Nape mwasisi CCJ - Mkanganyiko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape mwasisi CCJ - Mkanganyiko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kituku, Jun 5, 2011.

 1. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nipata mkanganyiko kidogo baada ya kusoma mahala fulani ambapo nape aliandika kwamba watu wa JF ni mambumbu wa uchambuzi baada ya kuanika picha ya nape inayoashiria kuwa alikuwa ni wa CCJ, na kudai picha ilikuwa computerized .... kumbe yalioonyeshwa ni kweli??? huu uchungu wa haya anayoyaongea sasa ya kujivua gamba yapo ndani ya damu au??? nimekanganyikiwa jamani  Source Mwanahalisi...toleo 243


  Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe.

  Aidha, nilikutana mara moja na Mh. Samwel Sitta baada ya Mh. Nape na Dk. Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza.

  Naye Mh. Sitta alinieleza kuwa nilichoelezwa na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe hakina chembe ya mashaka.

  Katika mikutano zaidi ya mitano niliyofanya na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wenzangu walinieleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM kwa hoja kuwa kilipofikia chama hicho hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka ya kuongoza dola.

  Walisema CCM hakiaminiki tena machoni mwa wananchi na kimepoteza mvuto mbele ya umma; yote haya ni kwa kuwa chama hiki kimekuwa kinaacha ile misingi ilivyoasisiwa na waasisi wake, kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Walinieleza, kihistoria Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi na kilijipa kazi ya kupigania wanyonge, lakini kikafika mahali historia hiyo ikaporomoka kwa kuingia katika mikono ya watu wasiojali, wasiokuwa na maadili ya uongozi na labda wasiowaaminifu.

  Wakati wote wa mazungumzo yetu, Mh. Nape na Dk. Mwakyembe walikuwa wakisisitiza umuhimu wa mimi kukubali kujiunga haraka na CCJ, ili kurahisisha upatikanaji wa usajili wa kudumu wa chama hiki, lengo likiwa CCJ kiweze kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2010.

  Hata hivyo, kila muda ulivyozidi kusogea, ndivyo nilivyopata kujua undani Mh. Mwakyembe na Mh. Nape wa kutaka kuanzisha chama chao cha siasa, kwamba kinachowasukuma katika mpango huo, ni matakwa binafsi ya kisiasa na hivyo nikaanza taratibu kuwa mbali na mkakati wao.

  Nimeamua kuyasema haya baada ya kuwasikia Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wakimkana Mh. Mpendazoe na kimsingi wakikana chama chao – CCJ.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiyo Nape anayeweza kununuliwa kwa bakuli a ugali
   
 3. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sasa si bora angekubali tu kwamba amesoma nyakati labda?
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Maneno anayozungumza Nape ukiyafungia kwenye chumba kimoja yanapiga yenyewe.
   
 5. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJf hebu tupiganie maslahi ya wananchi dhidi ya dhuluma wanazofanyiwa na viongozi wao!Suala la Nape kujiunga au kutojiunga na chama fulani halina maslahi kwa sasa.Maana kila mtu anajuwa upi mchele ipi chuya!Tutafute sababu za kwa nini maisha yanakuwa magumu kila panapokucha na suluhisho ni nini!Masuala ya Ngoswe tumwachie Ngoswe mwenyewe then itafahamika wanafiki wote watatengwa na jamii zao!Maana wananchi wanajua baya na zuri,hukumu inawasubiri!Nadhani tujadili maada za kuwasaidia wananchi.
   
 6. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo ya Ngoswe hatuwezi kumuachia Ngoswe mwenyewe kwani ni hayohayo ambayo ndio kiini cha umaskinini wa Mwananchi.
   
 7. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kumjadili Nape kuhusu Kujiunga CCJ itapunguza ukali wa maisha?au ndo vijiwe vya kahawa kuanzia asubuhi mpaka jioni ndo tutawakomboa wananchi?
   
 8. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Umetumwa na Nape ili umpunguzie makali ya mjadala. Umefulia!!!!......
   
 9. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape kama kiongozi wa chama kilichoshika dola ndie anaye jadili hayo badala ya kutuonyesha jinsi chama chake kitakavyo tekeleza ahadi zake za kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Kwa hiyo sio sahihi kumtetea kwa kauri finyu kama ya 'mambo ya Ngoswe.......' Umaskini na ukali wa maisha wa watanzania hauondolewi na mijadara ya humu bali utaondolewa na utayari wa serikali kuleta maendeleo na sio kutembeza bakuri kwa wafadhiri na kutapanya rasilimali za taifa hovyo. Kama mamilioni ya Kikwete yangepelekwa kwa wakulima wa mahindi kule Songea yangezarisha "new value" lakini yalipelekwa kwa wachuuzi wa pombe na saluni za nywele. Wewe unaona hayo ni mambo ya Ngoswe... Badala ya akina Nape kuimarisha elimu ya sekondari inayodorora kila uchao wao wanatumia mamilioni ya fedha kutafuta chanzo cha shule za kata kufanya vibaya kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha nne. Watoto wale hawakuwahi kufundishwa masomo ya sayansi tangu shule hizo zianzishwe, lakini walipelekewa mtihani wafanye. Je na hilo lina hitaji utafiti kulijua? Umaskini unaondolewa na kizazi cha wajinga? Haya kaka nakubaliana na wewe " Mambo ya Ngoswe..............."
   
 10. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maulaga..Maulaga don't quote me wrongly!uliyosema hapo juu nimeyaelewa mambo ya msingi kama Elimu kudorora,n.k. ni mambo yanayoumiza sana watoto wa Tanzania!na hii ni kwa sababu ya kuendekeza mitaji ya kisiasa kama vile kujenga majengo ya shule za kata bila kuwa na walimu,vitabu,maabara,n.k.Wakati watoto wa viongozi wanasoma shule zenye hadhi kila kitu kipo!Hii ni hatari sana!Lakini pia kumbuka JF inasomwa na watanzania wengi,tuwape Elimu ya namna raslimali zetu zinavyotafunwa!Upande kwamba namtetea Nape si kweli kwanza Nape hana hoja za utetezi wa taifa bali Nape yupo ki-ccm tu!ndo maana anatembelea magari ya bei mbaya,bila huruma akienda vijijini anatangaza chama na kujibizana na upinzani utadhi yeye ndo mpinzani!sasa kwa nini nimtetee mtu kama huyo?Mimi mantiki yangu ipo kwa taifa letu siyo kujadili wasaliti wa vyama vyao vya siasa mara CCM, mara Magamba,mara CCJ,Kila sehemu usaliti mpaka wabunge wamewasaliti wananchi wao waliowatuma bungeni kazi kula posho nono tu!Au ni dhambi kuzungumzia mustakabali wa taifa?Na unajua kabisa serikali yetu ilivyo na majuha wengi!ukiniambia kuandamana kuhusu gharama za maisha kuwa juu nitakubali.Lakini ukiniambia niandamane eti kisa Nape alitaka kuhama Ccm sitathubutu sababu haina maslahi kwa taifa!Lakini pia unaweza ukaendelea kumjadili huyo Nape wako na kuhusu kutaka kusaliti magamba menzake.Au ilikuuma sana alipotaka kuhama?
   
 11. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nkomaji, nakushukuru kwa uungwana wako. Umedhihirisha kwamba Jf nimahala pa kupeana maarifa na sio kubishana tu. Waogope sana watu wanaotangaza kuwa wapo kwaajili ya kuwatetea watanzania na kuuondoa umaskini wakati uhalisia wanaganga njaa zao na kujijengea umaarufu wa kisiasa tu. Naishi kijijini naninajua maana ya umaskini na ujinga. Fikiria jinsi watu wanavyo kufa na kuuana kwaujinga na umaskini. Leo unaanzishwa mjadala wa nani mwanzilishi wa CCJ na mawazo yote yana hamishiwa huko kana kwamba hilo ni lamsingi kuliko mengine yote! ama kweli "ignorance is a machine for some to make money".
   
 12. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maulaga,that's the JF we want.Pia mi nimezaliwa kijijini najua namna ujinga,umasikini unavyowatafuna wenzetu!hebu fikiria kule ambako wanafahamu kuwa Nyerere yu hai!!ni hatari si kidogo.Tuungane kutoa Elimu ya utaifa sisi watu wenye uelewa lazima tumkomboe Mtanzania kwa sababu tuna mchango mkubwa sana kupitia hili jamvi letu.Kwa sababu si wote wanaosoma humu ni members,kwa hivyo tuhakikishe kila anayesoma humu aone mchango wetu kwa jamii na yeye atawaambia watu wengine.Kwa kufanya hivi watu wengi wataelimika!Tusikubali kufanywa mitaji ya wanasiasa kwa kubaki kujibizana mambo ya vyama tukasahau kuwa taifa linatutegemea tulikomboe na matatizo mbali mbali na hili litafanyika tukiwa kitu kimoja.Hebu fikiria kipindi hiki naandika hapa nipo gizani mgao kama kawa!inauma sana mkuu!ukiambiwa kuwa mgao wa umeme Tanzania utabaki historia and vice versa is true kuwa umeme wa kudumu Tanzania itakua historia maana yake mgao milele!unajifunza nini hapo mkuu?In short nimekubali mchango wako!let's go together kuelimisha wasiojitambua wenye kupokea rushwa ndo watoe kura zao!Hawajui we the ones to make them understand the truth!siyo kuuza utu wao!pamoja mkuu.
   
Loading...