Tetesi: Nape Nnauye kuhamia CHADEMA?

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
987
NAPE KUHAMIA CHADEMA?

TAARIFA za uhakika zinasema kuna mazungumzo ya mara kwa mara kati ya mbunge wa Mtama Nape Nnauye na baadhi ya viongozi wa Chadema wakimshawishi kuhamia chama hicho.

Mmoja wa viongozi hao ni Edward Lowassa jambo ambalo tayari mwenyewe amethibitisha kupitia mkutano wake aliofanya hivi karibuni huko Mtama.

Kwenye mkutano huo Nape alisema wanakutana na Lowassa mara kwa mara na wanazungumza na kunywa chai pamoja ingawa hakuweka wazi wanazungumzia kitu gani.

Itakumbukwa kwamba, Nape na Lowassa wamekuwa kwenye mgogoro kwa miaka mingi na mbunge huyo aliwahi kumtuhumu Lowassa kuingia mkataba tata na mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya kiasia kwenye ujenzi wa jengo la Umoja wa vijana lililopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Nape pia amewahi kumshambulia Lowassa kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi na hata afya yake kwenye uchaguzi mkuu uliopita, lakini baada ya mazungumzo yao Nape kawekewa sharti la kuhamia Chadema.

“Moja ya masharti aliyopewa na Lowassa ni kuhamia Chadema, ingawa kuna watu wamemshauri abaki CCM kwasababu kuhamia Chadema ni mpango wa kummaliza uliopangwa na Lowassa ili kulipiza kisasi cha mambo aliyomfanyia, anajua akihama CCM na kwenda Chadema atakuwa kajimaliza kisiasa” alisema mbunge mmoja kijana wa Chadema kutoka nyanda za juu kusini.

Mbunge mmoja wa Chadema (jina tunahifadhi) amenukuliwa akimponda Nape na kusema Chadema wanakaribisha tatizo, huku akielezea jinsi alivyomtumia kutoa siri za chama na kuchapwa kwenye gazeti moja la kia wiki lenye nasaba na Chadema.

“Nape namjua mimi, haya mambo ya kumleta chamani yataleta matatizo, siri zote zitatoka nje, hana tofauti na Zitto. Nape kaleta siri nyingi za chama chake na tumechapa kwenye gazeti letu, tena alikuwa anakuja mwenyewe Kinondoni kuleta stori na tulikuwa tunampa kompyuta wakati mwingine anapacha stori, haaminiki” alinukuliwa mbunge huyo ambaye pia ni mwandishi wa habari.

Hata hivyo, licha ya wanachama wa chama hicho kumpinga Nape kuhamia Chadema, Mwenyekiti wao Freeman Mbowe anaendelea na msimamo wa kumtaka ahame CCM kwa lengo la kutaka kuongeza mtaji wa kisiasa huku akiamini hatua hiyo itaivuruga CCM.

Tayari Mbowe ameagiza kwa wahariri wa gazeti lake la Tanzania Daima kuhakikisha habari za Nape zinapewa upendeleo kwenye gazeti lake ambalo tayari maelekezo hayo yameanza kwa gazeti la 11, April kwenye ukurasa wa mbele.

Kikwazo kingine anachokabiliwa nacho Nape na kukwamisha safari yake ya kutaka kuhamia Chadema ambayo mwenyewe anaonekana yupo tayari, ni msimamo wake aliowahi kuweka wa kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya bunge wakati akiwa Waziri wa habari huku miongoni mwa wanaoiunga mkono Chadema wanaendelea kumpinga na kumuita ‘adui wa uhuru wa habari.’

Baadhi ya wabunge wanahoji, kama waliwahi kumshambulia Nape na kumuita aduia wa uhuru wa habari, wakamtolea maneno machafu na hata kufikia hatua ya kuponda uteuzi wake na kudai amepewa nafasi hiyo kwa kulipa fadhila kutokana na kushiriki kampeni, inakuaje leo anaonekana ni mtu muhimu kwa Chadema?

Wanahoji, waliwahi kumuita Nape vuvuzela, inakuaje Chadema inapokea vuvuzela kwa maana ya mpiga kelele ambaye hana tija kwa chama?

Mbali na hilo, wanaharakati mbalimbali wakiwemo wale wanaokiunga mkono chama hicho, wanajipanga kutoa tamko kulaani kitendo cha Nape kutembelea kwenye miili ya akinamama akiwa Mtama.

Kitendo hicho ambacho licha ya kutetewa na baadhi ya watu wanaomuunga mkono, kimepingwa na watu mbalimbali akiwemo Issa Shivji ambaye amesema ni kitendo kibaya na hakipaswi kuungwa mkono.

Shivji alisema, Nape alipaswa kuwashukuru akinamama hao kwa heshima waliyompa na kuishi hapo badala ya kutembea juu ya miili ya akinamama hao.

“Angekataa. “Nawashukuru sana mama zangu. Nilijitolea kuwahudumia kuwa chini yenu kama mtoto wenu, sio kuwakanyaga” aliandika Shivji kwenye ukurasa wake wa Twitter.
 
Kama ni kweli lowassa hatakuwa na Matatizo. Anatumiwa kisawa sawa!

Watu wanatafuta attention kwa Magufuli!
 
Mleta thread umelipwa nini kukizalilisha Chadema kuwa hula matapishi? Nani amekuambia anahitajika kama mtaji
 
doo, akili zako unazifahamu mwenyewe. ombi langu kwako uwe unajaribu kusummarize maana hii ni kama ulikuwa unatengeneza series ya kichina
 
Kawaulize usalama wa CCM na kikosi maalum au bwana yule, hapa hatuna majibu, samahani!
 
Nape hajawekeza akili kwa Lowassa kama atajiunga CHADEMA ni maamuzi yake binafsi nasiyo kwa sababu kashawishiwa na Lowassa.
 
Back
Top Bottom