Nape: Sikuwahi sema kuwa Mafisadi wataondolewa CCM baada ya siku 90 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Sikuwahi sema kuwa Mafisadi wataondolewa CCM baada ya siku 90

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jun 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,207
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo maelezo mapya ya Nape kuhusu ahadi yake kwetu ya kuwavua gamba mafisadi 3 vigogo ndani ya CCM ifikapo July 10;Nape alitamka maneno haya" hopeless" jana wakati anazungumza na wahariri wa magazeti ya Mwananchi Communication LTD.

  Kuhusu watuhumiwa wa ufisadi na siku 90 walizopewa kujiondoa kwenye nyadhifa wanazoshikilia ndani ya chama, Nape alisema kuwa hakuna suala la siku 90 bali ni vikao vya chama vitakutana na kutoa maamuzi.

  "Siku 90 zinazozungumzwa ni tafsiri ya watu pale mwenyekiti wa chama (Jakaya Kikwete) aliposema tutakutana baada ya miezi mitatu na watu wakatafsiri hivyo, lakini vikao vya NEC ndivyo vinatoa maamuzi,"alisema Nape.

  Alisema kuwa hadi hivi sasa hajui makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alichozungumza na watuhumiwa hao wa ufisadi baada ya kukutana nao.​

  "Sikuwepo kwenye kikao hivyo hadi sasa sijui walizungumza nini, na siwezi kwenda kumtaka Katibu Mkuu anieleze kilichozungumzwa kwani katika vikao vijavyo tutapata taarifa,"alisema Nape.

  Source:Gazeti la Mwananchi June 29,2011
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Katika hii "movie" ya magamba episode hii imekuwa ndefu . Ndio kusema midirector na waandaaji bado hawajui wanadae nini kwa episode zinazofuata . teh teh teh teh
   
 3. H

  Honey K JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SI swala la kudai wala vikao kuamua upya bali vikao VILISHAFANYA UAMUZI NA UAMUZI NI WAJIPIME NA KUONDOKA WENYEWE WASIPOFANYA WATAFUKUZWA NA CHAMA.

  SWALA LA LINI NI PERIOD KUTOKA KIKAO KILICHOPITA CHA NEC MPAKA KIKAO KIJACHO CHA NEC, AMBACHO KWA MUJIBU WA KATIBA HUWA KINAKUTANA KILA BAADA YA MIEZI MINNE. Lakini SI LAZIMA IWE MIEZI MINNE KAMILI,KATIBA YA CCM INARUHUSU KUWA NA VIKAO MAALUMU KATIKATI KABLA YA MUDA HUO,HIVYO NEC INAWEZA KUKUTANA KABLA YA MIEZI HIYO KATIKATI KAMA ITAONEKANA IPO HAJA. NA INWEZA IKAKUTANA BAADA YA MIEZI MINNE KUTOKANA NA MAZINGIRA,KWA MFANO NAFASI YA MKITI KAMA IMEBANA TUNAWEZA KUSOGEZA MBELE SO SI SWALA LA SIKU EXACTLY.

  ANGALIA HATA BUNGE KUNA MUDA UMEPANGWA LAKINI LINAWEZASOGEZA SIKU ZA KUANZA AU KUMALIZA KUTEGEMEANA NA HAJA YA KUFANYA HIVYO.

  Kikubwa hapa NI KUWA WAHUSIKA WAMEITWA NA KUJULISHWA UAMUZI WA NEC NA KUWA UPO MUDA WA WAO KUTEKELEZA WASIPOFANYA KIKAO KIJACHO CHA NEC NI KUWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAMUZI ITAKAYO ONYESHA IMETEKELEZWA KWA KIASI GANI NA KUTEKELEZA SEHEMU YA PILI YA UAMUZI.

  KUMBUKA ILISEMWA HAPA JF KUWA UAMUZI HUU HAUTATEKELEZWA NA KUWA HAYO YALIKUWA MANENO (yalitumika maneno makali, machafu) YA NAPE NA CHILIGATI SI UAMUZI WA CHAMA, AKATOKA DR. KIKWETE MWENYEKITI WA CHAMA AKASEMA PALE DIAMOND ALIPOONGEA NA MAASKOFU KUWA ANACHOSEMA NAPE NI UAMUZI HALALI WA CHAMA, WATU WAKAFUMBA MACHO NA MASIKIO NA KUENDELEA KUDAI NI YA NAPE NA KUWA WATUHUMIWA HAWATACHUKULIWA HATUA ZOZOTE HATA KUJULISHWA TU. WAMEITWA NA KUPEWAA UAMUZI WA NEC, WATU WAKAKIMBIA JF, HATA WALE WALIONITUKANA NILIDHANI WATARUDI KUPONGEZA HATUA ILIYOFIKIWA, SIKUWAONA.

  NINACHOWEZA KUHAKIKISHIA HAPA UAMUZI HUU WA KUWAWAJIBISHA BAADHI YA WATUHUMIWA HAUTABADILISHWA KWA KELELE ZA BARABARANI NA SARAKASI ZA WATUHUMIWA, TUMETHUBUTU KUAMUA, TUTATEKELEZA MAAMUZI.

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,442
  Likes Received: 81,491
  Trophy Points: 280
  Siye tunatega masikio kusubiri kuona juhudi zenu za kulivua gamba ili kujua kama kweli mtalivua gamba au ni usanii tu. Nasema hivi kwa sababu hao mnaotaka kuwafukuza wameshaonyesha nia ya kutokuwa tayari kuondoka kimya kimya na hapo ndio shughuli ya kulivua gamba itakuwa tamu.

  Je, CCM itabaki kama ilivyo sasa au itasambaratika na labda kuzaliwa chama kingine cha siasa?
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Safi, hii ndo tungependa mara nyingi ufanye hapa JF, always firm kwny unachoamini, tatizo 'vijana wako' hapa JF (you know what I mean) kama usingewahi kuyaandika haya mwenyewe wangei-spin hii habari na kusababisha watu kuhama hata hoja.

  Kidumu?
   
 6. 911

  911 Platinum Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  I'm not crossing my fingers.Yaani miezi mitatu inakaribia kuisha mara mnaleta kibwagizo kipya cha miezi miNNE?Fool me once shame on you,fool me twice shame on me.
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yale yaleeeeeeeeeee ya Riz1 kumpa Mtikila na Dr Slaa siku sijui 7 au mwezi la sivyo anaendashtaki kortini na afidiwe sijui Trillion ngapi. Ulipofika muda anapindisha. Nilishawahi kusema Rostam na EL ni kiboko ya CCM na watanzania wote.

  Rostam & EL are absolutely just untouchable just like Al Capone....manake kila mtu kuanzia JK, Nape, UVCCM, na sisi wabongo woooteee tunapiga kelele then wanaufyata mkia. Rostam and EL ni kiboko!!
   
 8. fige

  fige JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kujitokeza kujibu mh sana Nape.
  Caution
  Siku hazigandi aliimba JD

  Hata tukifanya mwaka hivi vipi ?au ongeza iwe mwaka na nusu.

  Tatizo watu siku hizi ukisema siku gani wenzako wanaanza kuhesabu,tena kwa sauti,ili na wewe usisahau.

  Naomba kuuliza, hivi hamna kipindi maalum ambacho Mwenyekiti haruhusiwi kupitisha bila kuitisha kikao ?
   
 9. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwanini ni baadhi tu ndio watawajibishwa wengine vipi? Mmewasamehe au mnawahitaji?
   
 10. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hekaya za nape na sarakasi za ccm tumechoka nazo
   
 11. h

  hans79 JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  ni nan aliyemsafi ndani yao?huyu dogo aache unafiki,alipokuwa tbc1 na mukama alisema walitajwa kwa majina na barua zao z tayar lakin wakawa wanapingana wao kwa wao.pinda alisema kuwafukuza mafisad nchi itayumba,kelele za bure hana hoja nape n mtupu kaja ubaguz na ushabik wa kishamba.
   
 12. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Naomba mwenye nukuu ya nape ya kuwapa mafisadi siku 90 aimwage hapa
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani umeliweka sawa hili suala. Sasa kwenye hapo pekundu: wapime na kuondoka wenyewe sasa nijuavyo mimi hawa wameishaondolewa kwenye CC wamebaki kuwa wajumbe wa NEC na ni Wabunge. Sasa wanatakiwa waondoke Chamani au kwenye nyadhifa za NEC na Ubunge? Najua wakiondoka Chamani basi automatically watakuwa si waNEC wala Wabunge. Naomba utuweke sawa hapa ili tujue ni maamuzi gani tunayategemea.
   
 14. m

  mbaba Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nape tizama wenzio wasije kufanya kisusio,Jk mwenyewe anawaogopa kuwagusa hata ww nimegundua hizi kelele zako ni mbinu za kisiasa,watu wajue bado linafanyiwa kazi wajomba wanaendelea kula bata.

  Tia maji tia maji uchaguzi huo Lowasa kasimamishwa mgombea wa ccm,now umebadilika miezi4 utakujasema miaka3,jitahidi hizo ndo siasa za bongo zilizojaa unafiki kula kuku nani atakae kuuliza,ww mwenyewe kupewa nafasi hio ili watu hasa vijana eti waikubali ccm kisa kuna vijana,wewe makamba...,hizo tunaziita fikira mfirisi,mguse Rostam,Lowasa unase bora ata mzee wa vijicent..jitahidi utaweza!!!!
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Nape, acha kujidharirisha bwana!

  Mtu aliekuwa anasisitiza kuwa baada ya siku tisini niwewe wengine walijaribu kuelezea hiyo tafsiri wewe ukakomaa kuwa ni ndani ya siku tisini.

  Usitufanye wote wajinga kama mnavyowadanganya wanamagamba wenzenu...Nakwambia, Lowassa hatoki ccm! Akitoka mapigo atayojibu Jk atakimbia nchi!
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  kadri ninavyojua juu ya sakata hili ni kwamba nape anapaka rangi upepo....kwa kifupi ni kwamba hakuna atakayefukuzwa....hata nape deep down anajua hili na ndio maana anakuja na kauli tata sasa hivi anapoona siku zake alizotoa yeye na jk zinakatika tartiiiiibu....

  Nape nenda kwa msekwa atakwambia juu ya hali ilivyo..na pengine unajua ndio maana unakwepa kwa kusema kuwa hujui kilichozungumzwa......lakini pia mazungumzo ya jk na lowassa na yale ya Aziz Rostam na jk wiki mbilizilizopita.....kama kama hujui umetegwa kisiki kijana wangu utakapojikwaa ndio utajua nini namaanisha.
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu!!!
   
 18. e

  ejogo JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunasubiri tuone kama kweli mmethubutu na kuamua la sivyo anguko kubwa litawajia!
   
 19. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mi tatizo langu ni hapo kwenye red........kwa nini baadhi tu?
  Au ndo yale yale ya mbuzi wa kafara kuwaaminisha waTZ kuwa mnadhamira ya kweli kumbe mnafunika kombe!!!
   
 20. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mwenye ile nukuu ya kutoa siku tisini tunaomba muiweke tuweze kusoma kwa ufasaha jamaa anavyokataa mimba yake.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...