Nape na wenzake Kupigwa 'stop' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape na wenzake Kupigwa 'stop'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maishamapya, Jul 29, 2011.

 1. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kundya ataka Nape,wenzake wapigwe 'stop'

  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza,Rajabu Kundya, amesema ziara zinazofanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nape Nnauye na wenzake katika mikoa mbalimbali nchini, zinapingana na taratibu za CCM.

  Kundya pia amesema kitendo cha viongozi hao kuwataja majina baadhi ya wanachama wanaotuhumiwa kwa mambo mbalimbali kinaleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho kinachotawala.

  Katika zira hizo mikoani, Nape amekuwa akifuatana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na wengine kadhaa.Akizungumza katika mahojiano maalum jana katibu huyo wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, alisema ingawa ziara kama hizo zingeweza kusaidia kuimarisha chama, lakini kutaja majina ya watu na kuwashutumu si sehemu ya kuimarisha chama bali kukibomoa.

  "Kama kuna mtu ambaye wanadhani ana tatizo kubwa ndani ya chama, utaratibu upo na wala si busara kumtaja katika mikutano ya hadhara, hili ni la kulisemea ndani ya vikao," alisema Kundya.Alisema taratibu za kusema zipo na zinatoa nafasi kwa mwananchama yeyote kuzungumza na hata kuwasema wenzake kupitia njia za vika ndani ya chama.

  Mtendaji huyo alisema kinachokifanywa na Nape na wenzake hasa kuwasema hadharani viongozi wanaotakiwa kujivua magamba, ni kukiuka taratibu. Alisema hata hiyo jambo hilo analiacha mikononi mwa chama, ili kiangalie namna ya kuwazuia viongozi hao ili wasiendelee kuvunja taratibu.

  Kwa kauli hiyo katibu huyo atakuwa anaungana na wenyeviti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja na Mkoa wa Dar es salaam John Guninita waliojitokeza kuwakosoa makada hao wa CCM.

  Source: Mwananchi.

  MY TAKE: Je, mkanganyiko huu wa viongozi wa chama cha magamba ni uthibitisho kuwa Nape hakutumwa na chama bali anafanya hayo kwa maslahi binafsi ya M/Kiti wa CCM Taifa kama ambavyo imedokeza hivi karibuni?
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hapo patamu tusubiri tuone nani ananguvu zaidi ya mwenzie maana leo hii kesho lile uhuni uhuni tu hakuna strategies za maana za kuendeleza nchi bali ni bulabula za kila siku na mipasho kama wanamziki wataarabu. sijui wamengeuka kuwa wana mziki wala sio wabunge au viongozi tunaotegemea wasaidie taifa kutoka hapa lilipo kwenda mbele zaidi
   
 3. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanaweja: hawa watavuana magamba sana tu
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 931
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndani ya CCM kila mtu ni mzigo Nape mzigo, Pinda ndo usiseme, Kikwete ndo kabisaaa, Sitta ndo haswa! Ndani CCM sasa nani ni nani. Njia ni moja tu wawaachie Magwanda nchi!!
   
 5. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu si unajua na wao wameanza kuiga kuvaa magwanda!!!
   
 6. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari nzuri kasoro TITLE YAKO HAIENDANI NA content mkuu.
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nape hakisaidii chama kwa sasa kwani hata hao mapacha wawili wakiondoka bado ccm ni chafu.

  juzi kati ccm ilivaa gamba lingine la kukumbatia posho
   
 8. A

  Aman Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm kweli wanafundishana uoga na unafiki,kwahiyo wanataka BELESHI ibadilishwe jina na kuwa LIKIJIKO LIKUBWA??Mtu kama ni mwizi ni mwizi!.thats it,Mapacha watatu ni MAJAMBAZI,and thats final,mtakaa kubembelezana mpaka lini.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Unajua CCM ni kama chama kichanga hivyo Nape anafanya kazi ya kukieneza ili kijulikane kwa watu Mbinu wanazo tumia hawa CCJ ni zile ambazo kama CCJ kingepata usajili basi wangezitumia na hapa hatujui la mbele kwa nini CCJ tu ndiyo Wainadi leo CCM ? JK asipokuwa makini CCM inakufa mara moja maana hawa jamaa wanajinadi kwa watu, wanajijenga ili hapo watakapo sema CCJ oyeeeeee watu waitikie pasi tatizo
   
 10. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hii kali Mkuu!
   
 11. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nape vuvuzela
   
 12. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Asante! Nilisahau hiyo alama (?) kwenye avatar yako
   
 13. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbona hata wao hawampingi nape na wenzake ndani ya chama wanatumia vyombo vya habari, naona huu ni muendelezo wa kugombania madaraka ndani ya CCM kati ya lile kundi maarufu la EL na Kundi la CCJ ambalo liliponea chupuchupu kufukuzwa sasa wanalipiza kisasi kwa kasi zaidi. Ila sasa hawa CCJ hawana watu mikoani wala ndani ya serikali na EL alipandikiza vibaraka wake kila kona ya CCM na Tanzania wakati akiwa PM.

  Rais mwenyewe pia ajitambui ndio maana haya yote yanafanyika, lakini pia hili kundi la wakina Nape nalo kama wahajui walifanyalo maana kama wangejipanga vizuri wao ndio walikuwa katika nafasi nzuri ya kupindua hii serikali dharimu kama kweli wao sio sehemu ya udharimu huu.
   
Loading...