Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 264
Mwanzoni mwa miaka ya tisini, nikiwa kijana mdogo kabisa kambini kwetu akaja mgeni. Mosses Nnawie. Kulikua na shuhuli fulani ya kijeshi.
Mosses Nnawie alikuwa mhamasishaji wa chama ndani ya jeshi. Alikuja na kinanda chake na mtoto wake. Mtoto wake alikuwa mdogo lakini akacheza kinanda, akajitahidi kutufurahisha. It was not the best but kwa umri wake alituburudisha. Nape Mosses Nnawie leo hii anafanya kazi aliyoifanya baba yake ndani ya chama hicho hicho, lakini siyo jeshini.
Wakati huo alimsindikiza baba yake kila mahali (akasahau kusoma). Leo ameteuliwa kuwasindikiza babu zake, Msekwa, Wassira, Chiligati, na Mukama. Wakati huo alibeba kinanda cha baba yake, leo hii itabidi abebe ugoro wa babu zake ndani ya chama. Wakati huo alicheza kinanda, leo hii anacheza rumba la nguvu ya umma na JF.
Ni kutokana na uzoefu wake wa kuwa anabeba mikoba ya baba yake tangu akiwa mdogo, ndiyo maana akafuzu vigezo vya kuteuliwa kufanya kazi na hao babu wa ccm. Ilikuwa ni jukumu la kifahari wakati huo, lakini kwa kazi hii mpya ni fedheha.
Vuta hisia, kama uliwahi kuishi nyumba moja na babu yako. Jiulize ni kwa namna nyingi kiasi gani asivyokubaliana na mawazo yako. Jiulize kuhusu babu kutokupenda kuonekana kwamba hajui. Jiulize kuhusu babu kutokubaliana na namna za kisasa za kufanya jambo. Babu anapenda kusikilizwa na kuheshimiwa.
Kuna mfano tayari. Msekwa anasema watapambana na JF (siyo Chadema!). Sijui kama anajua hasa anasema nini, natumani Nape anaelewa babu yake karopoka tu. Lakini by default and protocal ni Nape ndiye anatakiwa ahamasishe mapambano dhidi ya JF!
Jaribu kujiuliza ni vipi inawezekana kupambana na JF. Watafanyaje kupigana na kitu ambacho hakishikiki. Kitu ambacho siyo taasisi. Kitu ambacho kinaweze kuendeshwa kutokea mahali popote duniani, kinakuwa managed kutokea kwenye computer yoyote au simu. Ukifunga huku wanafungua kule. Ukimkamata huyu, wale wanaendeleza.
Kwamba Msekwa anamwagiza Nape apambane na keyboard? Ipi? Wapi? Hao mababu wana uwezo na nguvu ya kupambana na ufisadi ndani ya ccm na pia kudhoofisha Chadema na JF?
Well, Nape atafanikiwa tu kuwabebea hao wazee ugoro na siyo kupambana na nguvu ya umma wala JF.
Should I say, for ccm, it is as good as a doomsday conspiracy?