Nape na kinyago cha panya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape na kinyago cha panya

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by ISOPOWER, Jun 8, 2012.

 1. I

  ISOPOWER Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nape majuzi alikuwa nyumbani kwao. Katika pita pita akakutana na Makonde mmoja aliyekuwa anauza vinyago. Alivutiwa sana na kinyago kimoja kilichokuwa kinafanana na panya, na kilichochongwa kwa ustadi kiasi ya kwamba hata manyoya ungedhani ni ya panya; wacha kichwa, miguu, mkia na vingine. Akamwuliza huyo Makonde anauzaje hicho kinyago. Akaambiwa ni shillingi mia tano na mtu akisha kinunua hakirudishwi. Nape akaona hiyo ni bei poa kwani ni kama bei ya soda. Alilipa akaondoka nacho.  Hajafika mbali, maajabu yakaanza kutokea. Kila aina ya panya wakaanza kujitokeza majumabani , vichakani, mashimoni ana kwingine wakimfuata Nape. Akaingiwa na woga na kuanza kukimbia. Lakini wapi. Panya waliongezeka na kuongeza kasi yao. Woga ulimzidi huku akijiuliza afanye nini.

  Hapo alipokuwa ni karibu na Mto Ruvuma. Basi akakikimbia kuelekea huko na panya walikuwa bado wanamfuata na wakiongezeka. Kufika kwenye kingo za mto huo mkubwa, ailikitupa kile kinyago majini na hapo ndipo maajabu yalipotokea. Wale panya wote waliokuwa wakimfuata, walikifuata kile kinyago huko majini, wakazama nakufa.

  Kuona hayo, Nape ilikuwa ni kama amepatwa na wazimu. Aliondoka kwa kasi mithiri ya farasi, akielekea kwa yule Makonde. Mara kufika Makonde akawa mkali.


  “Nilichema chirudishe”

  “Tulia Baba. Una kinyago kinachofanana na Dr. Slaa?”

  “China. Tena nakwambia china kabisa”

  Nape alizimia papo hapo.
   
 2. kijembeee

  kijembeee JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 411
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  interestin
   
 3. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aisee! Lugha ya picha hiyo. Atakoma kuwaita wenzie vinyago!
   
 4. KML

  KML JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  we mkaleee
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Alitaka kinyago cha dr. Slaa aende nacho jangwani jana ili apate wafuasi wengi. Mkuu uko creative kinouma
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hahahaaaaaaaaaaaaaa aisee angepata cha dr Slaa naona angekitafuna akimeze ili wafuasi wa Dr Slaa wamfate yeye
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kama mpiga filimbi wa hamelin
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nimeipenda sana hii
   
 9. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwikwikwiiih!the funniest and the finest of the week.
   
 10. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,101
  Likes Received: 7,351
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa nasikia ni wa Kusini, so hao Panya nasikia kwao ni mishkaki poa sana


  Why alikua anawaogopa??
   
Loading...