Nape Nnauye akielezea "Fedha Chafu" za CHADEMA

Mungu ni mwema sana kawaweka watu watakaokichafua na kuhiharibu chama chao ili nchi ikombolowe
mfano Nape, hao mafisadi wanaoficha pesa nje, wabunge wala rushwa, wizi wa rasilimali nk
nape anafanya kazi nzuri sana za kukuzamisha chama nampa bigup
nashangaa mnaomshambulia badala ya kumsifu na kumshukuru Mungu kwa kutuwekea huyu mtu kama Nape.
 
Hahah napee. Jiangalie kaka CCM sio kama vile ujiavyo. Ngoja CDM wakuchukulie hatua ndio utajua.
 
Kwa kuzingatia kwamba hata CCM wanapokea 'kitu' kutoka nje, wamefanya harambee mara kadhaa Nimekumbuka hii (kutoka gazeti la mwanahalisi; si ajabu hatimaye lilifungiwa)

CCM wana ugonjwa wa kusahau



picture-252.jpg

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 28 March 2012

Wazo Mbadala


KATIKA maisha yake yote, Bogi Benda alikuwa msumbufu. Mtu wa vituko, dharau, kejeli. Bali alivumiliwa kwa vile alikuwa ‘bosi’.
Kuna wakati alipotaka kuzima hoja fulani ili kusumbua tu watu, aliamua kulala na kukoroma kwenye vikao.
Kuna siku alikwenda hospitali akitaka atibiwe ugonjwa wa kusahau aliodai unamsumbua sana. Akabahatika. Alimkuta daktari nje na hapohapo akamweleza kinachomsumbua.
Daktari akamtaka waende ndani ambako kuna vifaa. Daktari anasema, “Haya mzee tulia, nieleze tatizo limeanza lini na unajisikiaje ili nichukue maelezo na kubaini tatizo.”
“Tatizo? Tatizo gani?” eti kasahau. Lahaula walakuwata! Si hivyo tu, siku nyingine alikwenda akiwa ‘ameutwika’ akilalamika mwili unauma mno. Daktari akafanya kazi yake akampima kila mahali, lakini alibaini Bogi Benda alikuwa anasumbuliwa na uchovu wa mwili kutokana na ulevi.
“Samahani bosi, sijagundua tatizo lolote isipokuwa nadhani ni mchoko wa mwili kwa sababu ya mtungi mwingi,” alisema daktari. Bogi Benda akijua ameumbuka akachukua shati lake akafoka huku anageuza maneno; “Kwa hiyo nirudi ulevi wako utakapokuwa umeisha siyo?”
Kwa hiyo, haikuwa rahisi watu kujua ni wakati gani bosi wao ana busara na wakati gani ana akili chakavu. Mabosi wa aina ya Bogi Benda, yule mhusika mkuu katika katuni maarufu za gazeti la Daily News miaka ya 1980 iliyokuwa inachorwa na James Tumusiime, Mganda aliyekuwa anaishi Nairobi, wamejaa kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tazama, viongozi wa CCM wachovu kisiasa wanaokoroma bungeni, wamebebana, safari hadi Arumeru Mashariki kwa kampeni za uchaguzi mdogo – kama Bogi Benda – bila kujua wanakwenda kufanya nini.
Tazama, miaka yote CCM waliwaaminisha watu kuwa CHADEMA wanafanya ufisadi kutumia helikopta katika kampeni. Lakini, katika chaguzi ndogo za Kiteto na Igunga nao walitumia. CCM wakatumia helikopta tatu kwa ajili ya mgombea wao wa urais katika uchaguzi mkuu 2010.
Leo, eti wanaibana CHADEMA inafanya ufisadi kutumia helikopta Arumeru!
Bahati mbaya CCM wamepumbaza, wamewatia ujinga na kuwaloga watu kwa hirizi ya amani.
Tatizo la Arumeru, kabla na baada ya uhuru ni ardhi. Wameru walifikia mahali wakachanga fedha wakamtuma Japhet Kirilo kwenda Umoja wa Mataifa kudai ardhi yao.
Badala ya kuzungumzia hayo, mgombea wao anasema atapeleka maji ya bomba ili Wameru wasiwe na meno yenye rangi. CCM inaona hili ndio tatizo.
Halafu waziri usingizi akakusanya wazee kwa vijana akidai kapata bomu la kulipua. “Niseme, nisiseme,” aliuliza waziri usingizi na akajibiwa, “Semaaaaaaa.”
“Si mnawaona jamaa hawa (akionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA) wanaendesha harambee?” alihoji na umati ukajibu, “Ndiyoooo.” Akasema, “Wamekimbiwa na wafadhili Conservatives wa Uingereza kwa sababu Serikali ya Tanzania imekataa ushoga.”
Kwa waziri usingizi, CHADEMA kukimbiwa na wafadhili ndiyo tatizo la wakazi wa Arumeru. Pamoja na usomi wake na uzoefu wa miaka mingi serikalini, waziri usingizi huyu hajui kuwa chama kikiingia madarakani, hata marafiki hubadilika!
Mwingine, badala ya kueleza suala la ardhi akaenda Arumeru akaorodhesha ukoo wa Mwalimu, halafu akamtoa mmoja akisema “katika maisha yangu yote sijawahi kuambiwa huyu ni mtoto wa mwalimu wangu!”
Amezodolewa, amerudi Dar akilalamika ameaibishwa! Hivi alitaka upuuzi huo uaminiwe? Uchovu huu wa kisiasa ndio unachangia viongozi wakuu na hata wabunge kuzomewa. Ole wao!
 
Hapa walikuwa washapokea ngapi kutoka nje hata wakaamua kufanya harambee? Na hizo hela zilizopatikana hapa, kwa kiasi gani ni safi?

[h=2]Monday, April 12, 2010[/h][h=3]VICKY KAMATA ATUMBUIZA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA CCM[/h]


Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba(kulia) akiwaongoza wanachama wengine wa CCM kumpongeza msanii Vicky Kamata alipotumbuiza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni ya kukichangia Chama cha Mapinduzi kwa nia ya simu za mkononi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana jioni.Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Hapa Mheshimiwa Nape, kweli umefanya uenezi wa chama. Hongera kwa hilo. Naamini umeweza kuwaaminisha baadhi ya watanzania kile ulichomaanisha. Ila kwa weledi wa mambo (like I and I), duh!! unakazi kubwa ya kufanya. Hiv utatuaminisha vip kuwa hizo fedha za CDM ni haramu ili hali tunaju issue ya KAGODA (kampuni ya kimafia ya CCM) jinsi ilivyochota mabilion ya EPA kufadhili kampeni za Urais CCM? Je fedha hizo zilikuwa halali? Toa kibanzi kwenye jicho lako, ndo kisha utoe kwenye jicho la mwenzako. Ndugu yangu Nape, mzigo ulioubeba ni mzito kwelikweli!! CCM kutokana na makosa yake, historia yake na wimbi la mageuzi la kidunia imepoteza mvuto kwa vijana. Litambue hili na fanya kazi yako bila kukurupuka. Vinginevyo utaonekana kituko (kama kwenye ili) Inavyoonekana mnaiogopa CDM, ndomaana mnaipa umaarufu. Safisheni chama chenu bila uwoga, lazima mtakubalika. SHAULIYENU, CDM watawang'oa
 
Mimi wala sikuisikiliza hiyo show ya leo maana Nape namjua vizuri. nilisahau kumwambia Dada Fina. Tofauti ya Nape na wanasiasa wengine vijana kama Zitto au Mnyika

Nape huwa anatetea kile ambacho hata nafsi yake haikiamini. Ila kwa kuwa ni ajira yake lazima ajifanye anaongea kwa hisia. Ila ukikaa nae mkaongea kama washkaj, Nape anaichukia CCM ya JK kwa nguvu zake zote ila mambo ya mkate wa kila siku ndo yanasumbua.

Siwezi kumlaumu maana ni wengi huwa tunafanya kazi na mabosi tusiowapenda kwa style yao ya kazi au misimamo yao ila kwa kuwa ni ajira na ujira tunauhitaji, tunavumilia.
 
kweli ccm 2mekosa mwelekeo' huyu m2 2mempa hii kazi sijui 2liwaza nn!..tanzania kubadilika 2sahau, kama wanao tuongoza ndo typ za nape 2mepotoka m sure soon sudani kusini wata2pga gap!..siasa na viongoz vmefanya systm icorrupt tz!....
 
Tanzania ina hela tele

Waalimu na madokta walipwe.

Pia pension za wafanyakazi zirudiswe.

Nape acha porojo

mahela yapo watanzania, kwa nini tusiungane na kupanda maandamano na migomo??

Jamani twafa watanzania, uoga tuache. Tuandamane. Tuwasaidie CDM

Maana sisi watanzania tunaonyeshwa mwizi halafu tunakaa kimya wakati tunakufa kwa kukosa dawa na njaa
 
kuwa katibu mwenezi wa CCM inahitaji uwe na akili ya mvuta bange.
Na ndo maana anaitwa mtu wa PROPAGANDA na ORGANAIZATION avumilie mawe matusi na makombora na anatakiwa ajibu ili adui asisogee nani atamsahau yule Propaganda wa Saddam Hussein aliyesema watavibinua vifaru vyote na ndege za Marekani zitakapoingia Baghdad wakati walikuwa wameshaingia Mjini?
Nape amepunguza kasi ya SANGARA na M4C kabla ya vita yenyewe
Huyo ndio kamanda NAPE popote anafit
 
Huwa najiuliza sana sababu zilizopelekea kupewa hicho cheo, bado sijapata jibu.
Could it be kuna watu ndani ya CCM wanayo nia ya makusudi kabisa ya kuua chama? Hao watakuwa ni wanamapinduzi halisi. I salute them!
Moja ya sifa kupata uongozi CCM unapashwa uwe mbumbu, mnafiki,msanii na mbabaishaji, kwa sababu hiyo system ya utawala chini ya CCM haihitaji mtu makini kwani mtu makini atakua msumbufu na mdadisi kwa chama tawala.Tazama Mh.Rais JK ana maamuzi yoyote ya msingi katika jamii anayoyatatu mbali na usanii na kauli zinazokinzana.Hawa sio wanaotawala nchi nyuma yao mafisadi ambao ndio wameshikilia remote control na kuiongoza nchi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Shame on you!! Unafanya timing kwenye maisha yetu?? Na unadiriki kusema siasa ni timing,! Mbaya zaidi ukiwa ni kiongozi wa chama tawala? Kweli nimeamini umefungiwa duaniani na akhera.
 
Back
Top Bottom