Nape, Mwigulu, Juliana na Mwampamba ndio wanaokidhalilisha na kuitia aibu CCM!

CCM sasa imeishiwa. Maana hawa jamaa wapo kwa ajili ya maslahi tu. Kauli zao ni majanga matupu. Wasubiri waone T2015CDM na muziki wa wa ukombozi wa masikini wa nchi yetu.
 
MATUKIO kadhaa ya kisiasa, mwelekeo, kauli na mienendo ya baadhi ya wanasiasa waandamizi na wenye nguvu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) vimeibua mkanganyiko na hali tete ndani ya chama hicho.


Kwa muda sasa, kumekuwa na minyukano ya ndani kwa ndani miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM, huku baadhi yao wakilaumiana kwa "kuchafua na kuua" chama.


Baadhi yao wamefikia hatua ya kumlaumu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwapa madaraka makubwa baadhi yao, na kushindwa kuwanyang'anya pale wanapoonyesha dalili za "kuua" chama chao.


Gazeto hili linazo taarifa za baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM kupeleka ujumbe mzito kwa Makamu Mwenyekiti, Phillip Mangula, wakionyesha kukerwa na kauli au mwenendo wa baadhi ya viongozi waandamizi, hasa Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba.


Wanamtuhumu Nchemba kwa kushusha heshima ya CCM mbele ya umma, na kuchangia matokeo mabaya katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika Arusha mwezi uliopita, ambako CCM ilishindwa na CHADEMA katika kata zote nne.


Baadhi ya wazee na makada waandamizi wanasema Nchemba ni "mzigo wa Kikwete," kwa maana kuwa ndiye aliyempa madaraka, na ndiye anayemsikiliza na kumpa jeuri.


Nafasi anayopewa Nchemba imeleta mgongano wa chini kwa chini kati yake na Katibu wa itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye kwa muda sasa amekuwa ndiye kipenzi cha Rais Kikwete katika kutekeleza mikakati kadhaa na kutoa matamko yenye utata dhidi ya viongozi au wanachama "wasiopendwa" ndani ya chama hicho, au dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Kwa mujibu wa makada wanaokerwa na tabia ya Nchemba, kiongozi huyo amegeuka kero kwa viongozi wenzake, ambao wanasema ameingiza siasa za ujasusi wa waziwazi na mbinu nyingine chafu za kisiasa zinazomfanya aibomoe CCM na kuiongezea umaarufu CHADEMA mbele ya umma.


Mbali na mnyukano wa uongozi, Nape amejikuta katika mgogoro mzito na wazee ndani ya chama hicho baada ya gazeti moja kumnukuu akitamka kwamba wanaoshabikia mfumo wa serikali tatu katika kujadili rasimu ya Katiba mpya, ni "wazee wanaosubiri kufa".



Baadhi ya wazee na makada waandamizi wamekerwa na kauli ya Nape, wakisema inaonyesha jeuri isiyo ya kawaida kwa kijana mdogo kama yeye.


Miongoni mwa wanaodai kukerwa na kauli hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji, Joseph Warioba, na waasisi kadhaa wa CCM wakiwamo Joseph Butiku, Jaji Mark Boman, Dk. Salim Ahmed Salim, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na wengine, hata wale wasiounga mkono hoja ya serikali tatu.


Hata hivyo, Nape anadaiwa kuwa amepiga simu kwa baadhi ya wazee hao kuwaomba radhi na kukanusha kauli hiyo, akidai kuwa alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari.


Baadhi yao wanasema hata kauli ya majuzi ya waziri mstaafu, Mateo Qaresi, ya kuiponda serikali na uongozi wa CCM, imetokana na hasira dhidi ya kauli ya Nape, ingawa msimamo wake juu ya mfumo wa muungano wa serikali ni ya siku nyingi.


Waziri huyo mstaafu amenukuliwa akisema, "Hivi hawa viongozi wanajua tunakoelekea, leo hii ukiulizwa dira yetu ni nini hakuna anayejua, bali tunajiendea tu," kauli ambayo imeibua hisia kali ndani ya serikali na CCM.


Qaresi katika utumishi wake wa umma, amewahi kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko kati ya mwaka 1989 - 1990, Waziri wa Utumishi, 1996 - 2000 na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya tangu 2000 hadi Februari 2006.


Taarifa kutoka vyanzo kadha vya habari zinasema kauli ya Nape imepunguza makali ya hoja ya CCM kuhusu serikali mbili, na imeongeza hamasa kwa wanaotaka serikali tatu, hasa wenye umri mkubwa ambao Nape amesema wanasubiri kufa.


Kwa sababu hiyo, hata mjadala juu ya Katiba mpya unaelekea kuchukua mwelekeo tofauti kwani hisia hizi zimeanza kuibua makundi pinzani ndani ya CCM, wakati ambapo hoja kuu ya chama hicho ni muundo wa serikali mbili, ambayo sasa imeanza kuwagawa.


Zipo taarifa kwamba baadhi yao wameapa kuwaadhibu kina Nape kwa kuunga mkono hoja ya serikali tatu kwa kishindo, wakidai kwamba ni hitaji la wakati.


Huku CCM wakisisitiza kwamba serikali tatu ni gharama kubwa isiyoweza kubebwa na Watanzania, kina Qares wanasema gharama kubwa zinasababishwa na matumizi mabaya, ufisadi, na taifa kukosa dira.


Qares alisema kwamba hata bila serikali tatu sasa, serikali imetenga kutumia sh trilioni tano (5) tu kati ya sh trilioni 18 za bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14, jambo ambalo linadhihirisha kuwa watawala wanatanua badala ya kuelekeza fedha hizo kwenye maendeleo.

 
Tangu ashike cheo cha naibu katibu mkuu wa ccm amejitahidi sana kukifanya chama chake kupoteza mvuto kuliko kabla hajapata hicho cheo. Amejitahidi sana kuongeza idadi ya Wabunge na Madiwani wa Chadema (pamoja na ile 4-0 ya Arusha). Amejitahidi sana kufanya wananchi wapungue kwenye mikutano ya siasa ya ccm, ikiwa ni pamoja na mikutano yake mwenyewe. Amewezesha mahakama kuu kuwafundisha wanasheria wa serikali tafsiri ya ugaidi. Ameifanya Bavicha kuwa na amani na nguvu zaidi baada ya kuwaondoa wale makapi mawili na kuwatumia kuangamiza ccm. Amemfanya Tendwa kustaafu kwa aibu na huzuni. Amemtia aibu IGP na jeshi lake la polisi

Lakini ni vema Mwigulu akajua kwamba damu za watu zilizomwagika kutokana na harakati zake za kushusha hadhi ya CCM na jeshi la polisi hazitaacha kumlilia hadi uzee wake. Wanachama wa ccm ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika kimaslahi kutokana na harakati za Mwigulu hawatamsahau. Wanachama wa Chadema waliopata mateso kutokana na harakati za Mwigulu hawatamsahau milele
 
Opportunistic and psychopath Mwigulu,siku hizi anampigia kampeni Lowassa huku akiulenga utajiri wa tilionea huyo,Mwigulu anaweza kutoa hata nn ili mradi tu achumie tumbo lake

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Asante sana hawa ni wajumbe maalum waliotumwa na Mwenyezi Mungu kuja kuleta ukombozi wa kweli kwa Watanzania.Tungeyajua lini haya yote isipokuwa ni kwa juhudi za hawa vijana Nape,mwigulu na wengineo.nNawapa BIG UP
 
MATUKIO ya kikatili yanayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia kwa kisingizio kuwa ama wameamua kuandamana au wamekusanyika kwenye mikutano isiyokuwa na kibali hakutoi adhabu mbadala ya watu kupigwa risasi za moto.

Kushamiri kwa vitendo hivyo dhidi ya makundi ya raia kunaonyesha hofu na mashaka makubwa kwa jumuiya zote za wapenda haki na amani na ni nadra sana kukubali kuwa haki ya msingi waliyonayo walinzi wa amani ni kuona wananchi wakiumizwa.

Kadiri miaka inavyozidi kwenda kuna kila dalili za wazi kuwa matukio mengi yanayotokea yanasukumwa na utashi wa kisiasa. Mifumo ya kisiasa inayotumiwa na chama tawala kikiiongoza serikali yake kuadhibu wananchi kunaleta mtazamo mbaya.

Wananchi wanashuhudia matukio ya kutisha, wanaona jinsi wenzao wasiokuwa na hatia wakiuawa kwenye mikusanyiko ya amani na vyombo vya ulinzi na usalama vikihusishwa moja kwa moja na mashambulio hayo.
Kuwa matukio mengi ni ya kupangwa na yanayoshinikizwa kwa nguvu za kisiasa bila kujali ulinzi na usalama wa wananchi walioamua kukusanyika pamoja kufanya mikutano yao kwa amani na utulivu.
Risasi za kisiasa zinatumika hovyo ili kuwadhuru wananchi wanaoonekana kuwa na misimamo tofauti dhidi ya chama tawala na serikali yake, wanaoona kuwa hawatendewi haki wanapoamua kudai haki zao kwa njia ya majukwaa ya kisheria, wanapigwa na kujeruhiwa.

Inawezekana kwa kiasi kikubwa serikali inajitia doa kubwa kutoka kwa watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawaipendi serikali iliyopo madarakani na kwa makusudi nao wanaona inafaa kuwadhuru watu ili kujenga chuki dhidi ya mamlaka.

Si jambo la kubeza au kutupiana mpira kwa mtindo ulioanza kuwadhuru viongozi wa dini, wanaharakati na wananchi wasiokuwa na hatia kwa sababu hawana mwelekeo wa kukubali uongozi na mfumo wa kiutawala uliopo.

Viongozi wa dini, wanaharakati, wanahabari na wengine waliouawa kwenye mikutano ya siasa bado haijulikani waliohusika walitumwa na nani na pia anayeratibu utitiri wa matukio ya kinyama dhidi ya wapigania haki.

Naita risasi za siasa kwa kuwa matukio mengi ya watu kuuawa yanajitokeza kwenye harakati za siasa na huko ndiko zana za kijeshi hutolewa kwa lengo la kulinda na kuzuia harakati hizo.
Kwa hali waliyonayo Watanzania, kwa jinsi wanavyopenda amani, wanaishi kama ndugu na marafiki. Watanzania sio watu wa kuuana wenyewe kwa wenyewe hasa ikizingatiwa kuwa idadi yao kubwa hawamiliki silaha.

Wananchi wanaokwenda kwenye mikutano ya vyama vyao vya kisiasa hawabebi mabomu na risasi za moto. Wanaowajibika kubeba zana hizo ni wana usalama.
Tumeshuhudia wenyewe nyumba za ibada zikichomwa moto na watu wasiojulikana, lakini wapo viongozi wa kisiasa wanaoingia kwenye nyumba hizo hizo kutaka kujijenga kwa waumini wa madhehebu hayo hayo kwa lengo la kuusaka urais.

Tumeshuhudia viongozi wa dini wakiuawa na kumwagiwa tindikali, wanaofanya vitendo hivyo wapo na vyombo vya ulinzi na usalama vipo, lakini watu hao hawashikiki na wanasiasa wanaoutaka urais nao wanapita humo humo kwenye nyumba za ibada ambako viongozi wao wa dini wameuawa na kumwagiwa tindikali.

Haifurahishi na ndiyo maana nasema wazi kuwa risasi za siasa zinawaua watu wasiokuwa na hatia na ili kuweza kuondoa hali hii bado hofu na mashaka kunaongezwa na viongozi wanaotoa kauli zenye utata zinazoshinikiza vyombo vya ulinzi vipambane na raia wanaopigania haki na maslahi yao kwa njia za amani.

Kauli hizo zinasababisha risasi za siasa zitumiwe vibaya dhidi ya wananchi badala ya kutumika kupambana na majambazi, wawindaji haramu wa wanyama wetu (majangili) na maharamia. Kinyume chake risasi hizo zinatumika mchana kweupe kuwadhuru wananchi wasiokuwa na hatia.
Kwa kuwa nchi yetu imejaliwa kuwa na viongozi wanaowapenda wananchi wao wakati wa kampeni za uchaguzi, basi ipo haja wakatambua kuwa kila mwananchi aliyethubutu kunyanyua mguu wake, kupanga foleni na kuamua kupiga kura thamani yake ni kubwa na zawadi waliyostahili kupewa si risasi na mabomu au kumwagiwa tindikali.

Kubariki matumizi ya risasi za moto kwenye mikutano ya hadhara na kwenye maandamano kunazidi kuitia doa serikali, hasa ikizingatiwa kuwa haijawahi kutokea wananchi wakafanya vurugu kwa kudhamiria ili wapigwe risasi za moto.

Ipo haja serikali ambayo ndiyo mmiliki vya vyombo vyote vya dola ijaribu kuangalia mifumo ya kiutendaji na mianya inayotumiwa na watendaji wake ili kuwadhoofisha wananchi. Hakuna sababu ya kuwafanya wananchi waanze kuishi kwa woga ndani ya nchi yao.

Hakuna sababu za msingi zinazowafanya wananchi wajenge uhasama mkubwa kati yao na vyombo vya ulinzi na usalama. Yaliyotokea Mtwara wananchi wanajua jinsi risasi za kisiasa zilivyotumika, waliouawa Arusha wananchi wameshuhudia jinsi risasi za moto na mabomu yalivyotumika hadi makanisani.
Waliouawa Morogoro wananchi walishuhudia jinsi risasi za kisiasa zilivyotumika na maajabu ya Nyololo yaliyosababisha mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi auawe. Wananchi wanajua jinsi bomu la siasa lilivyotumika kumuua Mwangosi.

Sasa tutaendelea kuuana hadi lini? Ikumbukwe kuwa chama chochote cha siasa kinaweza kuondoka madarakani, lakini si rahisi kwa watumishi wote wa umma walioajiriwa wakafukuzwa kazi baada ya chama walichokuwa wakikitetea kwa risasi kitakapoondolewa.

Si rahisi wanachama wa chama kilichokuwa kikishika dola kinapoangushwa, wanachama hao wakafukuzwa nchini bali wataendelea kuwepo na watageuka kuwa wanachama wa chama cha upinzani dhidi ya chama kingine kitakachofanikiwa kushika dola.

Kwa maana hiyo na kwa mazingira ya demokrasia na utawala bora hakuna sababu wala tija yoyote ikiwa chuki za kisiasa zitapandikizwa kwa wananchi wanaoishi kwenye nchi moja.
Kitendo cha vyombo vya ulinzi na usalama kukikumbatia chama kimoja cha siasa kwa hofu ya kupoteza ajira zao, kunawapaka doa la damu watendaji hao ambao wametoka kwenye nyumba zenye heshima, wamezaliwa kwa ajili ya kumtumikia Mungu na wanadamu.

Hakuna kiongozi wa kisiasa wala serikali aliyezaliwa na shetani ili atende unyama dhidi ya wenzake, kuua raia wasiokuwa na hatia kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisiasa, kwa vile hiyo ni dhambi kubwa mbele ya Mungu na mshahara wa dhambi ni mauti.
 

Viongozi wa dini, wanaharakati, wanahabari na wengine waliouawa kwenye mikutano ya siasa bado haijulikani waliohusika walitumwa na nani na pia anayeratibu utitiri wa matukio ya kinyama dhidi ya wapigania haki.

.

Ni kweli ndugu yangu Hujuhi au Unazuga?
Au Umetumwa?
Hata Mtoto wa Chekechea anajua kuwa Hii kazi ya Mauaji wametumwa na Mheshimiwa Mteule Mtukufu Waziri Mkuu wa TanzAnia Mizengo Kayanza Pinda. Na Ushahidi wa Hili ni Kauli yake ya Bungeni aliposema Serekali Imechoka, Mpigwe tu na Liwalo na Liwe.
 
Zamani sawa. Si sasa. Chama chetu sasa kina mkusanyiko wa watu wenye malengo tofauti. Wapo wasaka sifa na madaraka hata yasiyo rasmi. Wapo walamba miguu. Sasa,vitengo vyote vya kichama havitumiki. Kila apendaye anaibuka na kuropoka atakavyo. Mtazameni Nape Nnauye au Mwigulu Nchemba ayasemayo na ayafanyayo. Halafu ananyamaziwa tu. Taasisi gani hii!? Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Last edited by a moderator:
Hahaha hahaha :peace:Hahaha hahaha hahaha :majani7: acha wafu wazikane wenyewe.
 
Zamani sawa. Si sasa. Chama chetu sasa kina mkusanyiko wa watu wenye malengo tofauti. Wapo wasaka sifa na madaraka hata yasiyo rasmi. Wapo walamba miguu. Sasa,vitengo vyote vya kichama havitumiki. Kila apendaye anaibuka na kuropoka atakavyo. Mtazameni Nape Nnauye au Mwigulu Nchemba ayasemayo na ayafanyayo. Halafu ananyamaziwa tu. Taasisi gani hii!? Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Na matokeo yake hata serikali imesha kuwa si taasisi tena. Kila kiongozi na wana familia wake wanaamua kutoka watakavyo. Kule Mr 6 ana bwabwanya anavyo taka. kila idara ni mparaganyiko kama ilivyo Lumumba.
 
kihandisi tunasema kuna PHASE DIFFERENCE...
AIBU YAO AIBU YETUUU ..AIBU YAO WENYEWE.. POLENI SANA SAA ZA UKOMBOZI NI SASA..
 
ni kwa sababu mwenyekiti wa CCM Taifa Dr wa Magumashi KIkwete ni dhaifu sana na ana madrni ya watu waliopachika kwenye uraisi
 
Duh, naona sasa ndo unashtukia, haya tulishayaona muda. tuliposhuhudia Enzi za baba, mama Na mwana tukajua sasa taasisi kwisha
 
zamani sawa. Si sasa. Chama chetu sasa kina mkusanyiko wa watu wenye malengo tofauti. Wapo wasaka sifa na madaraka hata yasiyo rasmi. Wapo walamba miguu. Sasa,vitengo vyote vya kichama havitumiki. Kila apendaye anaibuka na kuropoka atakavyo. Mtazameni nape nnauye au mwigulu nchemba ayasemayo na ayafanyayo. Halafu ananyamaziwa tu. taasisi gani hii!? mzee tupatupa wa lumumba,dar es salaam

wala hujakosea ccm si taasisi ni chama cha siasa..tanzania
 
Back
Top Bottom