Nape si mzima!!

Kageuka

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2012
Posts
241
Reaction score
59
DR. SLAA NA KADI YA CCM, NA UNAFIKI WA WATETEZI *WAKE

Kwa muda sasa wa karibu wiki tatu au nne pamekuwa na mjadala mkubwa juu ya kumiliki kadi ya CCM kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na padri aliye asi Dr. Wilbroad Slaa.Mjadala huu umeingiza watu wengi sana kwenye maeneo mbalimbali lakini ukigawa wajadiliji kwenye makundi matatu makubwa, kundi la kwanza la wanaoona Dr. Slaa kateleza hasa majibu yake juu ya kwanini anayo kadi ya CCM, kundi la pili la watetezi wake na kundi la tatu la watazamaji wasiokuwa na upande maalum.

Nikiri wazi kuwa pamoja na kuwa mimi ndie niliyeanzisha mjadala huu, namheshimu sana Dr. Slaa kama mtu mzima sana kwangu na ndo maana huwa namuita babu,lakini bila kumumunya maneno ana mchango katika demokrasia ya nchi yetu bila kujali ni chanya au ni hasi.

Nilipo hoji umiliki wake wa kadi ya CCM nikiri kuwa sikutegemea kama angekiri haraka kiasi kile kuwa kweli anamiliki kadi, tena anaitunza kama kumbukumbu. Ndio maana mara baada ya kukiri haraka sana nilitoka hadharani na kumpongeza kwa mara ya kwanza toka nimfahamu ameamua kuwa mkweli. Nikasema ameanza vizuri kujifunza kuwa mkweli,baada ya orodha ndefu ya uongo na uzushi mwingi aliouzoea katika maisha yake ya siasa na yale ya utumishi wa Mungu yaliyomfikisha kwenye kumuasi Mungu na kanisa achilia mbali familia yake yaani mke na watoto.

Jambo kubwa hapa ambalo wapambe wake wanalifanyia unafiki ni kuwa nilipohoji SIKUHOJI UANACHAMA WAKE, NILIHOJI KUWA NA KADI YA CCM MPAKA LEO, TOKA ATOKE CCM KWA MAKEKE. Natambua vizuri sana kuwa uanachama wa CCM kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 matoleo yote, moja ya sababu ya kukoma uanachama ni kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa. Kwa tafsiri rahisi inatosha kujua kuwa Dr. Slaa si mwanachama wa CCM tena. Swali langu likawa kwanini anamiliki kadi ya CCM mpaka leo?

Watetezi wake hebu muulizeni Dr. Slaa alipoasi upadri nyumba ile ya utawa aliyokuwa akiishi kama padri aliondoka na funguo za ile nyumba au vifaa vingine vya upadri kwa madai kuwa ni kumbukumbu kuwa alikuwa padri wakati flani katika maisha yake? Tusikurupuke kumtetea tukadhani tunamsaidia ,kumsaidia kwa kweli ni kumwambia ukweli kuwa hapa babu umeteleza.

Wapo wanaodai hoja hii haina mashiko eti kwasababu hawaoni kama itabadili maisha ya watu masikini. Hawana makosa kusema haya kwasababu ndipo uwezo wao wa kufikiri walipoamua uishie. Lakini hebu fumbueni macho mtazame ukweli huu, moja ya tatizo kubwa la binadamu wengi na hasa viongozi ni kuwa wazuri sana wa kusema wasiyoyaamini wala kuyaishi ndo maana nchi nyingi masikini, rasilimali zake hazifaidishi walio wengi bali wachache sana,huku wakidai tufunge mkanda wakati wao wanaongeza ukubwa wa suti kwani zinawabana zilizopo.

Wakati flani Kardinali Pengo aliwa kusema, wengi wa wanaopigia kelele ufisadi ni mafisadi watarajiwa lakini kwasasa kwasababu hawajapata furusa za kuwa mafisadi ndo maana wana piga kelele.

Ikumbukwe Dr. Slaa amekuwa akipiga kelele na kuwataka wana CCM waliochoka CCM warudishe kadi za CCM na mfano mzuri ni pale Jangwani ambapo baada ya kulewa ujinga akaamua kuubatiza jina jingine uwanja wa Jangwani, bahati mbaya watanzania wana akili wakampuuza na wakaendelea kuenzi historia nzuri ya uwanja wa Jangwani kwa kuuita jina lake la asili, nadhani ulevi ule ulipoisha wa babu na wapambe wake akagundua kuwa alikuwa amelewa tu ndio maana hawajakumbushia tena jina lile.

Kwanini kama ni mkweli wa nafsi yake asiwaambie wanaorudisha kadi za CCM ukweli kuwa hata yeye katunza yake kama kumbukumbu kwahiyo nao watunze zao kama kumbukumbu, badala ya kuwahimiza warudishe wakati yeye katunza yake? Wapambe wake hili pia mnalifanyia unafiki!!!

Wakati yeye akimiliki kadi ya CCM amekuwa bingwa wa kuwashutumu wenzake *kuwa ni mamluki eti wa CCM ndani ya Chama chake wakati kati ya hao anaowashutumu na wengine kuwafukuza wengine hawajawahi hata kuwa na kadi tu za CCM. Watetezi wa babu hebu tuwe wa kweli kama kadi hii angekiri anayo Zitto hali ingekuaje? Mngetoka kumtetea pia dhidi ya hasira za babu na wafuasi wake dhidi ya Zitto au hasimu wake yeyote mwingine?

Babu anatofauti gani na wanaohimiza watu kujikinga na ukimwi wakati wao hata kinga hawaijui? Wanahutubia mkutano wa kupinga rushwa mpaka mapovu yanawatoka wakishuka wao ndo wanaulizia rushwa tena kwa ukali mkubwa? Anatofauti gani na msimamizi wa hospitali anayehimiza watu wakatibiwe kwenye hospitali hiyo na huku yeye mwenyewe hana imani na tiba za pale matokeo yake hata homa tu anakwenda ng'ambo kuitibu? Huyu ndo mnataka awe kiongozi mkuu wa nchi yetu? Anasema asiyoyaamini na kuishi asiyoyasema??!!

Mnasema ni hoja ya kipuuzi huku bado kucha kuchwa mnaijadili? Kwanini mjadili hoja ya kupuuzi kama kweli ni ya kipuuzi? Huu ni unafiki haupaswi kufumbiwa macho, ni vizuri tujifunze kukubali kujikosoa na kukosolewa.

Sina tabu na umiliki wa babu wa kadi ya CCM kama tu angewahamasisha na wengine wafanye kama anavyofanya yeye, kuongoza ni kuonyesha njia. Si uongozi bora kusema fuateni maneno yangu na si matendo yangu, kiongozi wa namna hiyo hatumhitaji kwasasa.

Ndio maana tunashuhudia CHADEMA chini ya babu huyu kama katibu mkuu wa chama, wameshindwa mpaka leo kuweka bayana msimamo wao juu ya sera za ushoga huku wakiwa marafiki na wapokeaji wakubwa wa misaada kutoka kwa waumini wakubwa wa ushoga duniani. Wanasiasa wanaosema wasichoamini na hawatendi isipokuwa wanataka watu watende. Onyesheni upendo wa kweli kwa babu yangu huyu kwa kumwambia ukweli badala ya kumdanganya na kumfanya apumbazike. KUONGOZA NI KUONYESHA NJIA.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
 
Hata mie namwona ana HERNIA YA UBONGO...!!
 
Umelogwa nan nani? Ni njaa ya tumbo ndiyo inayokusumbua wewe mtoto wa nje ya ndoa.
Ndio maana wenzako hawakukushirikisha katika vikao vya kumbukumbu ya mzee Salumu Abdallah
 
Kama kweli imetolewa na wewe ni Nape nakubaliana na kichwa cha habari kuwa si mzima na hakuna wa kukutibu. Upumbavu ni majaliwa
 
jf huku anaanzishaga mijadala halafu anaikimbia..hii hatutamjibu tumechoka kubadilisha kwake maneno..mara mwanachama wa ccm,mara sikusema hivyo..vuvuzela
 
Nape,

Katiba ya ccm inasema kadi ni mali ya ccm ama ya mwanachama?

Huna mkakati mwingine wa kumarisha chama chako cha ccm zaidi ya kujidharirisha na mbinu hafifu za kuua mshikamano wa CHADEMA?

Huna sifa, uwezo wala vigezo vya kupambana na Dr Slaa wewe. Waliokushauri wana kudanganya.


Ushauri wangu, kama huna job description ama huna kazi za kufanya katika kufufua chama chako ccm, omba likizo isiyo na malipo ukapumzike. Unachokifanya sasa kinazidi kuharibu image ya ccm na kinaweka peupe namna gani mmebaki watupu.
 
dah ... akili nyingine zimechanganyika na silicon
 
Nape,
Kama ujinga unalewesha basi na wewe umeshalewa siku nyingi.
 

Msumari huo,nape yupo vizuri cha msingi ni kujibu hoja je ingekiwa zitto ingekuwa vipi ? Na je kauli ya padr mzinifu kwamba kuwa na kadi ya ccm ni laana nayo mnasemaje ? Na je kuwaadaa wenzakevwarudishe kadi za ccm wakati yeye bado anaitunza siyo unafiki ?
 
Ukisoma post hiyo siyo ya graduate wa masters mie nakataa kwa sababu zifuatazo:

Una lugha ya matusi,

Una lugha ya dharau,

Una chembe chembe za ubaguzi wa kiumri, na kidini,

Unajiona wewe ndio bora kuliko wengine.

Ningekuwa mimi ndo TCU ningekuvua digrii zako za kuchakachua
 

Ninahisi huu upuuzi wako ungeupeleka uhuru na mzalendo ungekupa sifa zenu za kijimga mlizozoea kupeana. Kiongozi mzima wa chama tawala huna cha kufanya ni aibu.watu wanauawa na polisi wenu mpo kimya kazi yenu ni kulisha ujinga watu mitandaoni, nape unabore na unasababisha tuendelee kuichukia ccm kwa upuuzi km huu
 

Nape usituondoe kwenye mada zinazo husu mateso ya waTanganyika yanayo tokana na UFISADI anao asisiwa na chama chenu.

Unataka kuwaambia waTanganyika kwamba hujui utumishi ndani ya Kanisa lolote lile unakoma, endepo Mtumishi anaamua kuacha. Uasi unao sema Dr. Slaa ameufanya ndani ya kanisa mbona wenye kuliongoza kanisa hawaja usema? Au wewe wakati huo ndio ulikuwa kiongozi wa hilo kanisa?

awali mlikuja na kashfa hapa kwamba Dr. slaa alikimbia na michango ya ujio wa Papa John Paulo, mkatoka hola!!!! Leo mnakuja na kashfa nyingine za kipuuzi puuzi hapa. Kama ni suala la kuachana na mke, mbona Mwenyekiti wako hatuja muona na mkewe wa kwanza? Naye si alitumia uhuru wake kuoa huyo Mmakua!!!!???? Au kwa vile mmehodhi media zote na haandikwi uchafu wake ndiyo mmepata cheti cha kukashifu watu wengine kisa kutetea ulaji wenu????

Pamoja na kwamba unataka kutuondoa kwenye mada kuu ambazo zinakitesa chama chako, tutaendelea kukomalia CCM hadi pale itakapo wafanyia waTanganyika maendeleo wanayo yataka kulingana na rasilimali zetu zilizopo.

Eti, sifa za kupata uongozi na kuitwa Mheshimiwa kwenye chama chenu si lazima uwe FISADI?

Nakuhakikishia kwamba kuanzia mapema mwakani, majukwaa mtaya kimbia. Mtabakia huko huko kwenye Radio na Telivisheni ambazo ingawa zinaendeshwa na kodi za waTanganyika mmeamua kuzi hodhi.
 

Wajadiliji ndio nini tena?
 
Nape kama mwanasiasa utakuwa umeacha legacy gani ukifa? Matusi? Upuuzi?
 
 

Kama unajadili siasa, ondoa neno PADRE kwani ni kiongozi wa imani ya watu wengine na Dr. Slaa si Padre kwani alishajiondoa katika huduma na kwa taarifa yenu alifuata taratibu zote za kusitisha huduma.

La pili ukiwa na akili angalau kidogo huwezi kuyachukua mawili haya kwa wakati mmoja:
1. Kama Dr. Slaa ana mapenzi na CCM, asingewaambia wengine warudishe kadi kwa kuwa atakuwa anaiangamiza CCM yake.
2. Kama CCM kweli wanamuona Dr.Slaa ni sehemu ya timu yao kwa kuwa ana kadi yao (which means anafanya kazi yao) how come Nape amuumbue ikiwa kweli ni pamdikizi lao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…