Naota serikali kubadili gia angani kuhusu baa la njaa. Sasa kukubali njaa ipo!!

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,121
Baada ya watu mbali mbali kupaza sauti kuhusu baa la njaa. akili yangu inaota ndoto za mchana na kuona muda si mrefu watakanusha kauli ya mkuu wa nchi na kusema hatukumwelewa.

Rais amesema hamna njaa asiye weza kununua chakula kwa bei kubwa kama kufwa na afwe!! Hata ikibid debe moja tubadilishane na ng'ombe watatu. Yaan wenye chakula wapandishe bei kadri wawezavyo!! Asiye weza kununua akalime chakula chake . Na asiwepo mtu wa kuingilia bei safari hii akamalizia kwa kusema kufa kufaana!!

Sasa hivi naota mawaziri watakuja kuokoa jahazi na kusema hizi kauli zilikua utani kwa vile rais alikua maeneo ya nyumbani lakn njaa ipo na uhaba wa chakula upo ila kufa kwa njaa watu hawatakufa tutawapa chakula. Watakuja kusema kauli ya rais kusema hatogawa chakula ilikua ni msisitizo ili watu wafanye kaz na wajifunze kujitegemea. Kiukweli nategemea kauli kama hiz muda sio mrefu sana. Stay tuned mtaniambia.

Je kwa utendaji wa serikali hii ndugu mwana jf hutegemei viongozi wengine kuja kuweka mambo sawa baada ya mtukufu -------------- kutibua tibua???
 
ad17393c4e7e9a20aa4e354166155f9a.jpg
"Amna chakula cha bure"
 
Bunge ni Wakala wa Raia. Katika hali kama hili, kama kweli njaa ipo basi Bunge lisimame ktk nafasi yake, liwasemee Wananchi. Maana WaBunge Wanatoka kwa Wananchi.

Wasiposema maana yake nikwamba kweli njaa haipo huko kwa Wananchi au nawenyewe wameona hao wananchi Wacha Wakufilie mbali.
 
Aliyesema hamna chakula cha bure muulize kwamba yeye chakula anachokula ni cha bure or sio chabure
Tunakamuliwa kodi zooote ili kumlipia hela za chakula chake na familia yake, nguo, malazi, matibabu na starehe zake lkn anavyotutenda eti yeye ana madaraka.

Hivi Nyerere angetumia madaraka yake Leo hii tungemgusa kweli yeye na familia yake?

Ulevi Wa madaraka ni shida Afrika
 
Njaa bado haijakolea ndo maana tunasema hakuna njaa. Ikishakolea tutakimbilia jikoni
 
Back
Top Bottom