Nape, Mwigulu, Juliana na Mwampamba ndio wanaokidhalilisha na kuitia aibu CCM!

Ndugu wana jf
Leo ni siku ya kwanza baada ya kikao cha wenye nchi kumalizika [yaani ccm] walikuwa wanajadili jinsi ya kututawala milele [mada ya kufa kwa ccm haitakaa iwe ajenda milele], najua Ndugu zangu Mh Mwigulu na Mh Nape sasa wanapata kikombe cha chai na mazagazaga ya kutosha huku wakiangalia simu zao aina ya Blackberry na kuperuzi issue tofauti [hivi unafikiri ukiwaambia kuwa yupo Mtanzania leo anakufa kwa njaa unafikiri watakusikiliza wakati wao meza imejaa na hakuna pa kuweka vitu, tena hiyo ni Asabuhi bado mchana na jioni].

Mashabiki wa ccm lazima waje na kejeli za aina yake [hizo mimi sizijali wala hazininyimi usingizi] kwani wanadhani kwao Tanzania hii wana hati miliki na wao ndio wanatakiwa watawale milele[Akili za mwendawazimu ndo huamini haya]. Machungu ya Watanzania yanazidi kupanda kila kukicha maana ccm ni kama UKOO WA PANYA kupata msafi ni hakuna wote ni wale wale tu.

Hebu tizama hizo picha kwa umakini wa hali ya juu, unaweza sema hawa ni watu wa aina mbili yaani mmoja yupo Tanzania mwingine yupo Ulaya, hadi watoto wadogo wamepoteza matumaini kabisa!!. Ukitizama Doctor aliyesoma zaidi ya miaka 7 baada ya kidato cha 6 leo hii posho yake kwa siku ni sh 10,000/= na Mbunge ni zaidi y ash 200,000/= kweli hapa kuna usawa!. Unajua lazima tuwe wakali na haya yanayotokea Tanzania ila tukiwaacha ccm wajifungie wenyewe ndani ya Bunge hakika wataiuza nchi [ kumbuka tu juzi juzi hapa walibaki wenyewe Bungeni na kuamua kuweka kodi ya simu card tena sh 1000 kila mwezi kwa mlala hoi ili tu wapate mahali pa kuchota wakiishiwa mifukoni mwao! [ni tama tu inawaendesha hakuna aliye na nia njema na mlalahoi wote ni wale wale tu!].

Lazima kila mwenye akili timamu awaandame ccm kwani nani mwenye Serikali? Ukiona kiongozi wa ccm awe mbunge, Waziri ama kiongozi wa kichama akikinyooshea kidole chama chochote cha upinzani na kudai ndo chanzo cha hali Fulani mbaya nchi ! hapo wenye akili kubwa tunajua anatafuta jinsi ya kukwepa Aibu hiyo [ hivi ndani ya nyumba Baba akisema no! nani atabisha?]sasa hawa Magamba wanajitetea nini? Wao watafune nchi hadi mifupa leo wanasingizia nini?.

Ndugu yangu mimi na wengi wenu ambao mnasoma hii thread tunahali mbaya[usibishe wakati hata mchana leo hujui ule nini?] na wenye nchi yao juzi juzi walikuwa Dodoma [kwani wewe ulialikwa? Kama haukualikwa jua wewe ni kibaraka tu ndani ya chama huna lolote mkuu (samahani ila natoa msisitizo tu) hivyo wao wakiamua wewe lazima ufuate ukikataa basi ni kipigo tu yaani utapigwa tu]. Hatuna budi kufanya maamuzi ya kujinasua kwenye hili ndimbi la umaskini wa kujitakia maana hakuna saye taka aishi vizuri sasa na uwezo wa kufanya hivyo tunao, hivyo basi sema NO NO NO NO NO kwa hawa wenye nia ya kutawala nchi hii milele. Kumbuka kuzaliwa maskini sio kosa kosa kufa huku ukiwa maskini na fursa zipo [Usilie mdau fanya maamuzi sasa haujachelewa!!!!!!?].

Asante, nawakilisha.
 

Attachments

  • 944644_10151627001253303_694538429_n.jpg
    944644_10151627001253303_694538429_n.jpg
    28.3 KB · Views: 102
  • 945730_10151577133583303_52546418_n.jpg
    945730_10151577133583303_52546418_n.jpg
    31.3 KB · Views: 109
  • 1095093_10151618706373303_1941204958_n.jpg
    1095093_10151618706373303_1941204958_n.jpg
    33.2 KB · Views: 105
  • 1229951_10151644164543303_349859481_n.jpg
    1229951_10151644164543303_349859481_n.jpg
    19.4 KB · Views: 106
  • HADI MTOTO KAKATA TAMAA.jpg
    HADI MTOTO KAKATA TAMAA.jpg
    8.1 KB · Views: 266
Hizi picha sio za tz naona kijana upo field ya journalism? Sasa unajifunza kuandika makala?
 
CCM ni mabingwa sana wa kujifanya kuwa hawapangiwi rafiki, na drama nyingine za kibabe za enzi za ujamaa...Ila very soon dunia itawalewesha mara hao comrades wenu wenye mirengo kigaidi, kidini, na kiharamia watakapoamua beba bendera za tanzania kuteka meli za Israel,US, Russia, China...UK...etc au hata kufikisha silaha au kushambulia kabisa...nadhani hapo ndipo mtapata fahamu ...


So far meshaingia ktk deep water huku mkiogelea kwa mtumbwi wa mtoni.....nadhani Membe ukiwa hai utaenda walilia unaowajibu kwa kiburi kuwa hampangiwi marafiki.

Siku hayo mataifa yatanuswa na maishu ya kigaidi kwa bendera yetu..israel ,urusi, China..watawafumua hadi magamba mnaouza unga, mnafadhilia uuzaji wa tembeo haramu, hadi nyie mnajificha ktk umoja wa Wahuni wa africa wenye milengo ya kiislam na kijamaa....hadi hapa US walishaaitawala ikulu yetu kwa isku kadhaa....siku watapata gia ...ole wenu....

modes tafadhani msiwe na haraka kuindoa
, hii ni fundisha kwa taifa kuwa watu watabeba bendeara zetu na kutupeleka pabaya kwa mataifa serious tukashuhudia walichokipata talibani, Idd amini etc.
 
Dunia kuna watu na viatu, hivi hata wewe mwenyewe ulichokiandika sijui kama unakielewa.

Usipende kuingia JF huku umekunywa viroba vya ZED.

Hebu jisome ulivyoandika.
 
Dunia kuna watu na viatu, hivi hata wewe mwenyewe ulichokiandika sijui kama unakielewa.

Usipende kuingia JF huku umekunywa viroba vya ZED.

Hebu jisome ulivyoandika.
Tunakujua,kuna vitu ukivisoma humu huwa akili yako inadata sana....huwa uantupia matusi y akujifariji huku ukiwa na hofu kubwa sana.Sijui kwanini umeka mileage kubwa sana ktk vitu hatari kijana.Nilipoandika kuhusu ikulu kuwa uchi kwa muda wamarekani wakipepo Dara..ulianza na matusi mengi sana ila wenye kaili walielewa..Sasa ktk hiyo ziara wamarekani wana informationza kutosha kujua meli yetu ikihataraisha mataifa yao nani ktk nchi hii anahusika na kigeugeu km Idd Amin.....huw ahawachelewi mfuat kwa makombora km si kumnyakua km noriega.
 
Weka simu yenye Internet mbali na Mlevi...umeshasahau yaliyompata Dr.HK
 
Weka simu yenye Internet mbali na Mlevi...umeshasahau yaliyompata Dr.HK

Haha...watu wa buku saba wengi ni hopeless sana...Ndio maana hata JK huwa anawashangaa na kuamua wakaubalia CDM mambo yao..halafu baadaye wanakuja juu...Sijui nini ch ajabu hapa...Irani walirusha bendera yetu akina membe wakajibu kwa dharau km mhongo.....sasa imeshikwa meli na bangi...soon hao wanachama wenu wanaodhani wanapiga mishemishe kwa maslahi ya chama...watajikuta wakilazimisha na hao maharamia au hata maharamia kutumia bendera na meli zenye usajidili wa nchi hii kwa issue ya kigaidi....Na ni wazi inteligensia ya marekani na israeli wanwajua watanzania wote wenye asili za nchi za kigaidi walivyojiachia ktk CCM ...hapo ndipo dua la watanzania litakapofika .....
 
Haha...watu wa buku saba wengi ni hopeless sana...Ndio maana hata JK huwa anawashangaa na kuamua wakaubalia CDM mambo yao..halafu baadaye wanakuja juu...Sijui nini ch ajabu hapa...Irani walirusha bendera yetu akina membe wakajibu kwa dharau km mhongo.....sasa imeshikwa meli na bangi...soon hao wanachama wenu wanaodhani wanapiga mishemishe kwa maslahi ya chama...watajikuta wakilazimisha na hao maharamia au hata maharamia kutumia bendera na meli zenye usajidili wa nchi hii kwa issue ya kigaidi....Na ni wazi inteligensia ya marekani na israeli wanwajua watanzania wote wenye asili za nchi za kigaidi walivyojiachia ktk CCM ...hapo ndipo dua la watanzania litakapofika .....

calm down dude, who is chasing you?
 
Vijana hawa, Nape, Mwigulu, Juliana na Mwampamba kwa sasa ndio vijana wanaoidhalilisha na kuitia aibu CCM. Vijana hawa wamepewa uhuru mkubwa wa kusema na kutenda lolote ndani ya CCM kana kwamba hakuna watu wa kuelekeza na kuwashauri mambo ya kusema na kutokusema au mambo ya kufanya au kutokufanya. Vijana hawa wakifungua midomo wanaongea mambo ya hatari sana kwa mustakabali wa chi yetu. Naweza kusema bila woga kuwa hawa ndio watakuwa chanzo cha kuvurugika kwa amani na usalama wa nchi hii. Wakati mwingine huwa napata shita kuamini kama chama hiki kina mwenyekiti anayeona hatari inayoletwa na vijana hawa au anaifurahia hali hiyo na hivyo naye ni sehemu ya uchafu huu unoenezwa na vijana hawa.

Vijana hawa kwa sasa ndio wanaoeneza chuki za ukabila, udini na ukanda.Wameacha kabisa kuhubiri sera za CCM wamegeukia mambo hayo hatari. Wao kwa akili zao finyu wanadhani wanaidhoofisha CHADEMA bila kujua kuwa wanaidhoofisha nchi kwa ujumla. Bahati mbaya sioni mtu mwenye busara ndani ya CCM akiibuka kukemea mambo hayo.

Wakati Fulani CCM ilipoona inazidiwa na CHADEMA ikawa inatumia polisi kusamabaratisha shughuli za CHADEMA. Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akawaambia CCM kuwa CHADEMA inafanya siasa kwahiyo na CCM nayo inatakiwa kufanya siasa si kuwazuia CHADEMA kufanya siasa. Mwanzoni walimpinga wakisema alipaswa atoe ushauri wake ndani ya vikao na sio hadharani na wakamzodoa kuwa anatamaa ya uraisi. Maana ndio CCM ya sasa. Mstaafu yeyote akitoa mawazo tofauti anaambiwa anautaka uraisi. Wamekuwa wanajadili watu badala ya hoja. Lakini pole pole tukaona wakitekeleza ushauri wake. Tuliona CHADEMA wakifanya mkutano Jangwani na wao wanafanya, CHADEMA wakienda mikoani kufanya mikutano, na wao wanakwenda kufanya mikutano kujibu hoja za CHADEMA tena wakaongeza nguvu ya mawaziri Mwakyembe,Magufuli na Tibaijuka kwenye ziara zao. Hiyo naona wakaona imeshindwa kudhoofisha nguvu ya CHADEMA. Wakarudi tena kutumia polisi. Ndipo tukashuhudia mauaji ya mwananchi mmoja kule Morogoro na baadaye mwandishi wa habari kule Iringa.

Kana kwamba hiyo haitoshi wakaendeleza hoja za wanasiasa waliofilisika za ukabila,udini na ukanda. Hiyo haikutosha. Sasa hivi tunaambiwa naibu katibu mkuu Mwigulu amekiri kuhusika na video ya Lwakatare. Hii ni aibu kubwa kwa chama tawala kutumia mbinu za kigaidi ili kukubalika kwa wananchi. Haya yote yanafanyika huku mwenyekiti akiwa kimya kabisa kana kwamba yuko ziarani ng'ambo kuhemea vibaba. Kama chama kingekuwa na uongozi imara, sasa hivi Mwigulu angelazimishwa kujiuzulu au kufukuzwa ili kulinda heshima ya chama. Na kama tungekuwa na polisi huru na si polisiCCM wa sasa huyu naye angekuwa ndani kama mtuhumiwa mkuu wa mchezo huo mchafu. Akina nape na kundi lake wangeonywa ili waache siasa mufilisi za ukabila, udini na ukanda. Nimekuwa najiuliza hivi Nape anapohubiri kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga, anakuwa anawapa ujumbe gani wachaga ambao ni wanaCCM? Kuwa waondoke CCM? Na hivi majuzi alikuwa Moshi. Je alikwenda kuongea na wanaCHADEMA au CCM? Anapodai kuwa CHADEMA ni chama cha kanda ya kaskazini, je wanaCCM wanaotoka kanda hiyo anawapa ujumbe gani? Au anapodai CHADEMA ni chama cha kidini yaani wakristo, je wakristo waliopo ndani ya CCM akiwepo yeye mwenyewe ndio kusema waondoke waende CHADEMA?

CHADEMA ni chama halali kilichosajiliwa baada ya kukidhi taratibu na sheria za nchi na ndio maana hata Jakaya Mrisho Kikwete alijiandaa kujiunga nacho kama angetoswa kupitishwa kugombea uraisi kupitia CCM. Vile vile Nape mwenyewe aliomba kujiunga nacho wakati wa matatizo yake na UVCCM wakati ule.
-------------------------------------------
NAPPE ashafanya hii nchi kama yake, can do anything kwa lugha ya dharau na kejeli na hafanywi kitu.
 
Back
Top Bottom