NAPE Live EATV Saa 4:00 Usiku Leo!

NAPE Live EATV Saa 4:00 Usiku Leo!

CCM ya Nape na Mabasha zake Ikipona itakuwa muujiza wa Karne hii ...
 
Namshukuru Mungu nimeamka salama,nasubiri ratiba ya movies zaleo studio ya futuhi sijui wanaanza kuonyesha ipi,wenye ratiba naomba msaada maana nasikia kuna wengine wanaanza part 2
 
Vipi lakini ,mlimsikia bosi wenu wa Lumumba jana au mliwahi kulala

We nae unapost bila kuangalia,umepanda bodaboda nini?.Mimi niwe wa Lumumba kweli?.Kwa taarifa yako hata ile njia siikumbuki kama bado inapitika
 
We nae unapost bila kuangalia,umepanda bodaboda nini?.Mimi niwe wa Lumumba kweli?.Kwa taarifa yako hata ile njia siikumbuki kama bado inapitika

Vipi, umeisahau njia..
 
Jana usiku nimekaa naangalia kipindi cha "Siasa na Siasa" kilichokuwa kinarushwa na kituo cha Televisheni cha EATV. Katika mjadala huo alikuwepo Dr. Ryoba toka UDSM - Mchambuzi, lakini pia alikuwepo Ndg. Nape Nnauye ambaye katibu Itikadi na Uenezi- CCM. Mjadala ulihusu ucheleweshwaji wa mchakato wa Kumpata mgombea urais - 2015.

Muongozaji wa kipindi Dada Carol Ndosi. Suala mojawapo aliloulizwa Bw. Nape ni kuwa ucheleweshaji wa mchakato huo haulengj kuwepo kwa mizengwe kumpata mgombea? Nape heye alisema kuwa hizo ni taratibu za Ki-chama, lakini pia Bunge la bajeti ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kucheleweshwa kwa mchakato sababu wajumbe wengi wao pia wako bungeni. Lakin lia Ndg. Nape aliulizwa juu ya CCM kinawezaje kuwaaminisha wananchi juu ya kupata ridhaa ya kuongoza nchi hali ya kuwa chama hicho kimeshindwa kuwawajibisha viongozi wanaotumia madaraka vibaya? Ndg Nape yeye alijisifu kwa kusema kuwa Chama kama kiliweza kumuwajibisha Waziri Mkuu kwa tuhuma za ufisadi na akajiuzuru je huko si kuwajibisha? Lakini pia Ndg. Nape amekuwa akimlenga Mh. E.N. L kama mfano wa kusafisha au kutokukubaliana na uchafu katika Chama chake. Mfano alitolea mfano. Ufanyaji harambee ktk nyumba za ibada na hata akawa miongoni mwa ma- kada 6 waliopata adhabu. Nape alitumia nafasi hiyo tena kukumbushia katika uchaguzi wa Urais 1995 kuwa Hayati Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere alihoji juu ya utajiri wa Lowassa hali akiwa kijana. Nape alifika mbali hata kusema kwa mfano endapo utamkabidhi Fisi bucha la nyama utategemea nini? Lakini mimi binafsi nashindwa kuelewa kuwa ni kwanini Ndg. Nape mara nyingi amekuwa akimshambulia Mhe. E.N.L?

Nionavyo mimi kukisafisha chama kwa kutolea mfano wa mtu mmoja haipendezi. Kwani baada ya Richmond hakuna kashfa kubwa nyinginezo? Je, ni mara ngapi Mawaziri wamejiuzuru lakini leo hii tunawaona nao pia wakitangaza nia?

Binafsi mimi si mwanasiasa au mwanachama wa chama chochote, lkn afanyayo Ndg. Nape ni dhahiri unatumia nafasi uliyopo kukandamiza baadhi ya wanachama wake.

Ni maoni yangu tu.
 
Wanajuana hao na ukiwafatilia snaa utaumizi bichwa lako
 
Wacha aseme anayojisikia. Nape ana viongozi wake, na amachofanya hajaanza leo. Mbona hao viongozi wake hawamkanyi? Inaweza kua anaongea kama Nape Binafsi na sio Katibu wa Itikadi na Uenezi.

Yote ya yote ni kua Ya Ngoswe muachie mwenyewe Ngoswe!
 
Wacha aseme anayojisikia. Nape ana viongozi wake, na amachofanya hajaanza leo. Mbona hao viongozi wake hawamkanyi? Inaweza kua anaongea kama Nape Binafsi na sio Katibu wa Itikadi na Uenezi.

Yote ya yote ni kua Ya Ngoswe muachie mwenyewe Ngoswe!

Teh teh teh
 
Back
Top Bottom