Nape aahidi kurudisha heshima tasnia ya habari

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema atahakikisha heshima ya tasnia ya habari inarudi hasa baada ya kupitishwa kwa muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari.

Waziri Nape alitoa ahadi hiyo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Mara na Shinyanga ambapo pia alipokea taarifa ya mikoa na kuwapatia vitendea kazi maofisa mawasiliano wa mikoa hiyo.

“Ule muswada utatoa tafsiri ya mwandishi wa habari, maana mwandishi wa habari lazima awe na sifa. Siku hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi halafu akajifunza kupiga picha, akajiita na yeye mwandishi wa habari. Ukifanya hivyo tasnia hii inakosa heshima, kwa hiyo sheria ile itatafsiri nani mwandishi wa habari,” alisema Nape.

Alisema sheria hiyo itatibu tatizo la waandishi wa habari kutolipwa stahiki zao ipasavyo na wamiliki wa vyombo vya habari huku ikisisitiza pia suala la elimu kwani ni lazima mmiliki wa chombo cha habari aajiri mtu mwenye taaluma na siyo kuokota kijiweni.

Waziri Nape aliwaasa waandishi wa habari na watangazaji wa redio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha Watanzania kupitia kalamu zao na vipindi vya vya redio au luninga na siyo kuwatenganisha.

Alitoa mfano wa yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari kwamba redio zilitumika kuhamasisha mauaji. Waziri Nape aliahidi pia kuimarisha vitengo vya mawasiliano serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapa maofisa hao vitendea kazi. Waziri Nape yupo katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera, Mara, Shinyanga, Tabora na Singida.
 
Haituhusu
 
Nampongeza naamini mswada wa Sheria mpya utakapopitishwa utafungua ukurasa mpya ikiwa sheria itafuatwa ipasavyo.
 
Back
Top Bottom