NAPE na SITTA wakalia kuti kavu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NAPE na SITTA wakalia kuti kavu CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Nov 3, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,234
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  HALI ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), inazidi kuwa tete baada ya wenyeviti wa mikoa wa chama hicho tawala, kupitisha azimio la kutaka Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), atimuliwe uanachama kwa madai kuwa amemtukana, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Mbali na kutaka Sitta atimuliwe, baadhi ya wenyeviti hao wametaka Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, adhibitiwe kwa madai kuwa amekuwa akitoa matamko ya upotoshaji yanayoenda kinyume na maazimio ya NEC.

  Wakati kundi la wenyeviti hao likimshambulia Sitta na Nape, kundi lingine lililoongozwa Mwenyekiti wa mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, liliibuka kumtetea Nape na Sitta, hali ambayo ilionyesha dhahiri kuwapo kwa makundi mawili yanayosigana ndani ya viongozi hao wa CCM mkoa.

  Hali hiyo ilitokea jana katika kikao cha wenyeviti wa mikoa wa CCM, kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

  Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti CCM Taifa, Pius Msekwa, kwa niaba ya Mwenyekiti, Jakaya Kikwete, zilisema kuwa jina la Sitta ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu, pamoja na Nape, lilitawala kikao hicho.

  Kwa mujibu wa habari hizo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, ndiye alianza kurusha mawe dhidi ya Sitta akidai kuwa Spika huyo wa zamani amemtukana Rais Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu (CC).

  Akifafanua hoja yake, Mgeja alisema Sitta alimtukana Rais Kikwete na wajumbe wa CC, kupitia kipindi cha dakika 45, kinachorushwa na kituo kimoja cha TV, akilalamika kwamba waliweka kigezo cha jinsi kwa shinikizo la mafisadi kumuengua kwenye kinyang'anyiro cha uspika ambacho kilijenga mazingira kwa Mama Anna Makinda kupita kirahisi.

  Chanzo chetu cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kilisema kuwa Mgeja alisema anashangazwa na ukimpya wa chama kutochukua hatua dhidi ya Sitta na kupendekeza kuwa afikishwe na kuhojiwa kwenye vikao vya chama na asipotoa maelezo ya kujitosheleza, atimuliwe.

  Mbali ya kumvaa Sitta, Mgeja pia alimshambulia Nape kwamba amekuwa akitoa kauli za kupotosha dhidi ya mkakati wa kujivua gamba wa chama kwa kuwalenga watu asiowataka.

  Ukimwacha Mgeja, baadhi ya wenyeviti wengine waliounga mkono hoja hiyo na majina ya mikoa yao kwenye mabano ni John Guninita (Dar es Salaam), Clement Mabina (Mwanza), Onesmo Ole Nangolo (Arusha), Nawab Mulla (Mbeya) na mwenyekiti wa mkoa wa Mtwara.

  Kwa mujibu wa habari hizo, wenyeviti hao kama vile walipangwa, walimwangushia lawama nyingi Nape kuwa amekuwa akipotosha chama kuhusu dhana ya kujivua gamba kwani hakuna maazimio ya NEC yaliyotaja majina ya watu wanaopaswa kujiuzulu.


  CHANZO: Tanzania Daima
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  A house that divides against itself can not stand. CCM's growing internal rows show that the long serving party is on the verge of going to pieces. I do pray day and night that those disputes soar to an extent of sundering the party's elite partisans so that to ease the exercise of removing them out of power.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,616
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vita vya panzi nifuraha kwa kunguru. Waendelee kurumbana!
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,228
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  kila amuzi la ccm linajenga anguko lake
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,217
  Likes Received: 4,110
  Trophy Points: 280
  Acha wavurugane maana woote wamekula hadi wamevimbiwa sasa hawamjui mwenye njaa....tutasikia mengi sana miaka 3 hii.......na haata kushikana mashati na mwendo wa sumu kali....
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Nape si alisema wanaompinga ni waasi?
   
 7. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,741
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wote hawana tofauti, majizi, majambazi, wauaji, mafisadi na watenda maovu ya kila aina. Watamfukuza nani wamwache nani? Kama ni kufukuzana waanze na mwenyekiti wao kwanza.
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 15,872
  Likes Received: 3,139
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa, hebu check maamuzi haya.,
  1. Kura za maoni 2. Kujivua gamba 3....
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,848
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Sitta kawakaba koo sana akina Lowassa, na kama kweli watamvua uanachama, basi mwisho wa CCM na anguko lao limetimia
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mnafiki six ataenda wap? Anywy waache wamalizane wao kwa wao sie tupite! Wafanye fasta...
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,173
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Waache wafu wazike wafu wao uaneni kbs,mmeshindwa kuendesha nchi mnabakia na majungu tu.
   
 12. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,127
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Naitakia magamba anguko njema tafadhali ongezeni bidii zaidi!!!!!!
   
 13. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 7,148
  Likes Received: 4,702
  Trophy Points: 280
  Ok....tufanye hatufahamu kitu kuhusu mgogoro wa kimaslahi au kundi walilmo hao watoa shinikizo waliotajwa na tujikite katika kutafakari madai yao kwa kifupi sana:
  Je, aliyoyaongea Sitta yalitokea au hayakutokea? Wanatakiwa wakanushe kwanza tena kwa vielelezo then ndiyo watoe mapendekezo.
  Kinyume na hapo watakuwa nao pia wamemtukana.
  Kuhusu Nape kinachotakiwa kufanyika ni kum-prove wrong kwanza, badala ya kulalamika kuwa anakigawa Chama kwa kauli zake, je kama zina ukweli?

  Najua ukweli ni rafiki atembeaye Uchi hakuna miongoni mwetu akikutana naye hadharani atamfuata na kumsalimu kwa furaha bali tutafanya jitihada kumkwepa.

  Hicho ndicho kinachotutesa ndani ya CCM.
   
 14. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,733
  Likes Received: 858
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Ila nilifundishwa pilipili usiyoila inakuwashia nini! Ngoja nikae kimya mwana kwetu maana haya mambo ni yao CCM
   
 15. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM kilishakufa sasahivi mm naoan ni mzimu ndo unaoparate,kam ni kuvua magamba wote mle magamba sasa nanai aondoke na nani abaki?Nape yeye alipoambiwa wewe mwenezi akadhani maana yake aongee bila data wala research
   
 16. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  leo ndo nimedhibitisha tarehe zako za MP huwa zinaanza leo, UR TOO MUCH APHRODIASITIC
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Wengine tulisha sema hakuna watakacho amua kitakacho wasaidia zaidi kitakuwa on our favour ili unabii utimie tena wanvyokazana kuamua ndivyo wanavyo zidisha speed ya kutimiliza huo unabii wa anguko lao utimie mapema....
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,942
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  CCM ni wahuni tu kama wahuni wengine tofauti yake wao wanafanyia uhuni kwenye ukumbi wa karimjee huku wamevaa tai,
  hawataki kuambiwa ukweli kwani ni uongo kuwa kanuni zilipindwa ili apatikane Makinda? imeandikwa wapi spika anapatikana kwa vigezo vya kijinsia?
  Na huyo Nape tulimwambia amewekwa pale kama chambo kuna siku atatuelewa tu atakapoanza kulia kulio cha mbwa mdomo juu.
   
 19. m

  mharakati JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,276
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  utoto huu CDM watakuja pata haya wakishindwa tu uchaguzi wa 2015....tafuta wachawi itaanza haraka bora CCm wameweza kuvumiliana kwa miaka 30+
   
 20. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CCM kamwe haiwezi kupona hata kama akina Sitta watapatanishwa au kufukuzwa. Hii ni kwa sababu mfumo unao endesha CCM hauewzi kuikoa. Huo sio uchulo kwa chama hiki ila ni kanuni ya msingi ya Historia katika kuanguka kwa dola/taasisi. CCM imeruhusu matabaka katika chama chake hivo lazima itapambana na mgawanyiko kila siku. Kupata uongozi lazima uwe na fedha sasa fedha zinatofautiana kuna matajiri kuna wakawaida na wakati. Wengi wanatoa rushwa ila wanazidiana katika viwango. Deals ziimekuwa mtaji wa kutafuta pesa za uchaguzi. Swali kuu ni, je kila mwana CCM ana nafasi sawa? Jibu ni hapana. je wangapi ni vibosile na wanapesa ndani CCM ? Jibu ni wa cache saaaana kulinganisha na wanachama wao millioni 5. Kwa hiyo CCM imebadilika na kuwa kama chama cha kisultani. Je wanachama watakubali? Haitawezekana so death is inevitable for CCM. Badilini mfumo au kubali kifo.
   
Loading...