Nape aandaa waraka wa kuwakana CCM

Nape aandaa waraka wa kuwakana CCM

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
646
Reaction score
1,225
Zikiwa zimebaki siku 8 tangu ROSTAM, LOWASA NA CHENGE kupewa siku 90 na CCM ikiongozwa na mwenyekiti wa itikadi na uenezi Ndg NAPE NNAUYE kujiondoa wenyewe, mambo yamekuwa tofauti na CCM walivyofikili,watanzania wakiwa na imani kubwa sana na hawa viongozi waliowekwa baada ya ile secretariet ya zamani iliyokuwa ikongozwa na Makamba mzee na kuwekwa hii inayoongozwa na Ndh Wilson mkama pembeni yake akiwepo NAPE, kiukweli mambo si mambo ndani ya CCM sasa kwani kila mmoja anashindwa atawaondoeje hawa wanaowaita magamba wakati mda wenyewe unakaribia kuisha wa siku 90,,,

Nape kipindi anaingia katika hii nafasi alijua ni kazi rahisi sana ila kumbe mambo yamekuwa magumu tena sana kwani kati ya ROSTAM,LOWASA NA CHENGE hakuna hata mmoja anaekumbuka kuwa
ana deni lakulipa kwa CCM ili CCM isiendelee kudaiwa na wananchi kile walichowaahidi cha kujivua gamba mnamo tarehe 10 April mwaka huu,,,

Kwa hali hii inambidi NAPE aandae walaka wakuwajibu makada wa CCM na watanzania kwa ujumla ili ile kazi aliyopewa kuhakikisha kuwa analiondoa gamba ndani ya CCM inakamilika au aandae walaka wa kuwakana CCM na watanzania kuwa hakupewa hiyo kazi japo alipewa fungu la kutosha la kuhakikisha gamba linavuliwa,alipewa gari lakifahali kutembea TZ nzima,alipewa ulinzi wa kutosha ili asipate tatizo lolote kutoka kwa maadui (MAGAMBA), sasa je siku ndo hizo zimebaki 8, JE NNAPE ameandaa nini cha kujibu wakati hakuna hata gamba moja lililong'oka??????

JE HAYA MAGAMBA YATAMBAKIZA NNAPE NDANI YA CCM MARA BAADA YA KUSHINDWA KUYANG'OA????
 
Nape mwepesi mno...hawezi shindana na heavy weight akina lowassa, rostam na chenge....hilo analijua ila mwanzoni alidhani ni kazi rahisi sana.
 
where are you "nnauye jr",

njoo ujitetee.



Huyu ndugu yangu NNAPE bora angeendelea na ukuu wake wa wilaya kule Masasi hili ziko ni zito sana
kwani waliolibeba wako pembeni wamemtoa kama kafara vile,, ndugu yangu NNAPE litue hili zigo kwani tayari limekuelemea, pole sana my brother...
 
Unajua kuna kauli nyingine ni burudani tupu hata kuzisikia. Hivi ni nani aliyetarajia kwamba CCM ingewaondoa akina Chenge, Lowasa na Rostam ilihali hao ndo wanaodetermine uhai wa CCM? Hawa ndiyo wafadhili wakuu wa CCM na ndiyo wanaoongoza nchi kwa mgongo wa JK, sasa ni nani mwenye ubavu wa kuwaondoa, ili hali kikwete mwenyewe ni kama remote control iliyoshikiliwa na Rostam? Kama alishindwa kumshitaki na kumfunga pale alipokwapua mabilioni through Kagoda, leo atamfunga kwa lipi? Ndiyo maana huwa siku zote nasema CCM got the strategy wrong. Gamba kuu la CCM ni kikwete na huyo ndiye aliyetakiwa atolewe CCM na si hawa watatu. Hadi hapo CCM itakapoweza kutenganisha uongozi wa nchi na wa chama ndipo kitakapoweza kuendesha serikali kwa umakini na si vinginevyo.
 
Whoz gamba? LA,EL au chenge? Cal them vigogo! They run CCM.....

For real these are not gamba, they are so strong myfriend, nadhani ukiitaja CCM bila hawa watu hiyo CCM ni batili, hawa ndoo vigogo, hawa ndio CCM,,,,,,,
 
Yealekea Nape hakujua ni nani aliyemwajiri huyo mwajiri wake. Hajui kana kuna Kings makers humu duniani.
 
Siku 90 ndio zilitolewa na haikuwa inamaanisha kuwa akina EL,RA na AC waondoke CCM. Waliambiwa kuwa wajiangalie, kama wanafit CCM wabaki na kama wanaona hawafiti wahame!Wameonyesha kuwa still wanahitajika, na mchango wao ni mkubwa kwa taifa. Sasa nyie mnataka waondoke waende wapi?
 
Nape huwa anakufa na kufufuka, hataonekana amekufa na ataibukia (atafufukia) ktk mada ingine isiyo na mashiko kama mtu asiye nazo. Kushabikia ccm mpaka uwe hamnazo kama tambwe hiza
 
Wapi MS,FF,Ecol,Ritz,Tumaini, Nnauye jr na wengine? Tunahitaji kauli zao?
 
RACHEL ni korodani za ccm, si magamba. Kama wana ubavu wazikate basi
 
Siku 90 ndio zilitolewa na haikuwa inamaanisha kuwa alina EL,RA na AC waondoke CCM. Waliambiwa kuwa wajiangalie, kama wanafit CCM wabaki na kama wanaona hawafiti wahame!Wameonyesha kuwa still wanahitajika, na mchango wao ni mkubwa kwa taifa. Sasa nyie mnataka waondoke waende wapi?
Ulikuwepo kwenye kikao hicho au ulisikia kama ilivyo kwa watz wengine?
 
Nape huwa anakufa na kufufuka, hataonekana amekufa na ataibukia (atafufukia) ktk mada ingine isiyo na mashiko kama mtu asiye nazo. Kushabikia ccm mpaka uwe hamnazo kama tambwe hiza
Modz wapi kitufe cha senkyu? Kama modz mnacho huko mgongeeni huyu Mkuu! Kwa niaba yangu pulizzz! Amenikuna.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom