Nape afunguka kuhusu mzee sabodo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape afunguka kuhusu mzee sabodo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wamapalala, Jul 9, 2012.

 1. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  ​ASEMA MZEE HUYO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO.

  [​IMG]
  "Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema.

  Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.


  Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote haya yamefanywa na serikali ya CCM.


  Sasa kama serikali ya CCM imefanya hivyo, cha ajabu hapa kwa mwanachama wake kufanya hivyo ni nini? Hivi kwanini tunataka kuwafikisha watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!


  Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!! Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni nini?!


  Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!",Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema katika taarifa yake..

  [​IMG]
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicheka bila uhasama na viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.  Habari kutoka Daily Nkoromo Blog.


  ​
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Kwani hata akiwa na kinyongo ata sema? Bali usishangae tukamkuta mzee wa watu kwenye poli la mwabe pande!

  Nape anasema mdomoni tu lakini moyoni hana amani na hawezi kufurahishwa na hicho kitendo hata mara moja!

  Tuna jua sasa hivi hawaongei ni mwendo wa kuhakikisha msitu wa pande una jaa!
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Nape bwana! He thinks he can say anything to and for everyone! Yale yale ya NEC imebariki kazi ya rais, do they have the mandate?
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Pamoja na mapungufu yake, katika hili ameongea vizuri. Namuunga mkono Nape, hapa ameamua kuachana na siasa za kufuata upepo. Ameamua kujipambanua yeye as an individual. Maana wengi wa wanaCCM wana kinyongo sana na huyu mzee, but yeye ameamua kutoa hisia huru. Tumpongeze kwa hili.
   
 5. i

  iseesa JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapa nami namuunga mkono Nape. Huu ni ukomavu wa Kisiasa kwa sababu hata CCM nayo imevilea vyama vya siasa bila kinyongo kwa kuvipatia RUZUKU kupitia kwa serikali zake.
   
 6. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninaamini Nape bado ni mwanasiasa mzuri, ila kwa kukubali kutetea na kuyasimamia mapungufu ya chama chake bila kukikosoa hapo ndipo palipomuweka pabaya. Kama CCM ingekuwa na dhamira ya kweli ya kujirekebisha na kudhibiti ubadhilifu ndani ya chama na serikali, hakika leo Nape angekuwa juu sana kisiasa.
   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,844
  Trophy Points: 280
  LAzima nape uongee maneno laini kwa mukubwa asije akachukia vinginevyo.............
   
 8. N

  Nambombe Senior Member

  #8
  Jul 9, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera Nape,hapo umeongea
   
 9. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kaongea kama yeye au ni mtazamo wa magamba? maana anasema mimi sioni tatizo ........................
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nafikiri huu ni mtizamo wake binafsi. Sidhani kama ni msimamo wa magamba.
   
 11. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanasiasa bana wenyewe wanafuraaaaahi! :happy:

  Wananchi kazi tunayo
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  KUDOS Nape kwa kauli yako hiyo ...... Mara chache huwa unajipambanua na akili mgando za wana Magamba Oooops Mabwepande
   
 13. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,886
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 180
  swafi Nape..kama huwezi kushindana nao, ungana nao tu mdogo wangu
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Amekuwa au changa la macho?
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mhhhhhhhhhhh! Kweli siasa haina mwenyewe!
   
 16. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa sio ugomvi,ni uelewa mfinyu tu ndio huzaa ugomvi wa kisiasa,humanity remains the same no matter political differences
   
Loading...