Nape majuzi alikuwa nyumbani kwao. Katika pita pita akakutana na Makonde mmoja aliyekuwa anauza vinyago. Alivutiwa sana na kinyago kimoja kilichokuwa kinafanana na panya, na kilichochongwa kwa ustadi kiasi ya kwamba hata manyoya ungedhani ni ya panya; wacha kichwa, miguu, mkia na vingine. Akamwuliza huyo Makonde anauzaje hicho kinyago. Akaambiwa ni shillingi mia tano na mtu akisha kinunua hakirudishwi. Nape akaona hiyo ni bei poa kwani ni kama bei ya soda. Alilipa akaondoka nacho.
Hajafika mbali, maajabu yakaanza kutokea. Kila aina ya panya wakaanza kujitokeza majumabani , vichakani, mashimoni ana kwingine wakimfuata Nape. Akaingiwa na woga na kuanza kukimbia. Lakini wapi. Panya waliongezeka na kuongeza kasi yao. Woga ulimzidi huku akijiuliza afanye nini.
Hapo alipokuwa ni karibu na Mto Ruvuma. Basi akakikimbia kuelekea huko na panya walikuwa bado wanamfuata na wakiongezeka. Kufika kwenye kingo za mto huo mkubwa, ailikitupa kile kinyago majini na hapo ndipo maajabu yalipotokea. Wale panya wote waliokuwa wakimfuata, walikifuata kile kinyago huko majini, wakazama nakufa.
Kuona hayo, Nape ilikuwa ni kama amepatwa na wazimu. Aliondoka kwa kasi mithiri ya farasi, akielekea kwa yule Makonde. Mara kufika Makonde akawa mkali.
Nilichema chirudishe
Tulia Baba. Una kinyago kinachofanana na Dr. Slaa?
China. Tena nakwambia china kabisa
Nape alizimia papo hapo.