Nape kakurupuka lakini waandishi wa habari mjirekebishe

KILLERS KISS GUY

JF-Expert Member
May 9, 2013
718
255
Kwa kila mwenye akili timamu na uwezo wa kufikiri ni lazima atalaani kitendo alichokifanya Nape kulifungia gazeti la Mawio mazima kwa sababu zifuatazo, Moja hakuwapa nafasi ya kuwasikiliza juu ya yale waliyo kuwa wanayaandika pengine yangekuwa ni msaada kwa Taifa, pili alitakiwa kuwapa onyo kwanza kabla hajafanya maamuzi magumu namna hiyo.

Lakini waandishi wetu wa habari nao mnapaswa mjirekebishe punguzeni kuwa watumwa kwa wanasiasa hamuandiki mpaka wanasiasa waseme, mbona kuna mambo mengi sana ya kuandika siyo kila siku mnaandika majina ya watu badala issues, jamii zetu zina matatizo mengi ambayo nyie waandishi wa habari mnapaswa kuya ripoti kwa lengo la kubadilisha jamii zetu.

Mnaishia kuandika habari za Dar tu kila siku wakati mikoani kuna mambo mengi sana ya kuandika, mna jukumu kubwa sana sema tu hamjui.

Mwanadishi anapaswa, kuirekebisha jamii yake, kukosoa, kuelekeza, kuunganisha, lakini waandishi wetu hamyafanyi hayo. mna jukumu kubwa sana sema tu hamjui.
 
Hivi haujui kwamba sheria lazima zifuatwe huu wakati sio wa kikweeeleeeee
 
Hukusikia kwamba mhariri wake alipewa onyo zaidi ya mara mbili Lakini akadharau. Nape amelifungia hilo gazeti KWA MUJIBU WA SHERIA, so yeye ni mwakilishi wa kilichofanywa lakini wewe unamuandama as if alilala tu akakurupuka bila kufuata sheria..u shud think twice bro.
 
Mawio niliwahi nunua mara 1. Nikaona hamna maudhui. Mpaka sasa nilikuwa siangalii hata kichwa, maana nilijua anaandika ZZK au Makonda. Hizi habari za watu zinatakiwa zipingwe ndo maana fb watu wamempalula Mbowe eti anatoa pole.

Watu wakamwambiwa wabadilike haraka sana.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali katika kipindi cha mwaka mmoja mhariri wa gazeti keshaitwa mara nne kushauriwa kuacha kuandika habari ambazo hazina ushahidi, za kutunga na kutumia gazeti kuchafua watu aombwe vipi tena.

Wacha liwe fundisho kwa wengine bado kuna magezeti mengi yanayoandika habari ambazo zinadumaza jamii kwa ujinga na uongo kitu ambacho akikubaliki kabisa ethically.
 
CCM bwana kweli vichwa maji wanataka kuwanyamazisha watu mbona hata Misri walifanya hivyo yakawatokea puani sauti za wananchi haziwezi nyamazishwe wanataka wasifiwe kwa lipi wakati wamejaza ufisadi tuu
 
CCM bwana kweli vichwa maji wanataka kuwanyamazisha watu mbona hata Misri walifanya hivyo yakawatokea puani sauti za wananchi haziwezi nyamazishwe wanataka wasifiwe kwa lipi wakati wamejaza ufisadi tuu
Hakuna sauti ya wananchi wanaounga ujinga wa Kubenea. Hata Marekani wanafuata sheria zao. ndo maana watu kama akina Snowden walikumbia taifa.

kama mnataka taifa kama hilo. Subiri 2040 au 2100.
 
All in all waandishi wetu wabadilike wapunguze kuwa watumwa kwa wanasiasa mbona kuna mambo mengi sana ya kuandika siyo kila siku wanaandika majina ya watu.
 
Mawio niliwahi nunua mara 1. Nikaona hamna maudhui. Mpaka sasa nilikuwa siangalii hata kichwa, maana nilijua anaandika ZZK au Makonda. Hizi habari za watu zinatakiwa zipingwe ndo maana fb watu wamempalula Mbowe eti anatoa pole.

Watu wakamwambiwa wabadilike haraka sana.
Mimi nimelisoma sana 2013 kabla ya kugundua sijitendei haki.
 
Unapokuwa na waziri wa habari kama Nape unategemea nini zadi ya alichofanya.
 
Hivi ile amri kwa radio na tv stations kuwalipa wasanii kila wapigapo nyimbo zao imeishia wapi? To start something impossible you must have an impossible mind. Fanyeni kwa kufikiri, kutafakari na kushirikisha wadau.
 
Bado kiu uwazi et al haya magazeti ni kinyaaa
Hayana taarifa za kuhatarisha maisha kama Kubenea. Mgazeti mengi ya Udaku ni ya kuuza hisia na matamanio. Hivyo, mpaka mtu anunue anataka atulie kulisoma kama unavyaangalia tamthilia na maigizo.
 
Je hicho kilichoandikwa hakina ukweli? Na kama hakina ukweli serikali ilitakiwa imwambie bwana Mawio kuthibitisha kwa ushahidi alichokiandika ndani ya muda fulani alafu asingethibitisha ndio afungiwe na kukamatwa lakini kila nikisoma humu naona watu wanasema jamaa alipewa onyo, labda kama sijui maana ya onyo. Onyo unaweza pewa ili usiseme ukweli yaani kukufunga mdomo hiyo lazima iwe ngumu kwa msema ukweli kukubali kukaa kimya kisa kaonywa au katishiwa. Ebu tuwekeni wazi serikali ilishawahi kutaka vithibitisho juu ya vilivyowahi andikwa au ndio imebaki kuita vyombo vya habari na kusema vimeandikwa vitu si vya kweli bila kuhitaji vithibitisho kutoka kwa waandishi husika au gazeti husika
 
Mimi nilikuwa namheshimu sana kubenea lakini baada ya kuona anawaandika watu kwa interest yake na sio kwa interest ya taifa nimeacha kusoma magazeti yake.hapa Jamhuri tu
 
Back
Top Bottom