Nape aipa tano Kurugenzi ya Mawasiliano na Habari Ikulu

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Dar es Salaam. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano

Nape ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kumwagiza mkurugenzi wa habari maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii.

Akizungumza leo (Jumatano) Waziri Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawaziliano Ikulu na idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni uungwana kumpongeza mtu anayefanya vizuri. Ni uungwana pia kumkosoa anapokosea
 
Lakini baadhi ya taarifa anazosambaza mkurugenzi huyo wa Ikulu huwa zina makosa mengi ya typo, factual na mengine yasiyosameheka.
Ajirekebishe awe makini zaidi.
 
Ni aibu kubwa sana kwa viongozi wa Serikali na hasa Rais na RC wa Dsm Kujikomba komba clouds media kwa kila jambo.
Badala ya kuiboost TBC ndio mnaimaliza kabisa.
Nape mweleze Sizonje na Daudi.
 
Sio kuikomba komba inamaanisha mkuu mwenyew hana trust na iyo TBC yao

Maana kila siku clouds hajawahi piga simu uko tbc au kubeep basi labda tuseme kakosea namba.......wala hajafanya ivyo
 
Dar es Salaam. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano

Nape ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kumwagiza mkurugenzi wa habari maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii.

Akizungumza leo (Jumatano) Waziri Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawaziliano Ikulu na idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali.

Chanzo: Mwananchi
Za trump na kumsifia father jesca hazikupitia ikuru nini
 
Back
Top Bottom