Mzee umesahau kwamba kila hoja inayotolewa na cdm siku hizi inapingwa na Spika wa Magamba? Hebu tukumbushe suala la Waziri Mkuu, Pinda kulidanganya Bunge limefikia wapi? Hongera Zitto kwa kuonesha mfano wa kuigwa!Zitto unatushangaza sana kuhusu suala lako la Posho yako kupelekwa KDI. Kama wewe unadhamira njema na si kutafuta umaarufu na ghiliba kwa Watanzania kwa nini usingepeleka hoja binafsi ya kubadili sheria bungeni ili muifute? Sheria huvunjwa kwa kupeleka Mswada bungeni sasa kijana unategemea kweli utaivunja kwa kumwandikia spika barua au kwa kuongea mitaani na barabarani. Zitto kuwa makini katika hili watu wanaokuheshimu na kukuona wewe kama mtu makini wanakudharau.
nimesoma Mpango wa maendeleo wa miaka mitano: "THE TANZANIA FIVE YEAR DEVELOPMENT PLAN 2011/12-2015/16".
nimevutiwa na kipengele hiki kizuri ukurasa wa 15:
On the expenditure side, containing Government expenditure will contribute towards ensuring that macroeconomic stability is maintained. This will require enhancing the expenditure control and accountability as well as ensuring value for money. One important area of expenditure is wages and salaries. Consolidation of most of the fringe benefits such as housing, transport and allowances into salaries and wages will be one of the ways of creating an appropriate incentive structure. Sitting and travelling allowances currently create a perverse incentive's structure, and will need to be rationalized or removed.
Najiuliza ina maana Mustafa Mkullo na ofisi ya bunge hawajui kwa undani mpango huu na mikakati iliyomo ndani yake. kama Mkullo anajua kwa nini anasema posho zitaendelea kutolewa. anataka kutuambia kilichomo kwenye mpango huo ni kiini macho. au mpango umeandaliwa ili kukidhi matakwa ya wahisani kumbe hatuna utashi wa kisiasa.
Nawapongeza chama cha chadema (wakiongozwa na Zitto Kabwe) kuanza kutekeleza kwa vitendo mpango huu ambao ni brand new. Hongera sana CHADEMA.
jamani mimi naendelea kujiuliza kwa nini serikali inapingana na maandiko yake yenyewe..... ukisoma paragraph hapo juu utaona kwamba suala la sitting allowance linatakiwa liondolewe.. sasa kwa nini Mkullo ang'anganie!!.
safi sana vijana inaelekea mnaanza kuwa na akili kidogo. sasa nataka muendelee kujadili kama kweli wanauchungu na hizo pesa kwa nini wawe na uchungu na hizi na wasiwe na uchungu na milioni 7 isiyotozwa kodi wanayomlipa Slaa. Acheni kuwa makasuku hapa hakuna nia yeyote njema zaidi ya kutaka umaarufu. lakini kwa miaka hii yote mitano iliyopita alipokea. Amekumbuka nini mwaka huu? I know Zitto vizuri toka nikiwa naye UDSM. He is the same hajabadilika ila kwa ninyi msiomfahamu endeleeni kula chaka.