Naona upotoshaji mkubwa juu ya historia ya mwanadamu na kila kinachoendelea ilimwenguni

April7

Member
Aug 5, 2019
36
70
Wakuu salamu zenu, awali ya yote naomba radhi kwa yeyote atakayekwazika kwa namna yeyote na uzi huu. Niko hapa jukwaani kuelezea baadhi ya mambo yanayotuzunguka katika jamii zetu kwa kuyatengenezea maswali na kuyajibu kwa hoja na so kufuata vile ambavyo tumeaminishwa.

Tofauti ya kimaendeleo kati ya mtu mweusi na mtu mweupe inanipelekea nifikiri tofauti kuhusu historia ya mwanadamu kiujumla. Mfano mdogo tu, taifa langu pendwa la Tanzania (zamani Tanganyika) mpaka wakati huu (2021) wastani lina watu milioni 64, lakini wakati mkoloni analiacha huru taifa hili (1961) aliliacha na watu milioni 9 tu.
Mwaka 1964 baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja taifa lilikuwa na watu milioni 12. Toka mwaka 1964 mpaka 2021 imepita miaka 57 lakini ajabu taifa limepata ongezeko la watu milioni 52.
Ukakasi wangu unakuja hapa; ikiwa tangu Tanzania izaliwe mwaka 1964 ikiwa na mtaji wa watu milioni 12 lakini ndani ya miaka 57 taifa limeongeza watu milioni 52, sasa tangu mwaka huohuo wa 1964 tukirudi miaka 57 nyuma hivi hili taifa lilikuwa na watu wangapi?.
Ukakasi mwingine unakuja kwenye usawa wa binadamu, mawazo yangu yananipelekea kuwa mtu mweupe hayuko sawa na mtu mweusi kwenye kila nyanja, kuanzia muonekano, kufikiri, kuamua n.k.
Mtu mweusi kawa mnuonge kwenye huu ulimwengu, anapangiwa kila kitu na mtu mweupe na lazima atekeleze eidha kwa kupenda au kutopenda. Mtu mweusi hana tofauti na mnyama wa kufugwa.
Mimi nahisi mtu mweupe alikuwepo kwa mda mrefu kwenye huu ulimwengu kwa miaka mingi sana kabla mtu mweusi hajatokea au yawezekana mtu mweusi ni zao la mtu mweupe na ndio maana mtu mweupe anamtumikisha mtu mweusi vile atakavyo.
Jamani kwa historia zote zinazomuhusu mwanadamu, mtu mweupe anaonekana shujaa kwenye kila kitu pia kutokana na ukale wa ulimwengu wa mwanadamu na uchache wa mtu mweusi na wingi wa mtu mweupe ukikokotoa haileti uwiano wa kimahesabu.

Nikija kwenye mambo ya imani/dini huku nako kumejaa ukakasi mwingi mno, nimevisoma vitabu viwili vya kiimani ya kikiristo na kiislamu ( Biblia na Qur'an ) lakini baadae nikaja kugundua hivi vitabu muandishi ni mmoja/kundi moja kwa maana yaliyomo kwenye hivyo vitabu ni kitu kimoja, au muandishi mmoja alikopi kwa mwingine na kupaste kwake.
Ukakasi wa mambo ya kidini unaanzai kwa mungu mwenyewe, kwa uwezo wangu wa kutafsiri mambo nimekuja kumtafsiri mungu wa kwenye hivi vitabu hajui anachokitaka na pia hana ukubwa, busara, huruma wala chochote alichotajwa nacho kwenye hivyo vitatbu.
Mfano mdogo tu wa ukakasi wa mungu wa kwenye biblia ni huu;

"Mungu mkuu (Yehova) alikuwa na uwezo wa kuufanya msitu wa Amazon kuwa taifa lake teule (Israel), lakini kwa mapenzi yake akawaamuru wana wa Israel kuvamia makazi ya watu wengine na kupora mali zao ili waifikie nchi ya ahadi (Palestine)
Ikumbukwe na hao waliovamiwa na kuporwa pia wameumbwa na huyohuyo (Yehova), hizo ni busara za Mungu mkuu.
Mpaka wakati huu kuna mapigano yanaendelea pale Palestine/Israel kwasababu ya ahadi ya Mungu mkuu kuwaagiza wana wa Israel kuelekea nchi ya ahadi (Palestine).
Kuna maeneo mengi sana ambayo hayakaliwi na watu, ambayo wana wa Israel wangepelekwa na Mungu ili atimize ahadi yake kwao, lakini aliwapeleka mahali ambapo pana makazi ya watu wengine. Je! Mungu alitaka kuwagombanisha watu au hapendi kuwaona watu aliishi kwa utulivu? Hapana Mungu ni mwingi wa busara na hekima.
Aibarikie Israel naye atabarikiwa, na aliaaniye naye atalaaniwa na Mungu mkuu
."

Pia ukiisoma abari ya ujio wa Yesu ni changamoto nyingine juu ya busara za mungu;

"Safari ya Yesu ilikuwa imepangiliwa kila kitu na Mungu mwenyewe, yaan kuanzia kuzaliwa, hatua za ukuaji mpaka kuteswa kwake hadi kufa. Biblia takatifu katka kitabu cha Luka, Marko na Yohana vimemuelezea kinaga ubaga huyu mpakwa mafuta (masihi).
Watu kama Kefa (Petro/Peter), Yuda Iskariot, Herode, Zakayo na wengine wengi katka maandiko yaliyomzungumzia Yesu ni wahusika ambao Mungu mwenyewe aliwachagua ili lije litimie agano la kukombolewa kwa ulimwengu kupitia mwanae wa pekee ambaye ni Yesu.
Tumaini langu ni kuona/kusikia hawa wahusika wakitajwa kwenye maandiko kuwa siku moja wote watakaa upande wa kuume wa bwana kwa maana walitimiza andiko la bwana la kutaka ulimwengu ukombolewe kupitia damu ya Yesu bila kubagua wahusika.
Yaan haijalishi Yuda Iskariot alimsaliti Yesu au Herode/Pilato walimuhukumu Yesu kwa maana hao wote walikuwa katika mpango wa Mungu wa kitimiza neno lake, wale wahusika wanaoonekana walikuwa waovu kwa Yesu kiuhalisia hawakuwa waovu kwa matakwa yao bali walikuwa programmed (kupangiliwa cha kufanya) na Mungu mwenyewe
".

Kwa hakika Kuna mambo mengi ya kufikirisha juu ya maisha ya ulimwengu huu, husuan kwenye hili suala la imani lina wahanga wengi na hapa natarajia kuitwa kafiri, mpagani, mpinga kristo/masihi dajali na majina yote mabaya.
 
Mim naamini hizi dini tumeletewa tu waafrika hatuna dini.mim naabudu mizimu yaani wahenga wa kale waliotangulia.
 
Maisha ni fumbo gumu sana. Kwa jinsi ninavyozidi kusoma mabandiko mbalimbali nazidi kujifunza hamna ajuaye tumetoka wapi, ingawa dini ndiyo imekuwa na mashiko zaidi ikifuatiwa na Sayansi.
Lakini bado naona umuhimu wa dini kwa sababu bila dini binadamu tungekuwa zaidi ya wanyama.
 
Kati ya ngozi nyeupe na nyeus naweza kufananisha na wanyama mwituni, tufanye Simba ndiyo mzungu, chui ndiyo mchina, fisi ni mjerumani na muafrika ndiyo swala. So katika ulimwengu kuna Superior na inferior katika viumbe wote. Hata kwa wadudu iko hivo spider anakula wadudu wanaokuwa traped kwenye mitego yake. Ila kwenye dini huko na Mimi najiuliza maswali kama yako mkuu.
 
Hiyo mizimu ndio dini zenyewe mkuu, kumbuka hata hao wazungu/waarabu wanaabudu mizimu pia, kwa uelewa wangu mizimu ni roho za watu ambao walishawahi kuishi kwenye ulimwengu huu and then wakafa, so that wakristo wanavyomuomba Yesu hakuna utofauti wa muafrika anavyowaomba mababu zake waliokufa miaka mingi.

Watu kama waarabu wanamtukuza Muhammad na wanaomba dua kwa jina lake, kumbuka Muhammad alishakufa miaka elfu iliyopita hivyo hakuna tofauti na kuomba mzimu.

My take about this religion; hawa miamba waliotuletea hizi dini walituzidi/wametuzidi nguvu nyingi sana na ndio maana wakapata hata nguvu ya kututawala na kutuambukiza tamaduni/dini zao, laiti ingekuwa na sisi( waafrika ) tungekuwa na nguvu hiyo pamoja na tamaa ya kuwatawala hao watu weupe maamini tungewaambukiza hizi imani za kiafrika ambazo leo waafrika wenyewe tunaziita shirki/kufuru kwa mungu Allah/Jehova.

Tafsiri yangu kuu kuhusu dini ni; Dini ni tamaduni kuu ya jamii fulani ya watu ambayo imekusanya kila aina ya imani na kuitegemea. Na ndio maana ukiitazama dini ya kiislamu kuanzia mavazi, lugha na namna ya kuabudu imebase kwenye maisha ya kiarabu halikadhalika na dini zingine ziko hivyo.

Wakati nasoma madrasat Su'udiyat mahali fulani Tanzania namkubuka vizuri mwalimu wangu wa kiroho marehemu sheikh masood kuwa siku tukifika peponi tutaishi maisha mzuri mno, kule kuna matunda ya kila namna vilevile kuna mito ambayo inatiririsha maziwa na asali, ikumbukwe pia kuwa hiyo mito kingo zake ni dhahabu. Lakini yote kwa yote kila mwanaume atakabidhiwa masuria/vigori/mabinti bikira 70 na wote utakuwa na uwezo wa kuwakidhi haja zao.

Nilimuuliza kuhusu wanawake wakifika peponi watapewa nini sikupewa jibu mpaka anafariki, pia kubwa kuliko sheikh aliniambia kuwa lugha ya mawasiliano huko peponi ni kiarabu. Kwa hayo tu utagundua kuwa uislamu ni tamaduni ya kiarabu kamwe haiwezi kuwa dini ya mungu anayemiliki ulimwengu wote huu kwa maana ikiwa hivyo basi mungu ni mbaguzi sana kwa maana kawarahisishia waarabu kufika peponi kuliko jamii nyingine yeyote
.

Kikubwa tutendeane yaliyo mazuri ili muendelezo uwe wa kutendeleana mazuri kwa faida ya wote na sio kutarajia kwenda peponi, pepo ambayo watu wachache wameiandikia script na kuipa kina aina ya sifa za kusadikika.
Mim naamini hizi dini tumeletewa tu waafrika hatuna dini.mim naabudu mizimu yaani wahenga wa kale waliotangulia.
 
Kinachonitatiza Mimi babu zetu waliabudu mizimu nk,ambayo hiyo mizimu iko katika ulimwengu Wa roho haionekani kwa macho ya nyama na walitenda miujiza kutokana na maombi ya babu zetu kila walichohitaji kwa wakati huo kama ni nvua waliomba mizimu,kwa hiyo naamini Mungu yupo na kuna maisha katika ulimwengu Wa roho wanaishi.
 
Sahihi mkuu, mungu ni asili na asili ipo kila mahali usipoijua asili yako watafika wengine watakupotosha ili wakutumie.
Kinachonitatiza Mimi babu zetu waliabudu mizimu nk,ambayo hiyo mizimu iko katika ulimwengu Wa roho haionekani kwa macho ya nyama na walitenda miujiza kutokana na maombi ya babu zetu kila walichohitaji kwa wakati huo kama ni nvua waliomba mizimu,kwa hiyo naamini Mungu yupo na kuna maisha katika ulimwengu Wa roho wanaishi.
 
Kuipata Historia halisi na ya kweli ni mtihani haswa.
 
Ni kweli, ila kubaini uwongo kwenye historia ni rahisi sana

Ebu cheki hii

Kwenye ishu ya mdau hapo juu alipozungumzia mpango wa Mungu kuwapeleka waisrael kwenye nchi ya ahadi ni mambo mengi ya kiuovu ambayo Mungu huyu alifanya

Wafuasi wa musa walipokutana na changamoto ya farao Mungu hakutunia busara kufanya suluhu.

Utakumbuka kuna muda aliagiza wapake damu ya kondoo juu kwenye milango yao na usiku atapita roho mtakatifu kukagua, nyumba ambayo itaonekana kutotii agizo hilo basi itapatwa na msiba kwa kufiwa na mtoto wa kwanza wa kiume.

Imagine mtoto ambaye hana hatia anauliwa na Mungu mwenye upendo wote kwa kosa la wazazi wao kutotii agizo la huyo Mungu

Imagine Mungu muweza wa yote anafanya haya ili kumthibitishia farao kua yeye ni mkuu, anadhuru viumbe visivyo na hatia na kumuacha farao mwenye hatia ili tu ashuhudie na kuona Mungu ni mkubwa

Hii stori mpaka hapo inaonesha wazi kua ni ya uongo, hauwezi kuwa na Mungu mwenye upendo wote na anayeua watoto wasio na hatia kwa wakati mmoja

Kibwagizo kingine kwenye safari ya musa na waisraeli kwenda israel ambapo hadithi zinasema walichukua miaka 40. Ukiangalia distance ya misri mpaka hapo israel ni kama KM 613 ambapo tunaweza kusema ni sawa na kutoka dar mpaka makambako

Lakini wakina musa walihitaji miaka 40 kumaliza hizo kilometer, by calculations kwa miaka 40 ni kwamba kila siku moja walikua wanatembea sentimita 30

Hii ni sawa na sekunde moja anayoitumia ussain bolt kwenye mbio, wafuasi wa musa walitumia siku nzima kuikamilisha.
 
Ili uweze kuzielewa hizi imani za majahazi inakubidi ujitoe ufahamu ulionao alafu usihoji chochote alafu amini unachoambiwa, na mtu yeyote mwenye hizo sifa tajwa hapo anajulikana kama mpumbavu.
Ni kweli, ila kubaini uwongo kwenye historia ni rahisi sana

Ebu cheki hii

Kwenye ishu ya mdau hapo juu alipozungumzia mpango wa Mungu kuwapeleka waisrael kwenye nchi ya ajabu ni mambo mengi ya kiuovu ambayo Mungu huyu alifanya

Wafuasi wa musa walipokutana na changamoto ya farao Mungu hakutunia busara kufanya suluhu.

Utakumbuka kuna muda aliagiza wapake damu ya kondoo juu kwenye milango yao na usiku atapita roho mtakatifu kugagua, nyumba ambayo itaonekana kutotii agizo hilo basi itapatwa na msiba kwa kufiwa na mtoto wa kwanza wa kiume.

Imagine mtoto ambaye hana hatia anauliwa na Mungu mwenye upendo wote kwa kosa la wazazi wao kutotii agizo la huyo Mungu

Hii stori mpaka hapo inaonesha wazi kua ni ya uongo, hauwezi kuwa na Mungu mwenye uoendo wote na anayeua watoto wasio na hatia kwa wakati mmoja

Kibwagizo kingine kwenye safari ya musa na waisraeli kwenda israel ambapo hadithi zinasema walichukua miaka 40. Ukiangalia distance ya misri mpaka hapo israel ni kama KM 613 ambapo tunaweza kusema ni sawa na kutoka dar mpaka makambako

Lakini wakina musa walihitaji miaka 40 kumaliza hizo kilometer, by calculations kwa miaka 40 ni kwamba kila siku moja walikua wanatembea sentimita 30

Hii ni sawa na sekunde moja anayoitumia ussain bolt kwenye mbio, wafuasi wa musa walitumia siku nzima kuikamilisha.
 
Wakuu salamu zenu, awali ya yote naomba radhi kwa yeyote atakayekwazika kwa namna yeyote na uzi huu. Niko hapa jukwaani kuelezea baadhi ya mambo yanayotuzunguka katika jamii zetu kwa kuyatengenezea maswali na kuyajibu kwa hoja na so kufuata vile ambavyo tumeaminishwa.

Tofauti ya kimaendeleo kati ya mtu mweusi na mtu mweupe inanipelekea nifikiri tofauti kuhusu historia ya mwanadamu kiujumla. Mfano mdogo tu, taifa langu pendwa la Tanzania (zamani Tanganyika) mpaka wakati huu (2021) wastani lina watu milioni 64, lakini wakati mkoloni analiacha huru taifa hili (1961) aliliacha na watu milioni 9 tu.
Mwaka 1964 baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja taifa lilikuwa na watu milioni 12. Toka mwaka 1964 mpaka 2021 imepita miaka 57 lakini ajabu taifa limepata ongezeko la watu milioni 52.
Ukakasi wangu unakuja hapa; ikiwa tangu Tanzania izaliwe mwaka 1964 ikiwa na mtaji wa watu milioni 12 lakini ndani ya miaka 57 taifa limeongeza watu milioni 52, sasa tangu mwaka huohuo wa 1964 tukirudi miaka 57 nyuma hivi hili taifa lilikuwa na watu wangapi?.
Ukakasi mwingine unakuja kwenye usawa wa binadamu, mawazo yangu yananipelekea kuwa mtu mweupe hayuko sawa na mtu mweusi kwenye kila nyanja, kuanzia muonekano, kufikiri, kuamua n.k.
Mtu mweusi kawa mnuonge kwenye huu ulimwengu, anapangiwa kila kitu na mtu mweupe na lazima atekeleze eidha kwa kupenda au kutopenda. Mtu mweusi hana tofauti na mnyama wa kufugwa.
Mimi nahisi mtu mweupe alikuwepo kwa mda mrefu kwenye huu ulimwengu kwa miaka mingi sana kabla mtu mweusi hajatokea au yawezekana mtu mweusi ni zao la mtu mweupe na ndio maana mtu mweupe anamtumikisha mtu mweusi vile atakavyo.
Jamani kwa historia zote zinazomuhusu mwanadamu, mtu mweupe anaonekana shujaa kwenye kila kitu pia kutokana na ukale wa ulimwengu wa mwanadamu na uchache wa mtu mweusi na wingi wa mtu mweupe ukikokotoa haileti uwiano wa kimahesabu.

Nikija kwenye mambo ya imani/dini huku nako kumejaa ukakasi mwingi mno, nimevisoma vitabu viwili vya kiimani ya kikiristo na kiislamu ( Biblia na Qur'an ) lakini baadae nikaja kugundua hivi vitabu muandishi ni mmoja/kundi moja kwa maana yaliyomo kwenye hivyo vitabu ni kitu kimoja, au muandishi mmoja alikopi kwa mwingine na kupaste kwake.
Ukakasi wa mambo ya kidini unaanzai kwa mungu mwenyewe, kwa uwezo wangu wa kutafsiri mambo nimekuja kumtafsiri mungu wa kwenye hivi vitabu hajui anachokitaka na pia hana ukubwa, busara, huruma wala chochote alichotajwa nacho kwenye hivyo vitatbu.
Mfano mdogo tu wa ukakasi wa mungu wa kwenye biblia ni huu;

"Mungu mkuu (Yehova) alikuwa na uwezo wa kuufanya msitu wa Amazon kuwa taifa lake teule (Israel), lakini kwa mapenzi yake akawaamuru wana wa Israel kuvamia makazi ya watu wengine na kupora mali zao ili waifikie nchi ya ahadi (Palestine)
Ikumbukwe na hao waliovamiwa na kuporwa pia wameumbwa na huyohuyo (Yehova), hizo ni busara za Mungu mkuu.
Mpaka wakati huu kuna mapigano yanaendelea pale Palestine/Israel kwasababu ya ahadi ya Mungu mkuu kuwaagiza wana wa Israel kuelekea nchi ya ahadi (Palestine).
Kuna maeneo mengi sana ambayo hayakaliwi na watu, ambayo wana wa Israel wangepelekwa na Mungu ili atimize ahadi yake kwao, lakini aliwapeleka mahali ambapo pana makazi ya watu wengine. Je! Mungu alitaka kuwagombanisha watu au hapendi kuwaona watu aliishi kwa utulivu? Hapana Mungu ni mwingi wa busara na hekima.
Aibarikie Israel naye atabarikiwa, na aliaaniye naye atalaaniwa na Mungu mkuu
."

Pia ukiisoma abari ya ujio wa Yesu ni changamoto nyingine juu ya busara za mungu;

"Safari ya Yesu ilikuwa imepangiliwa kila kitu na Mungu mwenyewe, yaan kuanzia kuzaliwa, hatua za ukuaji mpaka kuteswa kwake hadi kufa. Biblia takatifu katka kitabu cha Luka, Marko na Yohana vimemuelezea kinaga ubaga huyu mpakwa mafuta (masihi).
Watu kama Kefa (Petro/Peter), Yuda Iskariot, Herode, Zakayo na wengine wengi katka maandiko yaliyomzungumzia Yesu ni wahusika ambao Mungu mwenyewe aliwachagua ili lije litimie agano la kukombolewa kwa ulimwengu kupitia mwanae wa pekee ambaye ni Yesu.
Tumaini langu ni kuona/kusikia hawa wahusika wakitajwa kwenye maandiko kuwa siku moja wote watakaa upande wa kuume wa bwana kwa maana walitimiza andiko la bwana la kutaka ulimwengu ukombolewe kupitia damu ya Yesu bila kubagua wahusika.
Yaan haijalishi Yuda Iskariot alimsaliti Yesu au Herode/Pilato walimuhukumu Yesu kwa maana hao wote walikuwa katika mpango wa Mungu wa kitimiza neno lake, wale wahusika wanaoonekana walikuwa waovu kwa Yesu kiuhalisia hawakuwa waovu kwa matakwa yao bali walikuwa programmed (kupangiliwa cha kufanya) na Mungu mwenyewe
".

Kwa hakika Kuna mambo mengi ya kufikirisha juu ya maisha ya ulimwengu huu, husuan kwenye hili suala la imani lina wahanga wengi na hapa natarajia kuitwa kafiri, mpagani, mpinga kristo/masihi dajali na majina yote mabaya.
Umpangia aliyekuumba cha kufanya
 
Back
Top Bottom