Nape Nnauye: An exemplary leader!

Nape Nnauye: An exemplary leader!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,566
Reaction score
28,527
2.jpg


Nimeheshimu sana msimamo wa Nape Nnauye, kijana mdogo(kwangu) ambaye amesimamia si tu kauli yake bali hata kwa vitendo kuonyesha udhaifu uliotokea katika eneo lake na kuchukua hatua stahiki kulielezea, kuchunguza na hatimaye kama aivyosema , kukabidhi kwenye mamlaka husika.

Mtu kuwa mkweli, ni mpenzi wa Mungu.

Unafiki, woga wa kutumbuliwa hausaidii sana mbele ya ukweli.

Nape ameonyesha jinsi ambavyo amekuwa consistent katika suala zima linalo mkabili Makonda.

Kama tungekuwa na viongozi kama Nape, kutokubali kuwa waoga hata pale wanaofanya madudu katika maeneo yao ya utawala ni wakubwa, tungekuwa mbali kiuwajibikaji.

Vyeti feki vina eneo lake, wenye eneo hilo wako kimya kama maji ya mtungi, wanajitukanisha kwa kweli.

Hata leo, Nape aidha akiondolewa au kujiuzulu, mfano chanya utakuwa umewekwa katika uongozi wa Taifa.

Watu kama hawa huja kwa nadra.

Big up Nape Nnauye, mwana wa Moses.
 
Nadhani Nape ameonyesha njia amesimamia kazi yake. Sio sababu yamkuu kumgusa ama kumchukia na akifanya hivyo basi Mkuu ataingia kwenye vitabu vya historia.
 
ni nadra sana kwa viongozi kutofautiana..hadharani

kibongobongo nape jiandae...yaani jipange
 
Tatizo sasa haya aliyofanya yatamfurahisha baba yake mtoto pendwa anayependezwa naye???
 
Back
Top Bottom