Nape amvaa Dr. Slaa

Nape amvaa Dr. Slaa

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Katibu wa itikadi n uenezi wa chama cha mpinduzi (ccm) Nape Nnauye amemtaka katibu kuu wa chadema dr. Wilboard Slaa kuwaeleza Watanzania fedha ambazo amepewa na nchi za Ulaya kwa ajili ya uchaguzi mkuu na masharti yake ni yapi na asipoeleza CCM itayaweka bayana.

Nape alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyikakijiji cha Biharamulo mkoani Kagera amabapo alisema wanaushahidi wa masharti aliyopewa Dr. Sla kwa niaba ya chama chake na lengo za nchi hizo la kufanikisha uchaguzi mkuu

Alisema kabla ya kuanza kutumia fedha hizo ni vemaDr. Slaa akawaambia watanzania masharti gani amepewa ili wapime na kuona dhamira ya chama hicho kinyume CCM itaeleza kila kitu hatua kwa hatua na kutaja masharti yote amabayo Dr. Slaa amepewa na waliotoa fedha hizo

Akifafanua, Dr. Slaa yupo nchi za Ulaya na kilichompelek ni kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu na tayari nchi kadhaa zimempa fedha tayari kwa kwa masharti ambayo lazima wayatekeleze na ccm tayari imepata masharti hayo, hivyo kabla ya kuwaambia Watanzania, Dr. Slaa aseme akishindwa hawatakaa kimya.

Alisem kwa sehemu kubwa fedha amabazo zimetolewa na baadhi ya nchi za ulaya kwa chadema hazina nia njema kwa Watanzania ndio maana wanataka Dr. Slaa awe mkweli kwa kueleza masharti gani aliyopewa.

Chanzo: jamboleo

June 16, 2015
 
Nape aache kubwabwaja vitu visivyo na msingi...
Aweke wazi na sio kumtishia mtu mzima utadhani anajibishana na watoto wenzake...
Misaada wanayochukua CCM na kuipeleka mifukoni kwao mbona hawaweki wazi??

Nape pia atutajie wezi wa ESCROW wote!!!
 
Mimi ni CCM lakini huyu Nape huwa mropokaji tu hana lolote, amejaribu kumtikisa Lowassa kwa zawadi ya jimbo la Membe akaishia kutikisika mwenyewe. Ni bora akomae na madomokaya wezake UKAWA.
 
Popoma tu huyu anaona wivu na wao wamteuwe wa kwao aende kubisha hodi kama kawaida yao mwaka huu wanalo.
 
Slaa fisadi sana... kafisidi hadi mke wa mtu...!!! Sasa kaenda kupewa mapesa na makameroon sijui atalipaje...!!! Maana masharti yao hao makameroon wanakupiga kabaang...wallaah hatukubali huo mchezo mchafu...Noo..!!!
 
Dr Slaa hawezi kujibizana na Nape ni Bwana mdogo sana.Nape saizi yako ni Lowassa..........

anatafuta kiki ya dr slaa?hawezi chadema ni chama makini sana akiwezi kujibu upuzi kama huu na ikilazimika kujibu tutatafu diwani amjibu nape
 
Slaa fisadi sana... kafisidi hadi mke wa mtu...!!! Sasa kaenda kupewa mapesa na makameroon sijui atalipaje...!!! Maana masharti yao hao makameroon wanakupiga kabaang...wallaah hatukubali huo mchezo mchafu...Noo..!!!

watanzania tuwaogope wanaopewa masharti na wale wenye kale kmchezo kachafu ka kugezana
 
Huyu Nape kachoka na Lowasa karudi kwa Dr. Slaa
Mie nasubiri matokeo Lowasa ashinde ama UKAWA halafu nione atakavyohama nchi
Tehehetehe kazi ya uvuvuzela hovyo sana
 
Back
Top Bottom