KUOTA NAPAA MARA KWA MARA...
Mambo vipi ?
Nimekuwa na tabia ya kuota NAPAA mara Kwa mara Toka zamani na kucheza michezo ya kupaa sehemu mbalimbali aswa kwenye milima,miti yaani naota nafurahia balaa kupaa kitu ambacho watu wengine wanakuwa hawawezi na sa zingine unakuta tunafanya kitu kama kutembea au kuchuma matunda kwenye miti pale ambapo wenzangu nawapigia ni kupaa tu na unakuta nawashinda .
Na hii kitu naota zaidi ninapolala Kwa kuangalia juu .
Tafsiri ya iyo ndoto sijui ni nini, wataalamu wenye uwezo WA kutafsiri ndoto nisaidieni kunipa tafsiri.
Maelezo Ya Ndoto
Hakika wewe ni mtu upendwaye na Mungu
Mistali Wa Kusimamia
Isaya 40:31
[31]bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Maana Ya Ndoto
Mungu anakujulisha kuhusu status(Hali) Yako ya Kiroho kuwa wewe ni Mtawala na ni Mtu Mwenye Nguvu.
Kupaa Juu ya milima inamaanisha Kuwa Kiongozi(kidini / kiserikali)
kupaa Juu ya Miti yenye Matawi.. nikuwa juu ya watu wenye uwezo wa kuzarisha sana (biashara/ kiroho)
Na mwisho una neema Ya kuwasaidia Wengine kuweza kufika Juu..
Mwisho
Unahitaji kukaa karibu Sana Na Mungu ili aweze kukujuza nikipi unacho takiwa kukifanya ili uweze kufikia hapo
Nimalize kwa kusema
Kutafsiri Ndoto ni kazi ya Bwana mwenyewe.
Mkabizi Mungu njia zako nawe utathibitika
Mwanzo 40:8
[8]Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.
Waweza kujiunga na Chanel yetu Whatsapp
πSiri za Ndoto / Secrets of Dreams | WhatsApp Channel