Nape nchi hii ni yetu sote..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape nchi hii ni yetu sote..!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jambo1, Sep 18, 2011.

 1. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alisema: “..Haiwezekani CCM tukae kimya. CCM hatuko tayari kuona viongozi wetu wakidhalilishwa. Kuna vijana wameletwa kutoka mikoa mbalimbali na CHADEMA, hivyo nasi tutatumia vijana wetu kuwalinda viongozi na chama chetu na tusije kulaumiwa kwa litakalotokea..”
  Sasa tuambie kiongozi gani wa CCM aliyedhalilishwa...,na je uko tayari kubebaya damu ya wana-IGUNGA itakayo mwagika kutokana na kauli za uchochezi kama hizi..!
  Mnasisitiza Amani alafu mnaleta vijisababu vya kupoteza amani hiyo..!
   
 2. R

  Robert kivuyo Member

  #2
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jaman ccm yamekua hayo tena?badala mlinde aman mkijua kabisa nchi ipo mikononi mwenu mnachochea vurugu!ss damu ya wanaigunga ipo mikononi mwenu hata mkicngizia picha 2lishakwisha soma.
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  CCM maji ya shingo!ndo maana wameamu tumia kila namna jimbo libaki kwao!tumeni makini katika hili!haiwezekani kuhujumiwa kila kukicha!nguvu ya umma itumike endapo watahujumu kura za wananchi.
   
 4. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hacheni habari za NAPE jamii ishamuelewa yeye ni mtu wa aina gani, kuendelea kujadili nini NAPE anafanya na kusema ni kukosa umakini huyu ni sawa na mrema hana mbele
   
 5. N

  Ndumilakuwili Member

  #5
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana IGUNGA hebu fikirieni vizuri, kama Mungu wenu Rostam Aziz Kwenye kiti hicho cha ubunge kwa tiketi ya CCM ameona matatizo yaliyopo kwenye kiti hicho KUPITIA CCM sasa kwa nini msiachane na CCM mkachagua CHADEMA, Mkiendelea na wabunge wa CCM hapo Igunga mnatwanga maji kwenye kinu!
   
 6. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ulimi ulikiponza kichwa, wahenga walisema.
   
 7. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Wantu wa Igunga si wajinga, safari hii hawatomchagua mwakilishi toka chama cha magamba, hawatashiriki tena siasa uchwar.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCM si chama tena ni genge la wezi
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  NAPE ANAFIKIRI HII NCHI NI YA CCM,NASEMA HAKUNA KITU KAMA HICHO HATUTAKUBALI KUTISHIWA,KUNYNYASWA,KUBURUZWA nasema hivi NAPE wewew ni mtu wa kupita kama upepo unapopita,na hata mkiwaambia FFU wamalize watu kwa risasi,jua ya kwamba hata wewe utakufa tu hata kwa kuliwa na simba,MUNGU sio MWARABU anaehonga watu suti UTASHUDIA mambo yanavyogeuka.
   
 10. M

  MSEJA Member

  #10
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napeeeeeee! sema nipo! Kijana mwenzetu amefrastrate na amepoteza mwelekeo na hana jipya tena. Just imagine a young boy like Nape thinking okwadly like this it si shame Nape! Halafu anajifanya anauwezo wa kusafisha wanamagamba wote! kanafiki tu kanauendeleza. Igunga muaibisheni huyo pamoja na wanamagamba wote. Amepiga kelele kuzunguka Tanzania nzima mwisho amechukua gamba alivulia chumbani kwake kalivaa tena Pole NAPEEE! Just know Nape that HUNA JIPYA UMESHA ZEEKA KIJANA!
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Selective memory at its best. Hivi wewe hali ile ya kumwagia watu tindikali, kubaka msichana na hata kumdhalilisha mkuu wa wilaya unaona kwa standard ya Chadema ni vitendo vya kudumisha amani? Hebu tuondoleeni balaa yenu hapa!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Dah! ndiyo yamekuwa hayo tena ya jicho kwa jicho!!!? haya anzisheni umwagaji wa damu nchini mtaziona gharama za maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu.
   
 13. R

  Robert kivuyo Member

  #13
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaigunga,2tawashangaa sana kuruka majivu mkanyage moto,nyie wenyewe ni mashaidi ya maendeleo mliyonayo.Nikweli hapo mlipo kimaendeleo ni sawa?kama c sawa bac niwakati wa kuachana na siasa za kufuata upepo na ushawishi wa uongo na kujikomboa kifikra nk.CHADEMA TUKAZE BUDI TZ INATUTEGEMEA,CHADEMA UKOMBOZI DHAHIRI>TUNAWEZAAA,TUNAWEZAAAA.
   
 14. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Nape anatafuta umaarufu! Mimi nashangaa sana na sielewi anatoa wapi hii jeuri. Sitaki kuamini kuwa nafasi pekee aliyo nayo ya ukatibu mwenezi ndiyo inampa hii power.
   
 15. m

  migomo ya vyuo Member

  #15
  Sep 18, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape **** wewe mods ukipenda nifungie tuu lakini uvumilivu umeisha bora unitimue humu
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ccm wamegundua hilo jimbo halirudi tena mikononi mwao ndo mana wameanza kutapa tapa, Namchukia sana huyu kilaza Nape, ni mkuu wa mataahira!
   
 17. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,718
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Aah bongo hivi tukipata jimbo moja la igunga litasaidia nini pale gengeni?. nchi hii igawanyike kimajimbo tuwe na masenator ndio tutapata maendeleo. Tuwe na Jimbo kama Bukoba state, Mbeya State na Kilimanjaro state tuone kama huu upuuzi utaendelea.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Hali tete Igunga
  • Wabunge wa CHADEMA wasota Polisi

  na Mwandishi wetu
  Tanzania Daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  KATIKA hali inayotia shaka na kuzusha wasiwasi kwa wakazi wa Jimbo la Igunga, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza hali ya hatari na kuagiza vijana wake waliokuwa katika kambi za mafunzo kwenda jimboni humo kwa kile kilichodaiwa kulinda amani, huku kikisema kuwa kisilaumiwe kwa yatakayotokea kuanzia sasa.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema wamechoka na vurugu wanazofanyiwa na vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, na hawapo tayari kukaa kimya wakishuhudia ukatili huo.
  Alisema chama hicho kimeamua kuchukua hatua za kujilinda kwa kuwatumia vijana wake, ingawa alidai kwamba vijana hao hawataingilia kazi za Jeshi la Polisi.
  Nape alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu, Dar es Salaam.

  Katika wiki inayomalizika leo, CCM imejikuta katika mgogoro mkubwa Igunga, baada ya kutuhumiwa na CHADEMA na ikakiri kwamba inaandaa vijana katika makambi; mara kiongozi wake mwandamizi anayeongoza kampeni za CCM akafumaniwa na mke wa mtu; halafu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario, akafumwa na vijana wa CHADEMA akifanya mkutano na wajumbe wa CCM jirani na eneo la mkutano wa CHADEMA, akaondolewa kwa nguvu.

  Nape alisema CCM wamechoka kushuhudia vitendo vinavyokwenda kinyume cha sheria na maadili ya Mtanzania.
  Alisema tangu Septemba 9, mwaka huu kumekuwa na matukio ya udhalilishaji yakiwamo ya kubakwa na kupigwa kwa wanachama na viongozi wa chama hicho, hali inayoashiria kuvurugwa kwa amani kunakofanywa na kikundi cha watu wachache.

  Alisema: "Haiwezekani CCM tukae kimya. CCM hatuko tayari kuona viongozi wetu wakidhalilishwa. Kuna vijana wameletwa kutoka mikoa mbalimbali na CHADEMA, hivyo nasi tutatumia vijana wetu kuwalinda viongozi na chama chetu na tusije kulaumiwa kwa litakalotokea."

  Alitaja matukio ya vurugu kuwa ni kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali kwa kijana Mussa Tesha kulikotokea Septemba 9, mwaka huu alipokuwa akibandika picha za mgombea wa CCM. Aliongeza kuwa Septemba 11, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Michael Shija, alikatwa mapanga na kuibiwa simu na baiskeli yake.
  Mbali na matukio hayo, alisema Septemba 12, Mwalimu mstaafu Francis Msalika, alivamiwa nyumbani kwake saa saba usiku na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 alibakwa na kutupwa katika eneo la mto.

  Wabunge wa CHADEMA wakamatwa tena

  Siku moja baada ya Jeshi la Polisi wilayani Igunga kuwakamata na kuwaachia wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wabunge hao jana wamekamatwa tena na kuzuiliwa kwa kile kinachodaiwa ni maagizo kutoka ngazi za juu.
  Wabunge hao Slyvester Kasulumbai (Maswa Mashariki) na Suzan Kiwanga (Viti Maalumu) pamoja na Kamanda wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Anwar Kaswega, wanashikiliwa kwa tuhuma za kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario, alipokuwa kwenye shughuli za kiserikali katika Kijiji cha Isakamaliwa.

  Wakati Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Makao Makuu, Naibu Kamishna wa Polisi, Issaya Mungulu, akisema kukamatwa kwa viongozi hao wa CHADEMA ni sehemu ya upelelezi wao, Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) alisema polisi wamekataa kuwaachia wabunge hao kwa dhamana.

  Aliongeza kuwa polisi walisema wamewakamata wabunge hao baada ya kupokea maelekezo kutoka ngazi ya juu. "Sasa sijui ni nani, labda Stephen Wassira, nimempigia IGP Mwema hajapokea, nimemtumia ujumbe hajajibu. Kwa hiyo hatujui ni mkubwa gani," alisema Lissu.

  Alisema wabunge hao wanatuhumiwa kumpiga DC, kumvua hijabu na kumwibia simu yenye thamani ya sh 400,000. "Nimezungumza na Mkuu wa Operesheni Mungulu, akasema watawashikilia mpaka hapo watakapowapata wengine waliokuwepo kwenye hilo kundi," alisema Lissu.

  Akizungumzia tuhuma hizo, Tundu Lissu alisema kukamatwa kwa wabunge hao ni njama za kupunguza kasi ya kampeni za CHADEMA. Amesema wakati polisi na watu wote wamekisukumia chama hicho lawama, polisi hao hao wamepuuzia malalamiko yaliyotolewa na CHADEMA dhidi ya mkuu wa wilaya.

  Lissu alimtuhumu mkuu wa wilaya kwa kufanya mkutano wa kampeni kwa kuwahutubia wazee maarufu, viongozi wa dini na mabalozi wa CCM ili wasiende kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliokuwa ukihutubiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa.
  Alisema kanuni za maadili ya uchaguzi zinawakataza watendaji wa serikali kama wakuu wa wilaya kujihusisha kwa namna yoyote kuingilia kampeni au kukibeba chama cha siasa na kutumia gari na muda wa serikali kufanya kampeni.

  Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa, amesema CCM na polisi wanamlinda mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye anashiriki kuhujumu mikutano ya chama chake. Aliongeza kuwa polisi kama ni wakweli na watenda haki, walitakiwa kumkamata kiongozi huyo wa serikali badala ya wabunge wa CHADEMA ambao walikuwa wakipinga dhuluma wanayofanyiwa na mkuu huyo wa wilaya.

  Dk. Slaa alisema sasa watazunguka nchi nzima kutangaza uovu wa polisi na wa CCM wanaofanya kazi ya kuwakandamiza viongozi wa vyama vya upinzani na kuwataka Watanzania kukikataa Chama Cha Mapinduzi.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, amedai kuwa alikuwa na mkutano wa ndani na viongozi wa serikali ya kijiji, ikiwa ni sehemu ya kazi za kawaida za kiserikali na kwamba hakuwa na lengo la kuingilia mkutano wa CHADEMA.

  Aliwatuhumu wabunge hao kwa kumdhalilisha na kumtukana matusi ya nguoni, hali aliyodai kuwa imemfedhehesha sana.
  Habari za kuaminika zinasema kuwa sakata zima la tukio hilo lilianza baada ya msafara wa CHADEMA kufika katika eneo la kampeni saa 8:00 mchana na kabla mkutano haujaanza, Meneja wa Kampeni wa chama hicho, Sylivester Kasulumbai, aliarifiwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo alikuwa akifanya mkutano wa ndani na viongozi wa eneo hilo.
  Kasulumbai baada ya kusikia taarifa hizo, aliwaongoza viongozi wenzake hadi katika ofisi ya mtendaji wa kata kulikokuwa kunafanyika mkutano huo ambapo walihoji aliko mkuu huyo wa wilaya.

  FFU wenye silaha watanda

  Wakati Nape akitangaza hali hiyo, mjini Igunga, idadi kubwa ya askari polisi wakiwamo wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wametanda kila kona ya mjini hapa. Askari hao wakiwa wamevalia rasmi mavazi ya kazi, siku nzima ya jana walikuwa wakizunguka katika mitaa ya mji wa Igunga wakiwa na magari yao na yale yanayobeba maji ya kuwasha.
  Kuongezeka kwa polisi hao kumewatisha wakazi wengi ambao hawakuzoea hali hiyo, jambo ambalo limelalamikiwa na CHADEMA.Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa CUF, wameeleza kufurahishwa na ulinzi huo na wameishambulia CHADEMA kwa madai ya kuhusika na vurugu zinazotokea.
  Taarifa hii imeandaliwa na Joseph Senga, Irene Mark, Mustapha Kapalata (Igunga) na Bakari Kimwanga, Shilila Mzavah (Dar es Salaam).


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tulia mkuu, huwezi kufungiwa. Ungefungiwa kama ungemtukana hata kiongozi wa shina wa CDM lakini siyo wa CCM, hata akiwa mwenyekiti wa taifa!
   
 20. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tumechoshwa na uchochezi wa Tanzania Daima na kulia lia. Kama mlidhani hakuna ushindani wa haki si mngeacha. Kura hazitolewi kwa misingi ya huruma hata siku moja. Kazeni buti muuze sera. FFU wameletwa kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani amabvyo viko associated na CDM.
   
Loading...