Nape awatetea UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape awatetea UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIGENE, Oct 28, 2012.

 1. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kuwa Watanzania hawapaswi kushangazwa na kitendo cha vijana wa UVCCM kuchapana makonde juzi hadharani kwani tukio hilo si la kwanza kutokea kwao.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Nape alisema ugomvi wa juzi katika makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam ni mambo yanayowakuta vijana wengi katika maeneo mbalimbali na kwamba kinachotakiwa ni namna ya kuutuliza.

  "Mimi niko Mwanza, sijapata taarifa sahihi hivyo siwezi kukupa tathmini yangu, lakini tambua haya yalianza enzi za kina John Guninita, hata mimi na Nchimbi tulishawahi kugombana mwaka 2003 kwa sababu ya umoja huo, cha msingi ni kuangalia nini kitafanyika baada ya tendo hilo," alisema Nape.

  Alisema wakati wa kina Guninita kanuni za uchaguzi zilifuatwa na bado kulitokea hali ya kutoelewana na kusisitiza kuwa hata marehemu baba yake Moses Nnauye akiwa kiongozi wa jumuiya hiyo, walishachapana kwa bakora kwa ajili ya kuweka mambo sawa.

  Aliongeza kuwa anasikitishwa na hali ya vijana wa chama hicho kukosa uvumilivu hata kufikia hatua ya kuvamiana mwilini na kupigana na kwamba chama kitakaa baada ya kupata taarifa kamili na kisha kutoa tamko lake juu ya tukio hilo.


  CHANZO: Tanzania Daima
   
 2. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wavuta bangi wanajuana
   
 3. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tabia hujenga mazowea,,,,,........
   
 4. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo zilipofikia siasa ndani ya CCM kwa sasa, hao vijana wamakunjana sio kwa sababu wanataaka kuweka mambo sawa au wana uchungu na chama, hao wanataka waonekane na waliowatuma katika kambi zao za urais kuwa wanafanya kazi, achananeni na nguvu ya pesa......mpaka 2015 tutashuhudia mengi ndani ya CCM.
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ana haki kuwatetea sababu anajua watachapana makonde zaidi 2015.

  Hizo ni rasharasha tu
   
 6. h

  hacena JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wanatwangana hivyo je wakikuta mtu wa chama kingine ndio maana wanataka kuua kumbuka yaliyowapata Mh Kiwia na Mh Machemli na leo Rechal Mashishanga. Mungu waondoe CCM ili viumbe wako tuishio hapa Tanzania tuishi kwa amani, upendo na haki.
   
 7. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  • Nape awatetea adai kuchapana ni kawaida

  na Betty Kangonga na Abdallah Khamis

  SIKU moja baada ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), kuchapana hadharani kupinga viongozi wao wapya wakidai uchaguzi wao ulitawaliwa na rushwa, baadhi ya viongozi wa dini wameta hatua zaidi zichukuliwe kukomesha rushwa inayozidi kushika mizizi.

  Wao viongozi wa dini walikemea rushwa huku wakitaka pia nyumba za ibada ziheshimiwe badala ya kutumiwa kama majukwaa ya kisiasa na baadhi ya watu.

  Akizungumza katika Kanisa la Christian Misssion Fellwoship la jijini Dar es Salaam kwenye ibada ya Jumapili iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kuombea amani, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mgulu Kilimba, alisema kitendo cha vijana hao kutwangana makonde kinaonyesha hakuna mafanikio ya kukabiliana na tatizo la rushwa.

  Alisema serikali na watawala wamekuwa wakilaani na kukemea ubaguzi wa dini, rushwa na ufisadi bila kuwepo kwa mafanikio ndiyo maana taifa linashuhudia vijana wakitwangana kutokana na kushamiri kwa matendo ya rushwa.

  "Hii yote ni vita ya kiroho. Chuki na rushwa ni roho ya shetani na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini huku watawala wakitakiwa kuchukua hatua ili kukabiliana na tatizo hilo linalozidisha chuki kwa jamii," alisema.

  Alisema kuwa kutokana na matatizo hayo, kanisa hilo limechukua hatua ya kufanya ibada maalumu ya kuombea taifa amani iliyohusisha maombi kutoka makabila 12 ambapo waliomba kwa lugha zao pamoja na kuimba wimbo wa taifa kwa ajili ya kusisitiza amani.

  Huku akisoma maandiko kutoka katika kitabu kitakatifu cha Biblia 1Timotheo 2:1-2 ‘Basi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani, tukimcha Mungu na kuwa wenye heshima kwa kila njia.'

  Kuhusu nyumba za ibada, Dk. Kilimba alionya viongozi wa kidini kuhakikisha kuwa nyumba za ibada zinatumika kwa ajili ya mahubiri ya neno la Mungu na kuepuka kutoa mahubiri ya kisiasa yanayochangia kuwepo kwa vurugu.

  Alisema kuwa viongozi wa dini wanaaminiwa na jamii inayowazunguka iwapo watatoa neno lolote linaweza kujenga nyufa na kujitokeza kwa chuki.

  Dk. Kilimba alisema kuwa iwapo amani itaondoka matajiri na walio na fedha watalazimika kukimbia na kuwa wakimbizi katika nchi nyingine huku maskini wakikosa mahali pa kukimbilia na kuishia kuuawa hivyo ni muhimu kuitunza na kuilinda amani kwa gharama zozote.

  Alisema amani hiyo ni tunu iliyotoka kwa Mungu ambapo waasisi wa taifa hili akiwemo hayati Julius Nyerere waliiacha na inapaswa kuenziwa.

  Naye, Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni B Assembilies of God, Dk. Getrude Rwakatare, alisema kuwa ibada ya Jumapili imetumika mahsusi kwa ajili ya kuombea taifa amani.

  Alisema kuwa ni muhimu Watanzania wakaishi kwa kusameheana na kuondokana na makundi ili taifa liendelee kujivunia kuwa kisiwa cha amani.

  "Manung'uniko hayajengi na wala hayasaidii tuondoe kunyoosheana vidole ili tuzidi kuijenga nchi yetu na taifa liendelee kuwa kimbilio la nchi nyingine," alisema.

  Aidha mchungaji Niku Kiungu kutoka nchini Marekani, alisema kuwa Mungu ataendelea kulibariki taifa hili kwa kuwa hata wimbo wa taifa umeanza kubariki mataifa mengine kwanza.

  Nape awatetea UVCCM
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kuwa Watanzania hawapaswi kushangazwa na kitendo cha vijana wa UVCCM kuchapana makonde juzi hadharani kwani tukio hilo si la kwanza kutokea kwao.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Nape alisema ugomvi wa juzi katika makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam ni mambo yanayowakuta vijana wengi katika maeneo mbalimbali na kwamba kinachotakiwa ni namna ya kuutuliza.

  "Mimi niko Mwanza, sijapata taarifa sahihi hivyo siwezi kukupa tathmini yangu, lakini tambua haya yalianza enzi za kina John Guninita, hata mimi na Nchimbi tulishawahi kugombana mwaka 2003 kwa sababu ya umoja huo, cha msingi ni kuangalia nini kitafanyika baada ya tendo hilo," alisema Nape.

  Alisema wakati wa kina Guninita kanuni za uchaguzi zilifuatwa na bado kulitokea hali ya kutoelewana na kusisitiza kuwa hata marehemu baba yake Moses Nnauye akiwa kiongozi wa jumuiya hiyo, walishachapana kwa bakora kwa ajili ya kuweka mambo sawa.

  Aliongeza kuwa anasikitishwa na hali ya vijana wa chama hicho kukosa uvumilivu hata kufikia hatua ya kuvamiana mwilini na kupigana na kwamba chama kitakaa baada ya kupata taarifa kamili na kisha kutoa tamko lake juu ya tukio hilo.


  Source: Tanzaniadaima 29.10.2012
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  dr. Mgulu kilimba???? dr. Getrude Lwakatare??? Taasisi ya Imam Buhari & sheikh khalifa???
  wameimba shairi moja.
  Maswali mengi kuliko majibu, labda wenzangu mna majibu.
   
 9. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Baba mtukutu huzaa watoto watukutu na wakiwa wakubwa wataendeleza utukutu.
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Yaani katibu Mwenezi wa Chama anaeneza umahiri wa kihistoria wa vijana ndani ya chama chake kutumia nguvu badala ya hoja?
   
 11. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]CHRISTIAN MISSION FELLOWSHIP[/FONT]
  [FONT=&quot]P.[/FONT][FONT=&quot]O. Box 55024 Dar Es Salaam Tanzania, E-mail:[/FONT][FONT=&quot]info@cmftz.org[/FONT][FONT=&quot], website: [/FONT][FONT=&quot]www.cmftz.org[/FONT][FONT=&quot][/FONT]​
  [FONT=&quot] Tel: 0715200551, 0755200550 : Tarehe 28/10/2012[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI NCHINI[/FONT]
  [FONT=&quot]Neno la Mungu limetuagiza katika 1Timotheo 2:1-2; kuwa, kabla ya mambo yote nataka DUA, SALA, MAOMBEZI NA SHUKURANI vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Tukiwa Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno ili Amani tuliyopewa na Mungu na kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa.[/FONT] [FONT=&quot]Ndugu zangu Watanzania sote tufahamu kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika Katiba yetu ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, ni kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini. Katiba Ya 1977 Ibara 13(5).[/FONT] [FONT=&quot]Kwa upande wa madhehebu ya Dini Tanzania tuna dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo; Dini kubwa ni Ukristo, Uislamu na Dini za Kijadi. Wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika Nyumba moja na kufanya shughuli za Kijamii kwa pamoja bila kubaguana kabla na baada ya miaka hamsini (50) ya uhuru Nchi yetu. [/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Ndugu zangu wakristo na watanzania wezangu kwa ujumla napenda kuwafahamisha kuwa, hakuna nchi yeyote katika bara la Afrika yenye idadi kubwa ya wakristo na waislam wanao ishi kwa amani na upendo kama Tanzania.Ila kwa sasa watu wasioitakia amani Nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini ili isiwe nchi ya amani bali vurugu.[/FONT] [FONT=&quot]Hivi karibuni, tumeshuhudia kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa nazo sawa na Dini nyingine. Hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya habari; Mathalani: Redio, Magazeti na Machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa Jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika Jamii iliyokuwa imeshikamana. Aidha, mgawanyiko huu unazidi kukua na kusababisha hali ya Chuki kwa mamlaka ya Nchi, na hatimaye Dini moja na nyingine. [/FONT] [FONT=&quot]Baada yakufanya utafiti wa kina kwanini kuwe na Chuki baina ya makundi ya Dini na Serikali tumeona kuwa, makundi haya ya Dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea Dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika utawala. Hata hivyo, Madai ya kundi hili yanawapelekea kuwafanyia Vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa linapendelewa na Serikali, jambo ambalo linawafanya (wanaofanyiwa vurugu) wasitumie uhuru wao wakufanya ibada ambao kimsingi wamepewa Mungu na kuandikwa katika Katiba ya Nchi Yetu.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]Tukiwa Kanisa la Mungu, hali hii inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za Nchi zinalindwa na kutekelezwa. Kimsingi, haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi. [/FONT] [FONT=&quot] Hivyo, Kanisa baada ya Kumlilia Mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa uwajibikaji usio wa maneno tu; kwani suala la kutoa matamko ya kulaani limefanywa na Dini na Serikali kwa mkazo mkubwa. Kwa upande wa Serikali, watawala wa Nchi yetu wamekuwa wakilaani na kukemea, ubaguzi wa Dini, rushwa na ufisadi katika Taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa sababu hii ni vita ya kiroho na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa jinsi hii, Kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa Shetani; hivyo watu wa kiroho tunalo jukumu la kuziopinga hila za Shetani kwa DUA, SALA NA MAOMBI ili kuleta amani ya kudumu katika Taifa letu, ambalo linasifika kuwa ndiyo kitovu cha amani Afrika na Duniani. Ndugu zangu wakristo na viongozi wa dini; ikumbukwe na izingatiwe kuwa nyumba za ibada ni sehemu ya kumwabudu Mungu, hivyo zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na Mungu na sio siasa, na pasiwe mahali pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu. Viongozi wa dini wanaaminiwa sana na waumini wao na lolote watakalo waambia waumini, huaminiwa kuwa limetoka kwa Mungu. [/FONT] [FONT=&quot]Aidha tukumbuke kuwa, tunafanya kila kitu vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo. Amani isipokuwepo hakuna kitu kinaweza kufanyika katika Nchi; iwe kwa waumini na wasio wauimini, iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa watakimbia na kuwa wakimbizi wa Nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kawahiyo ni vema kuitunza amani yetu na kuilinda; kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu; hii ni tunu tuliyopewa na Mungu na kuachiwa na waasisi wa Nchi yetu ili tuienzi, hivyo kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema Hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani.[/FONT] [FONT=&quot]Nichukue fursa hii kumpongeza Kamanda Suleiman Kova kwa juhudi zake za kuifanya Dar-es-salaam iendelee kuwa bandari ya Amani; Kamanda Kova ameonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake, kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola nchini na kwa watanzania wote. Kanisa la Mungu ambao tumeitwa kw[/FONT][FONT=&quot]a Jina la BWANA, leo hii tunaomba na kuutafuta Uso[/FONT][FONT=&quot] wa BWANA tukiwakilisha zaidi ya makabila 120 ya Tanzania kwa Kutumia Lugha Zetu za Makabila kama alama ya Umoja na mshikamano wetu, tukimsihi Mungu aiponye Nchi yetu. Tunaitakia Nchi yetu amani na Utulivu, katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Amini.[/FONT]
  [FONT=&quot]NDIMI NDUGU YENU KATIKA KRISTO YESU [/FONT]​
  [FONT=&quot]……………………………………………….[/FONT]​
  [FONT=&quot] ASKOFU MKUU DKT. MGULU KILIMBA .[/FONT]
   
 12. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nape ana lake jambo anajua huo ugomvi kausuka yeye baada ya wagombea aliowataka salum hapy na makonda kushndwa kwa sababu ndan ya ccm nape yupo na sita kwa taadhar na yupo na membe kulinda ajira kuptia rz sasa yupo mwanza anahamasisha ccm halisi huyu kijana anakurupuka sana sijui ccm bado wanamvumilia kwa nn
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ukisema sijui kwa nini CCM wanamvumilia unadhani wanastahili kumvumilia nani humo ndani? CCM kwa ujumla wake haivumiliki
   
Loading...