T2015CCM
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 7,931
- 987
Kama mtakumbuka Miaka ya nyuma kidogo Nape alisababisha vurugu kubwa sana pale umoja wa vijana akiwa mjumbe wa baraza kuu la UVCCM hadi akavuliwa uanachama, Records zipo.
Baada ya muda mrefu kidogo J.K akampa ukuu wa wilaya ya Nanyumbu. Ikumbukwe kuwa marehemU mzee Nnauye na Kikwete Jakaya walikuwa marafiki sana na Kikwete na Mzee Makamba na Nnauye hawakukutana barabarani. Walikutana Singida wakati Kikwete ni katibu wa CCM, Makamba ni katibu tarafa na Nnauye alikuwa nani sijui, nimesahau.
Kwanini nimekumbusha haya?
Ni kwamba Nape alikuwa bado anaamini kuwa anafanya kazi na baba zake walezi kwa hiyo amesahau hizi ni zama zingine.
Namuomba Nape sasa atulie. Atulize kichwa. Kila zama na kitabu chake.