MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
[video=youtube_share;6oejkH1DCz4]http://youtu.be/6oejkH1DCz4[/video]
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amepeleKa ‘msiba' Kwenye vyama vya upinzani, baada ya kusomba wanachama wa vyama hivyo ambao wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut), tawi la Mwanza, wakiongozwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (Sautso), Philbert Saimon.
Wanachama hao ambao wengi ni wanachama wa CHADEMA waliamua kuhama chama hicho jana, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Nyamalango, nje kidogo ya Chuo cha Saut, ambapo Nape alikuwa mgeni rasmi.
Akieleza sababu zilizomfanya ahame CHADEMA, Philbert Saimon alisema, "Tumepoteza muda mrefu kuwatumikia watu wasio na mwelekeo, watu ambao wamejaa uongo na ubabaishaji mwingi, wakati sisi tunahangaika, tunaacha masomo kwa ajili yao, watoto wao wanasoma vizuri, tumechoka kutumiwa, CCM ndio mpango mzima."
Vijana wengine walipohojiwa kwa nyakati tofauti walisema kwa muda sasa CCM imeanza kwa kasi kubwa kurekebisha upungufu uliokuwa ukikabili chama hicho na hivyo kuvutia wengi kuiamini na hili linayochangia kuua kabisa vyama vya upinzani nchini.
Nape kwa upande wake alisema: "Wenzangu walikuja hapa na talalila nyingi sana, leo nitajibu hoja moja baada ya nyingine na nitaanza na la changamoto za elimu."
Alisema mchakato wa ujenzi wa shule za sekondari za kata ulipoanza, wapinzani wengi walikejeli na kuzipa majina mbalimbali, lakini walioanza shule za sekondari za kata mwaka ule leo ndio wanamaliza vyuo vikuu nchini na wengine wako nje ya nchi.
Alieleza jinsi Serikali kwa kushirikiana na wananchi, inavyojenga maabara kwenye sekondari za kata na kupeleka walimu kwa mamia kila wilaya, ili kuboresha elimu nchini na kuwataka wananchi kupuuza wote wanabeza mafanikio hayo.
Kuhusu Kikundi kinachojiita UKAWA. Nape aliendelea kusisitiza msimamo wa CCM wa kutowabembeleza wajumbe hao kurudi katika Bunge Maalumu la Katiba, akidai ni kupoteza muda kwa watu wasiokuwa na nia njema ya kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.
"Hawa wenzetu wamegeuza huu mchakato kama mchezo, kila wakigoma wanabembelezwa, wanapewa juisi Ikulu wanarudi bungeni, sasa wamegeuza mchezo, safari hii habembelezwi mtu, kama noma na iwe noma.
"Sheria ya mchakato Katiba mpya wameshiriki tukatunga wote, na sheria imeeleza wazi kuwa tutakuwa na awamu tatu kuu za kukamilisha mchakato wa Katiba mpya nchini.
"Awamu ya kwanza ni ya kukusanya maoni, awamu ya pili ni ya kujadili na kuyachambua maoni na awamu ya tatu ni ya kuipitisha kwa kupiga kura za maoni kwa wananchi. Asiyetaka kufuata utaratibu tuliojiwekea, hana nia njema na upatikanaji wa Katiba mpya," alisema Nape.
Nape alisisitiza kuwa hoja ya kuwa CCM haitaki Katiba mpya ni hoja mfu kwani aliyetangaza na kuanzisha mchakato ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Serikali ndiyo inayotoa fedha za kugharamia mchakato huo na kama CCM isingetaka Katiba mpya, isingefanya hayo yote.
"Hata mjadala wenyewe na utoaji wa maoni kwenye rasimu hakuna taasisi iliuchukulia kwa umuhimu mkubwa mchakato huo kuliko CCM, mpaka tumetoa maoni yetu kwa maandishi na machapisho kadhaa.
"Sasa wenzetu wanaounda genge la UKAWA wakati hata mmoja wao hana chapisho lolote zaidi ya ubabaishaji na kelele nyingi. Ndio maana wanafikia mahali wanadai muundo wa serikali tatu utadhibiti ufisadi nchini, nataka kujua serikali tatu inadhibiti vipi ufisadi? Si lazima kuwa na serikali tatu ndio udhibiti ufisadi," alisema Nape.
Nape alisisitiza kuwa UKAWA itasambaratika bila mkono wa CCM, na kuwa CCM hawana muda wa kuhangaika kusambaratisha upinzani kwani upinzani utajisambaratisha wenyewe kwa mbegu mbaya walizopanda na wanaendelea kuzipanda.
"Huwezi kupanda mahindi ukavuna uwele, kile unachopanda ndicho utakachovuna," alisema.
============================== =================
BAADHI YA PICHA ZA MKUTANO.
Wanachama wa Tawi la CCM SAUT wakiburudisha kwa kucheza na kuimba nyimbo mbali mbali.
Wanachama wa CCM SAUT wakionyesha ujumbe kutoka kwenye mabango
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage na wananchi wa Nyamalango wilaya ya Nyamagana, Mwanza ambapo aliwaambia kuwa CCM itaendelea kuongoza kwani ndio chama pekee nchini chenye sera na mipango inayoeleweka kwa wananchi huku ahadi zake zinatekelezwa kila kona ya nchi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea kadi ya CHADEMA kutoka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki ambaye amejiunga rasmi na CCM,katika mkutano huo zaidi ya wanafunzi 86 wa chuo hiko wamejiunga na CCM.
Kadi za wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine Mwanza.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine, Ndugu Simon Philbert Macheyeki akiwa na wanachama wengine wapya wakila kiapo cha kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamalango wilayani Nyamagana.
Wanachama wapya zaidi ya 420 wajiunga na CCM kutoka Chuo Kikuu cha SAUT.
Ujumbe kutoka kwa Tawi la CCM SAUT
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wananchi na wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage Mwanza.