Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,653
- Upo msemo usemao ngomaikilia sana ipokaribu kupasuka.Wewe kwakua ni mwanasiasa maarufu naamini unajua pia uzuri na ubaya wa kuwa maarufu ila inakua mbaya zaidi ikiwa watu waliokupigania ukawepo mahalifulani ukashindwa kutimiza ndoto zao na ukatimiza matakwa ya wasiokupigania na katika hali hiyo ndipo wewe( Nape) na Kinana mliwaita baadhi ya mawaziri ni mizigo.
- Wapo wanasiasa wawili na maarufu hapa nchini ambao nitawatumia kama somo kwako nao ni LUKUVI na WASSIRA watu hawa wawili wanafanana kiutendaji na kimitazamo lakini pia hutofautiana kwabaadhi ya mambo nikirejea hasa kwenye mchakato wa katiba mpya iliyobaki kuwa kitendawili miongoni mwetu
- Lukuvi alikua anajua sana kucheza na hisia za watu,kushawishi,kubadilika kutokana na mazingira na kuwa na akiba yamaneno ingawaje anaomchango mkubwa kwenye kukwama kwa mchakato ule pia
- Wassira ni mfia chama,akakosa akiba ya maneno kejeli nyingi kwa wenye mawazo tofauti na yeye na akawa mbabe kwayeyote aliye kinzana nae kwahoja.Alijiona kama yeye ni CCM na CCM niyeye.Nahatimaye kwasababu anazozijua yeye akawa na mchangomkubwa sana kwenye kuirudisha nyuma rasimu ya WARIOBA na akafanikiwa.Sidhani kama iposiku aliyofikiria kwamba atalitazama bunge kwakuikosa fursa ya yeye kuwapo pale mjengoni tene MAGUFULI NIZAIDI maana hajamuita .Nakibaya zaidi anataka labda kuona yatendekeyo Dodoma naye pia haoni kwa wakati kama sisi nahapo ndipo amejua maana ya nguvu ya umma
- Nape siasa itakupiga kumbo na chama kitaendelea kuwepo kwakua huzijali hisia na mahitaji ya waliowengi tena waliokuweka hapo.Ng'ombe hatambui thamani ya mkia wake hadi ukikatika na nzi wakimtambaa ndio huukumbuka umuhimu wa kiungo hicho,nenda kwa Wassira ukamuulize funzo alilolipata na wapi aliteleza atakuambia.Inawezekana kabisa wewe pia ukaja kujutia uamuzi wako huo kwani usipokua pale ndani nilazima utataka kujua yanayojadiliwa ila hutaona