Nape aandaa waraka wa kuwakana CCM

Bora NNAPE arudie ukuu wake wa wilaya kule Masasi lasivyo kachemka kwa hawa watu,
 
Uzuri sisiemu Zanzibar wanausemi wao wansema " CCM MAPINDUZI DAIMA''falsafa ya msemo huu ukiitumia huku bara ndio kusema CCM HAIN MWENYEWE,ingawa watu walijisahaulisha na kuanza kuimba huyu mwenzetu.Kwa sasa nyimbo hizo azina mashiko,rejea mwalimu alipotaka kuludisha kadi ya CCM kaw kusema CCM sio mama yake,hivyo kama Mwalimu hakudiriki au kuwazia kuwa CCM ni mali yake pamoja na kumilki kadi na moja.Nani anaweza kusema CCM ni mali yake.Huyo atakae ibuka tunaomba wana CCM wamuulize awatajie namba ya kadi yake.Kitakachofuata afunguliwe hotuba ya Mwalimu kuwa CCM sio Mama yake.Kama mwasisi chama sio mali yake wewe nani useme CCM mali yako.

Yanayoendelea sasa ni mapinduzi daima,kama wangeekuwa wasikivu wangetoka kimya kimya na kujituliza pembeni kusubiliwa watu wengine waelevu watakao thamini mchango wenu na kuangalia madhambi ya zama zile kama mitihani ya kipimo cha ubinadamu, na si dharau na mabezo.
 
Siku 90 ndio zilitolewa na haikuwa inamaanisha kuwa akina EL,RA na AC waondoke CCM. Waliambiwa kuwa wajiangalie, kama wanafit CCM wabaki na kama wanaona hawafiti wahame!Wameonyesha kuwa still wanahitajika, na mchango wao ni mkubwa kwa taifa. Sasa nyie mnataka waondoke waende wapi?


Aisee akili yako inafanana na avatar yako yaani kama kulwa na doto
 
Nnape jitokeze mkuu uchangie hii mada.
atawaambia hivi "haya ni masuala ya ndani chama na yatamalizwa na vikao halali vya chama, kwa hiyo tuwe na subira wananchi, nia yetu ya kujivua gamba ipo palepale, hatutajali dini, rangi, cheo, umri wala kabila ya mtuhumiwa - fagio la chuma litafanya kazi yake". mwisho wa kunukuu wa hisani ya nape.
 
Sasa ndugu zangu naomba mnisaidie maana huu mziki hauchezeki hata kidogo uwanjani, jamaa ndo hao wanaonekana
hawayumbi kwa maneno ya ndugu yangu NAPE sasa afanyeje maana tunataka tuijenge nchi japo NAPE hakuwa muwazi wa
kuomba mawazo ya msaada kwa hili suala, uwezo wake umeishia hapo SASA AFANYEJE MAMBO YAMEKUWA MAGUMU
NA SIKU NDO HIZO ZINAISHA BILA MATOKEO CHANYA KWA WATZ NA CCM ILIYOMTUMA KWA GHALAMA KUBWA JAPO KAZI
HAIJAFANYIKA....

Mkuu huu mziki unachezeka kabisa, kinachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu. Mguu ukipata saratani unakatwa ili kuokoa saratani kuenea mwili mzima na kuleta kifo.Ili kuikoa nchi yetu na angamizo la ufisadi lazima CCM wachukue uamuzi mgumu wa kuwaondoa mafisadi wote na siyo hao watatu tu, waanzie na gamba kubwa yaani JK,kwani yeye ndiye mlezi na mtetezi mkubwa wa mafisadi kwa kuwa yeye ni zao la ufisadi, ukipanda bangi lazima itaota bangi na kamwe siyo mchicha. JK aliingia madarakani kwa nguvu ya fedha ya mafisadi ambao leo hii ndiyo wanaitwa magamba, hii siyo sahihi hata kidogo. JK atimuliwe yeye na genge lake ndipo nchi itapona.
 
yaani small bado kubwa NAPE is very minute kwa ma giant and heavy weights kama EL na Rostam...
Duh kwa hiyo ni sawa na KIBAJAJI eti kithubutu kuvuta SEMI TELA na nyomi ya SEMENTI toka wazo. aisee...
 
Kwa kimombo watu kama Nape wanaitwa "barking cum attack dogs". Hata mbwa akiona chatu ubweka sana matokeo yake uishia kuliwa! Nape ataishia tumboni mwa mapacha watatu.
 
Si kwamba Nape alikuwa hajui kuwa hii kazi ilikuwa nzito, bali alitaka tu Wtz wamsikie akifikiri anajenga jina. Kama wenzangu walivyotangulia sema hapo juu ukitaka kusimama na kuzungumzia uzuri wa ccm nyakati hizi lazima ujifanye kichaa sana si kidogo na Nape kajifanya kichaa kwelikweli.
 
yaani small bado kubwa NAPE is very minute kwa ma giant and heavy weights kama EL na Rostam...

Nadhani toka mwanzo Nape alionyesha kukosa adabu, hawezi kulumbana na watu rika ya babake tena waliofanya kazi nae wakati wa uhai wake. Hapa alitumika na akatumika vizuri tu, huku akiweka mbele tamaa ya maslahi binafsi bila kujali utu na heshima za kibinadamu.
 
zikiwa zimebaki siku 8 tangu rostam, lowasa na chenge kupewa siku 90 na ccm ikiongozwa na mwenyekiti wa itikadi na uenezi ndg nape nnauye kujiondoa wenyewe, mambo yamekuwa tofauti na ccm walivyofikili,watanzania wakiwa na imani kubwa sana na hawa viongozi waliowekwa baada ya ile secretariet ya zamani iliyokuwa ikongozwa na makamba mzee na kuwekwa hii inayoongozwa na ndh wilson mkama pembeni yake akiwepo nape, kiukweli mambo si mambo ndani ya ccm sasa kwani kila mmoja anashindwa atawaondoeje hawa wanaowaita magamba wakati mda wenyewe unakaribia kuisha wa siku 90,,,

nape kipindi anaingia katika hii nafasi alijua ni kazi rahisi sana ila kumbe mambo yamekuwa magumu tena sana kwani kati ya rostam,lowasa na chenge hakuna hata mmoja anaekumbuka kuwa
ana deni lakulipa kwa ccm ili ccm isiendelee kudaiwa na wananchi kile walichowaahidi cha kujivua gamba mnamo tarehe 10 april mwaka huu,,,

kwa hali hii inambidi nape aandae walaka wakuwajibu makada wa ccm na watanzania kwa ujumla ili ile kazi aliyopewa kuhakikisha kuwa analiondoa gamba ndani ya ccm inakamilika au aandae walaka wa kuwakana ccm na watanzania kuwa hakupewa hiyo kazi japo alipewa fungu la kutosha la kuhakikisha gamba linavuliwa,alipewa gari lakifahali kutembea tz nzima,alipewa ulinzi wa kutosha ili asipate tatizo lolote kutoka kwa maadui (magamba), sasa je siku ndo hizo zimebaki 8, je nnape ameandaa nini cha kujibu wakati hakuna hata gamba moja lililong'oka??????

je haya magamba yatambakiza nnape ndani ya ccm mara baada ya kushindwa kuyang'oa????
alishakana zamani kuwa hajawahi kutoa siku 90 kwa mafisadi.
 
Mkuu huu mziki unachezeka kabisa, kinachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu. Mguu ukipata saratani unakatwa ili kuokoa saratani kuenea mwili mzima na kuleta kifo.Ili kuikoa nchi yetu na angamizo la ufisadi lazima CCM wachukue uamuzi mgumu wa kuwaondoa mafisadi wote na siyo hao watatu tu, waanzie na gamba kubwa yaani JK,kwani yeye ndiye mlezi na mtetezi mkubwa wa mafisadi kwa kuwa yeye ni zao la ufisadi, ukipanda bangi lazima itaota bangi na kamwe siyo mchicha. JK aliingia madarakani kwa nguvu ya fedha ya mafisadi ambao leo hii ndiyo wanaitwa magamba, hii siyo sahihi hata kidogo. JK atimuliwe yeye na genge lake ndipo nchi itapona.

Mie siamini kama JK ni gamba maana alifanya maamzi magumu ya kuvunja baraza la mawaziri kipindi cha LOWASA kama alivyosema Pinda..
 
Niliwahi kuseam hapa kuwa RA.CH.EL hao ndio roho ya CCM. Ukimwacha CH, hawa wengine kwa lugha ya nyepesi ya wakenya wanaitwa "masonko" (matajiri waliopindukia) mf. RA kupitia kampuni lake moja la mawasiliano nasikia sijui kama ni kweli kuwa anatengeneza faida ya 5b kwa siku. Wakitoka hawa ccm basi chama watakachokianzisha kitakomba wafuasi wote wa ccm. Kumbuka ule msemo unaosema "hapendwi mtu inapendwa pochi"
 
Nape hana habari kuwa ametolewa kama Mbuzi wa sadaka,mtu mjanja anamtumia kama mpiga tarumbeta wake yeye kashindwa,atawaachaje maswahiba wake?wakati asingekuwepo pale bila wao.
 
ninanvyofahamu na imekuwa ikirudiwarudiwa na katibu mukama na kamanda mwenyewe nape.watu wale walipewa siku 120 na sio 90 na kama wakishindwa kuwajibika wao wenyewe halmashauri kuu ya ccm itawawajibisha.na nape mwenyewe amekuwa akikanusha juu ya siku 90.hivyo tusubiri muda bado.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom