Nape kutangaza na kuzuia Kwa nguvu zote Bunge kuwa Live, Je Bunge lipo kwenye Wizara anayoiongoza?

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Nashindwa kuelewa maana Bunge ni chombo cha wananchi, sasa inakuwaje Waziri wa Serikali kuwa na nguvu ya kulipangia? Je wabunge ni mali ya Serilali? Au wawakilishi wa wananchi.
 
Baadhi wanasema eti wakati wa jk nchi ilikuwa kwenye 'auto piloting' na wengi waliona ni tatizo, lakini itakuwa mbaya zaidi kama awamu ya JPM tutawakabidhi 'pilots' wa baskeli kuendesha Boeing 777. si ndio haya tunayooona, au mnasemaje!?
 
Kafanye kazi uongeze kipato chako na cha familia yako! Achana na Bunge halitakulipia karo wala luku!
Kuna baadhi walikuwa wamefanikiwa kuongeza vipato kwa shilling kama 300/- per day lakini wamejikuta ni kama wameongeza sifuri baada ya sukari kuwa 2,600/- kutoka 1,800/- kwa kilo.
 
Nashindwa kuelewa maana Bunge ni chombo cha wananchi, sasa inakuwaje Waziri wa Serikali kuwa na nguvu ya kulipangia? Je wabunge ni mali ya Serilali? Au wawakilishi wa wananchi.
Hakuna bunge tena. Hicho kinachoonekana kuwa ni bunge, kiuhalisia ni idara ya serikali
 
Kuna baadhi walikuwa wamefanikiwa kuongeza vipato kwa shilling kama 300/- per day lakini wamejikuta ni kama wameongeza sifuri baada ya sukari kuwa 2,600/- kutoka 1,800/- kwa kilo.
Hayo yote ni chini ya serikali yetu sikivu na inayo wajali wananchi wake haswa wale wenye kipato cha chini kama sisi
 
mambo mengine yanashangaza kweli ILA woga wao ni kutokana na WELIDI wa UKAWA wakati wao CCM sio watu wa kujenga hoja au hata kusoma makabrasha kwa ajili ya kuchangia kama walivyo wenzao wa UKAWA!CCM wao ni mipasho na ndiooooooooooooooooooooooo!
 
Hakika anavyopinga anaonyesha usoni mwake kwamba anatetea maslahi.
Kitu chakistaajabisha serikali hii inataka kutumia mbinu za kidikteta bila kuangalia nyakati.
 
Nashindwa kuelewa maana Bunge ni chombo cha wananchi, sasa inakuwaje Waziri wa Serikali kuwa na nguvu ya kulipangia? Je wabunge ni mali ya Serilali? Au wawakilishi wa wananchi.

Pole.Bunge ni department chini ya ofisi ya Rais.Kwa sasa in short hakuna Bunge bali kuna mkutano wa Wanachama wa CCM wanaoitwa Wabunge
 
Kafanye kazi uongeze kipato chako na cha familia yako! Achana na Bunge halitakulipia karo wala luku!

Hata JKN aliona umuhimu wa kuweka Bunge live sasa sijui nyie mnasemaje?JKN aliwaasa wana CCM akasema yale mabaya msiyaige lakini yale mema myaige na kuyafanyia kazi.Lakini ninachokiona ni kwamba mnaiga maovu na kufumbia macho mazuri
 
Bunge halitonyeshwa live bali litarekodiwa na kuonyeshwa jioni, finito Mada imefungwa nenda kokote utakatako! Ukitaka kuonyesha Bunge live shindeni uchaguzi kwanza muongoze Serikali ndiyo muonyeshe Bunge live!
 
Back
Top Bottom