Nape Nnauye: Process ya kumfukuza mtu CCM ni ndefu

Nape Nnauye: Process ya kumfukuza mtu CCM ni ndefu

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amesifu utaratibu wa CCM unaofuatwa kabla ya kumfukuza mtu uanachama na amesema kwa CCM kuna vikao vingi kabla uamuzi wa kumfukuza mtu uanachama haujafikiwa.

Pia,Nape amedai kinachomponza Zitto ni kuhoji maswala ya ukaguzi wa ruzuku na nia yake ya kugombea uongozi ndani ya chama.

Vile vile Nape amepiga kijembe kwa kusema kama watu hawa wakipewa madaraka makubwa ya kushika dola itakuwaje kama madaraka ya kuongoza chama tu wanayatumia hivyo.

Nape allikuwa akiongea katika mahojiano na mtangazi wa TBC 1 asubuhi hii kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1.

MT TAKE:
CCM waliwahi kujaribu kumfukuza nani uanachama katika siku za hivi karibuni?

Na hapo ndipo ulipo ubora wa CHADEMA. Hawafugi wahalifu ambao baadaye watakigeuza chama kuwa cha mafisadi kama ilivyo CCM.
 
Ukweli ni kuwa kama Nape aliongea hivyo hajasema uwongo. Katika CCM hakuna utaratibu wa kufukuzana na ndiyo maana nchi yetu inaendeshwa hovyo kwa sababu ya kuongozwa na chama kisichoweza kuwawajibisha viongozi wake. Nape alipopewa nafasi aliyonayo alitoa siku 90 kwa mafisadi kujiuzulu na kwamba wasingefanya hivyo wangeshughulikiwa. Hadi leo hakikufanyika chochote zaidi ule wimbo alianza kuuimba na Ndugu Kinana kuwa kuna mawaziri mizigo.

Kwa kusema kuwa katika CCM kuna process ndefu ya mtu kufukuzwa katika CCM siyo jambo zuri bali ni udhaifu. Udhaifu huo ndio ambao unalipeleka taifa pabaya. Fikiria twiga anasafirishwa nje ya nchi hakuna anayewajibishwa kwa sababu process ni ndefu ya kuwajibishana na mwisho wa siku hakuna kuwajibishana. Kwa sababu ya uzembe wao huo tunashangaa eti tembo wanauawa wengi na wapo hatarini kutoweka, tunataka tumlaumu nani?

Tunakushukuru Nape kwa kauli yako hiyo kwani umekuwa mkweli lakini ujue unatuambia udhaifu wenu na wala hatuna la kuiga hapo.

Hamna lolote mna homa ya uchaguzi na ukaguzi wa hesabu za ruzuku,
haya ndio yanayomponza ZZK.
 
Vikao gani vilikaa kuwafukuza uanachama Aboud Jumbe pamoja na Seif Shariff Hamad kama sio CC ya CCM ikiongozwa na Mwalimu? Nape acha unafiki , wenzio wanakuchora tu kwani wanajua kuwa wewe ni ccj!!!
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amesifu utaratibu wa CCM unaofuatwa kabla ya kumfukuza mtu uanachama na amesema kwa CCM kuna vikao vingi kabla uamuzi wa kumfukuza mtu uanachama haujafikiwa.

Pia,Nape amedai kinachomponza Zitto ni kuhoji maswala ya ukaguzi wa ruzuku na nia yake ya kugombea uongozi ndani ya chama.

Vile vile Nape amepiga kijembe kwa kusema kama watu hawa wakipewa madaraka makubwa ya kushika dola itakuwaje kama madaraka ya kuongoza chama tu wanayatumia hivyo.

Nape allikuwa akiongea katika mahojiano na mtangazi wa TBC 1 asubuhi hii kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1.

MT TAKE:
CCM waliwahi kujaribu kumfukuza nani uanachama katika siku za hivi karibuni?


Mansoor alivyotolewa kafara juzi juzi. Ccm wao kwanza njia yao ni fupi zaidi tena ya haraka Kolimba ilikuwaje mpe sumu kabla hatoa siri nje. Sokoine ulia mbali kabla mafisadi hawajakamatwa.
 
Mansoor Himid aliyefukuzwa Kisiwandui ndani ya siku tu na shauri lake kuletwa CC-Dodoma then kufukuzwa bila yy kuitwa kujitetea ndiyo process ndefu?Ukiwa muongo usiwe msahaulifu

Process ndefu my stinking foot!
 
Ni kweli Komred Nape ndo maana ni ngumu kuwafukuza mafisadi,majangiri na wala rushwa waliopo chamani. Process ni ndefu ndo maana heri wabaki tu coz ni hasara sababu vikao ni vingi.
 
CCM hakuna wa kumfukuza mwingine wote wananuka rushwa,ufisadi
Yule Mansor wa Zanzibar wamefukuza kwa kudai kwake zanzibar huru kitu
ambacho kitawaharibia mashali ya chama.
kwa utashi wake amekataa kuwa mbunge wa mahakama..
CCM haana uthubutu wa kumfukuza mtu wa bara,hebu wajaribu kwa Lowassa tuone,
Nape hajui kilichomfanya Zitto avuliwe vyeo vyake alivoomba mwenyewe kujiuzulu??
 
Touch-Log Out

Forum-New Posts-Settings-Search


->-Forum->-General Forums->-Jukwaa la Siasa

Topic:-nape wa ccm ni sawa na zito wa chadema

longinos-12:00 Today-

Ukifuatilia siasa za hawa dogo zinafanana, nape alipoleta ukorofi kuhusu jengo la uvcccm alijifanya ni mpambanaji, mtetezi wa vijana nakujifanya ccm anaijuwa kuliko akina EL eti kwa sababu baba yake alikuwa kwaya masta wa ccm(kama komba)kilichompa nafasi moses nnauye ni kuimba si weledi wa siasa.Nepi aliporudishwa kundini na jakaya alirudi na kauli mbiu KUFUKUZA MAGAMBA NDANI SIKU 90 naamini ni siku 90000.Kinachojitokeza ni kunenepeana kwa Nepi bila majibu ya siki 90.
Zito nae kaja na gear hiyo hiyo, nilijiunga cdm nikiwa na miaka16 so what oh wengine wametoka ccm wanajifanya wanakijua chama, hizi ni kauli na kijuha ambazo hazina mshiko sijui zito alitaka watu watokee mwandiga au kwa ndugu zake wa asili Bujumbura? Kama unakipeleka chama mahakamani unategemea huruma gani kwa wana cdm? Tamaa na kutaka sifa ndiko kunakowasumbua waili hawa na hawatafika popote kisiasz maana WANAFIKI walilaaniwa hata kwenye vitabu vya dini mwisho wa zito na nape 2015 sababu Kikwete akitoka Nepi inabini akajiunge na Frelimo ya msumbiji na MM Zito mahakama itakulinnda mpaka 2015 baada ya hapo utatupwa chali, wapi masumbuko lamwahi, poleni sana.

Edit-Reply-Report Post


Tags

Up

Copyright JamiiForums.com
 
:hand:Nape kubali tu kuwa CCM ni dhaifu ndo maana mnaogopa kufukuza,kwani kilicho baki ndani ya chama chenu nikulindana ili kulinda uhai CCM huo ndo ukweli.
 
Barongo alipofukuzwa uwanachama vikao vilikaa miaka mingapi au ulikuwa hujazaliwa we dogo kwa misifa ni kama zito
 
Hajui kuwa maisha hayana formula na kila kunavyokucha akili za binadamu ambao ndio wanachama wa vyama zinabadilika.
Siku akiinuka mtu ambaye anasema kuwa "siwezi kuwa chini ya mwenyekiti kama jk" na hata mwenyekiti yeyote bali mimi mwenyewe. Mkamuita huko Chimwaga kumhoji badala yake akaenda Kisutu ndio utatupa maoni ya hiyo michakato yao.
 
Nape anatumia 75% ya hotuba zake juu yaCDM,anwazungumzi Slaa na Mbowe kuliko JK na Kinana.CDM kuliko CCM anaogopa nini?
 
Sasa Lowasa ndie atakaegombea uraisi kwa tiketi ya ccm, kamwambie huyo Nape anze mpango wa kutafuta uraiya wa nchi jirani kama alivyo aidi.
Nape utaangaika sana ndo maana ccm kuna mgawanyiko na ww unajulikana upokundi gani na kuhusu zzk mchukueni aje afanye siasa safi ccm na kwa ushairi jenga chama chako achana na cdm
 
Back
Top Bottom