MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
CCM kupitia makada wake (comrades) itaendelea kutoa somo kwa wapinzani mpaka pale watakapopata uelewa mzuri kwa nini CCM ni chama ambacho katika utafiti uliofanywa mwaka 2016 kimeshika nafasi ya 43 kati ya 210 ya vyama vilivyoko madarakani katika vigezo vya utaratibu wa kuwapata viongozi ndani ya chama, kubadirika kulingana na mazingira/vizazi na pia jinsi chama kinavyosimamia serikali.
Ukitaka kusoma zaidi kuhusu utafiti, gonga hapa, Utafiti: Ubora wa vyama vya siasa duniani, CCM yapata nafasi ya 43 kati ya 210
Wanazi wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA walikuwa wanashangilia sana wakati Nape Nnauye na Hussein Bashe wanaisurubu serikali bungeni na kwenye mitandao ya kijamii mpaka baadhi yao wakawa wanawaita mashujaa huku wengine wakiwaomba wajiunge na CHADEMA. CHADEMA hawakujua walichokuwa wanakifanya ni sawa na kutengeneza silaha ili ukuangamize wewe mwenyewe!
CHADEMA hawakufahamu kuwa moja ya nguvu ya CCM ni makada wake kuambiana ukweli bila unafiki kiasi kwamba kwa mtu asiyeifahamu CCM anaweza kudhani kuna mgawanyiko kiitikadi au kuna mpasuko lakini linapofika suala la kutetea maslahi ya chama hushikamana na kuwa wamoja. Hata kwenye vikao vikuu vya CCM kama Halmashauri Kuu huwa wajumbe wanasurubiana kama wewe ni mgeni unaweza kudhani kuna mgawanyiko.
Hata Edward Lowassa baada ya kuimarisha 4U Movement na Friends of Lowassa aliamini angeweza kuigawa CCM katika Uchaguzi Mkuu 2015 baada ya kuhama CCM na kuwaahidi CHADEMA kuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti wa mikoa wa CCM zaidi ya 22, Wenyeviti wa wilaya zaidi ya 80 na wakuu wa wilaya lakini kilichoshangaza baada ya kuondoka CCM, alifuatana na genge la wachumia tumbo wachache wasiozidi kumi ambao wengine wameanza kurudi CCM huku vijana wake wa karibu kama Hussein Bashe wakibaki CCM ili kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola.
CCM huwa ninaifananisha na nchi ya Israel inavyopambana na kikundi au nchi ambazo inadhani zinahatarisha usalama wake. Wanasiasa wa Israel huwa wanaisurubu serikali bungeni unaweza ukadhani kuna mgawanyiko au mpasuko ndani ya nchi lakini linapokuja suala la kiusalama huondoa tofauti zao zote na kuwa wamoja katika mapambano mpaka ushindi.
Uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 umeendelea kudhihirisha umoja wa CCM pale Nape na Bashe walipopanda majukwaani kuwaonyesha wapinzani kuwa wao kuwa CCM sio kama wafikiriavyo.
Alianza Nape Nnauye kwa kuwaambia CHADEMA wasipoteze muda wao kudhani ataihama CCM bali wajenge chama chao chenye viongozi walewale, siasa zilezile na mbinu zilezile.
Ukitaka kusoma zaidi alichokisema Nape kuhusu CHADEMA, gonga hii thread,
Nape Nnauye: CHADEMA acheni kuhangaika, siwezi kuhama CCM
Baada ya siku moja akaibuka Bashe na kuwaambia wana CCM wasiwe wanyonge na kuruhusu kushambuliwa na wanaCHADEMA bali wajibu mapigo kwa sababu hata vyombo vya dola viko chini ya CCM lakini kikubwa zaidi watawanyoa CHADEMA kwa chupa kupitia sanduku la kura.
Ukitaka kusoma alichokisema Hussein Bashe kuhusu CHADEMA, gonga hii thread;
CHADEMA watoa sauti ya Hussein Bashe akiwahimiza makada wa CCM wawapige CHADEMA
Mzee Kinana ambaye kila siku walikuwa wanaaminisha wafuasi wao eti yuko kwenye kifungo cha ndani (kizuizini) ndio maana haonekani au hasikiki aliamua kuwafuata huko huko kwenye ‘’ngome zao’' Arusha na Hai ili kuwachapa viboko vya kisiasa. Madhara ya viboko vya Kinana yameifanya CHADEMA kutoambulia hata kata moja.
Wakati CCM wakisurubiana kabla ya uchaguzi na kushikamana wakati wa uchaguzi, vyama vya upinzani nchini hufanya kinyume chake. Wapinzani huwa wamoja kabla ya Uchaguzi lakini huanza kusurubiana wakati wa Uchaguzi. Hawawezi hata kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja katika kata, jimbo au Taifa.
Kama mazingira yataendelea hayahaya mpaka baada ya 2020, siwezi kushangaa kuona idadi ya madiwani na wabunge kutoka kambi ya upinzani ikipungua kutoka idadi ya sasa.