tofauti na zamani ambapo kulikuwa na mawaziri na watu wenye vyeo vingine hivyo kushindwa kukitumikia chama kikamilifu.

Kwa mfano, katika kitengo changu cha Itikadi na Uenezi, tumefanya mabadiliko hata ya watumishi.
Kuna makatibu wa mikoa sita waliokuwa wamepitisha muda wao tumewastaafisha. Kwa hiyo, tunaangalia mfumo mzima wa chama.
Vilevile, tunataka kupeleka madaraka ya kiuchumi mikoani ili isitegemee ruzuku kutoka makao makuu. Kuna mikoa yenye rasilimali za kutosha katika chama, wanaweza kabisa kulipana mishahara na mambo mengineyo, wafanye tu.

Tunataka pia kupitia upya utaratibu wa kupata mgombea urais kupitia chama chetu.
Aidha, tunataka kuwe na utaratibu mpya wa kuwapata wajumbe wa halmashauri kuu. Wasitoke tu mikoani, balipia katika wilaya.


Mytake: Kaona siku 90 zimepita hajafanya lolote anaanza kuleta blabla.
 
Ushauri wangu kwenu mkae kimya kwa kipindi hiki kigumu ambacho chama kinapitia.
Wengi wetu tumeanza kupima nakuona kuwa mna dharau kubwa mno kwa waliowapita umri kama
Lowasa, Dr Slaa na Chenge.Majibizano ya kutetea yasiyo wahusu wacheni, nawewe Riz1 kama hutaweza kumpeleka Dr(wa ukweli) mahakamani ukae kimya ili usifanye watu wakaona kama umefundishwa kiburi na chama au wazazi wako au yote mawili.W.Malecela acha vicheko vyako vya ha ha ha! wa tz wana fikiria na baba yako ana kujibu he he he, Nape sasa unaona Chenge amesafishwa bungeni wewe una mwita gamba?

USHAURI WANGU

mtulie kimya kama mabinti mabikira walivyo kuwa wanashauriwa (enzi hizo) na mabibi na makungwi zao usiku wa kuamkia ndoa kuwa kila kitu kita kuwa sawa na msihofie mume wako mpya, utamfurahia siku zote maisha.stahimili japo mnaumia.....just lay back and relax!
 
Yaani una maana watulie wanyolewe?!
Naamini umewapa ushauri mzuri maana walitaka kuwa wana CCM kuliko Kikwete mwenyewe na hii si sawasawa.
 
Ushauri wangu kwenu mkae kimya kwa kipindi hiki kigumu ambacho chama kinapitia.
Wengi wetu tumeanza kupima nakuona kuwa mna dharau kubwa mno kwa waliowapita umri kama
Lowasa, Dr Slaa na Chenge.Majibizano ya kutetea yasiyo wahusu wacheni, nawewe Riz1 kama hutaweza kumpeleka Dr(wa ukweli) mahakamani ukae kimya ili usifanye watu wakaona kama umefundishwa kiburi na chama au wazazi wako au yote mawili.W.Malecela acha vicheko vyako vya ha ha ha! wa tz wana fikiria na baba yako ana kujibu he he he, Nape sasa unaona Chenge amesafishwa bungeni wewe una mwita gamba?

USHAURI WANGU

mtulie kimya kama mabinti mabikira walivyo kuwa wanashauriwa (enzi hizo) na mabibi na makungwi zao usiku wa kuamkia ndoa kuwa kila kitu kita kuwa sawa na msihofie mume wako mpya, utamfurahia siku zote maisha.stahimili japo mnaumia.....just lay back and relax!

anaboa sana huyu
 
Watoto hawa bado wana fikira za enzi za machifu kuwa mtoto wa chief anathamani kubwa kuliko watoto wengini wakati siku hizi mambo ni tofauti kabisa kila mtu anajitafutia sehemu ya kulala kama watoto wa bata hawakumbatiwi kama wa kuku.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom