Nape akabidhi vyakula vya sh. Milioni nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape akabidhi vyakula vya sh. Milioni nne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Dec 24, 2011.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CCM YASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR, NAPE AKABIDHI VYAKULA VYA SH. MILIONI NNE.
  [​IMG]Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikabidhi msaada wa vyakula kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik , katika ofisi ya mkuu huo jana. Vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 4, vimetolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia waliokumbwa na maafa ya kafuriko yaliyosababishwa na vyua katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

  [​IMG] Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye akizungumza na kina mama wenye watoto, ambao aliwakuta kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, leo, alipokwenda kutoa msaada wa CCM wa vyakula kwa waliopatawa na mafuriko. Kina mama hao, Mariam Msimbi na Asha Selemani (kulia) walifika kwenye ofisi hiyo kutafuta ufumbyuzi wa ndoa zao ambapo wamedai wametorokwa na waume zao huku wakiwa na watoto wadogo.
  [​IMG]Nape akizungumza na baadhi ya wananchi alipofika kwenye kambi maalum ya Mchikichini walikohifadhiwa waathiorika mwa mafuriko, wilayani Ilala.
  [​IMG]"Tunashukuru serikali imetuhudumia vizuri sisi waathirilka.. wanaolalamika ni wale wanaojichomeka ili wapate msaada wakati si wahusika.." akisema mmoja wa wazee (kulia) ambao Nape alizungumza nao kujua serikali ilivyosaidia waathirika wa mafuriko, alipotembelea kambi la Mchikichini walikohifadhiwa kwa muda waathirika hao,leo.
  [​IMG]Nape akipata taarifa za matibabu wanayopatiwa waathirika wa mafuriko, katika kituo cha muda cha wathirika hao, shule ya msingi Mchikichini
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Kwani naye Mwandishi wa habari(mpiganaji)?
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  La hasha,si muandishi wa habari yeye ni mpiganaji mwenzetu wa ufisadi humu jf kwa miaka mingi tu,wengine tumewapoteza njiani kama kawaida ya vita yeyote ile....
   
 4. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa nini anapenda sana kutoa ulimi nje au ni ugonjwa.

  [​IMG]
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Naona ndio kilema chake na yeye si unajua hakuna alo kamili,hata wewe pengine kuna mambo usiyoyapenda mwilini mwako yawepo lakini ndio maumbile yako ukivyoumbwa...hicho ndio kilema chako nawewe!
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Mkuu do you think atamng'oa EL?
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Halafu hiyo milioni nne labda ndo lunch ya watu flani, hivi msafara ya muungwana ukitua pahala lunch ni haifiki em nne kweli?
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kung'olewa kwa Lowassa na wenzake mbona sasa kuko wazi zaidi,hofu ilikua ni kukwamishwa na NEC,lakini mbinu iliyotumiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete, kurudisha suala hilo kuamuliwa na Kamati ya Maadili kisha kuwasilisha maamuzi yake kwa Kamati Kuu ni wazi kabisa kwamba yametimia hata lowassa analijua hilo ndio maana unaona kina kibanda wanajaribu kubeza ili kuwapoteza wananchi i maamuzi yakapokuja kufikiwa ionekana kama ni ghafla mno kwa kuwa suala lilishamalizwa na nec wakati sio kweli.Lowassa kete yake ilikua ni nec ambako ana mamluki wengi mle wanaomuunga mkono na walijiiandaa mno siku ile hata mimi sio siri niliogopa nikajua ccm pangewaka moto siku ile,lakini kwa katiba ya ccm mwenyekiti wao ana nguvu nyingi sana ndio mana kwa kutumia nguvu alizonazo akalivusha pale kwa ya kutonywa na wakongwe pamoja na taarifa za kiintelijensia alizopewa na anaowaamini huko uwt.Lowassa tatizo hana watu kwenye kamati ya maadili ukimuacha swahiba wake mpya Amani wa zanzibar ambae kuna ahadi wamepeana kama lowassa atafanikiwa kupata tiketi ya ccm aigombea urais.

  Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM ni Mwenyekiti wa Taif Rais Jakaya Kikwete, Makamu Bara Bw. Pius Msekwa, Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Iddi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. Chiligati, Vuai Ali Vuai.

  Hapa Lowassa hatoki.Kwa mujibu wa taratibu za CCM Kamati ya Maadili inaweza kuchukua hatua moja kwa moja au kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu (CC) ambayo pia wajumbe wake karibu wote wanaingia pia kuyabariki.Unaona ilivyokuwa ngumu,na kamati kuu ik kipindi kile aliivunja makusudi ili aidhibiti kwa kuteua watu watiifu kwake kama kina mohammed seif khatibu(wamekua pamoja toka TANU youth league seif akiwa mwenyekiti),zakia meghji,mzee wasira,bingwa wa siasa za ccm mh.kinana n.k. sioni lowassa anapona vipi labda ndio huo mpango wa kuigawa ccm vitoke vyama viwili ufanikiwe,maana ana wa nec na wabunge wa kutosha,we can't deny this!
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Ok mkuu, lets wait and c...
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kumbe Nape naye ni mpiganaji? Mi nilikuwa sijui hili!
   
 11. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Karolit man at work,
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  yah! ni wa ufisadi ndani ya ccm................
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Si rahisi kukata tawi la mti ulolikalia...
   
 14. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alilipwa ngeleja na malima kila mmoja thamani ya msaada wa chama kwa janga la mafuriko
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Sijakupata vyema mkuu.
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hata mimi sijamsoma mchizi,sijui alikua ana maanisha nini ati....
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  mla denda mashuhuri
   
 18. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Taarifa za kiintelijensia tulizonazo ni kwamba CCM walienda kuomba msaada kutoka kwa Bakharesa ili wakavikabidhi vyakula hivyo kama wao ndio wamevitoa!
   
 19. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwita Maranya,
  Unajua rafiki yangu ukichukua wanafunzi wa darasa moja kutoka shule zote nchi nzima waliokuwa wa mwisho katika Muhula flani wa masomo then ukawakutanisha na kuwashindanisha kwenye mtihani mwingine lazima kuna mmoja wao ataibuka kidedea! Ndivyo NAPE alivyo Mpiganaji ndani ya CCM!

   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yah kweli kabisa ndio maana akathubutu hata kumvaa lowassa na rostam kuwataka wajivue gamba na matokeo yake nadhani mmeyaona,rostam hatunae tena,kabla ya hapo nani aliweza kuwa na ujasiri wa kuwasema 'vibaya" hawa mafisadi papa...so far nape amefanya kazi kubwa ndio mana hata chadema amewatingisha na wanamuona ni tatizo wanapambana nae humu,hiyo ndio siasa ya vyama vingi ya ukweli,hutegemei chadema kumpongeza mtu wa ccm....zamani ukisikia kupinga ufisadi ndani ya ccm walikua ni chadema kina zitto,slaa n.k.nape akasema hapana kwa nini niwaachie chadema kazi ya kukisafisha chama changu????akasema kazi hiyo nitaifanya mimi sasa na ameweza nasema,Kinara wa ufisadi rostam leo hayupo kutokana na siasa "uchwara" za nape
   
Loading...