Naona mbendera ya tanzania nusu mlingoti. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona mbendera ya tanzania nusu mlingoti.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TumainiEl, May 26, 2012.

 1. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,896
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kila anaye soma hilo neno hapo anapata shida kuelewa kwanini muandishi ameandika maneno hayo hapo juu, ila kwa mwenye macho ya ndani atagunduwa taifa hili bendera yake ktk macho yakawaida inaonekana kawaida ila ktk macho ya ndani taifa lipo bendera nusu mlingoti, nilazima viongoz wa taifa hili tangu Rais mpaka kiongoz wakijiji wajuwe yupo Mungu na yakuwa hatokuwa kiongoz wa milele kwa watanzania.

  Viongoz hawa tulio wachaguwa kwa kura zetu watanzania wametugeuka na kuwa vibaraka wa watu wachache wakat watanzania mamilion wakihangaika nakuteseka hata hawajuw watakula nini? Hawajuwi watavaa nini? Hawajui watapata wapi madawa na nyumba zao ni za udongo tangu nyakati ya mkoloni.

  Viongoz wa taifa hili wametia sahihi kwenye mikataba kwa kufumba macho na leo hii wapo watanzania kwa malak wanahama hama ktk taifa lao, elimu bora imetolewa kwa walio nacho na wasio nacho wanakalia mavumbi nakuandika ktk udongo. Ajira nazo nzuri kwa watoto wa vigogo hata kama hawawezi ila ajira wanazo wakati wapo watoto wawakulima wenye uwezo mkubwa wanakuwa makarani.

  Haki hakuna, kesi ya tajiri inahukumiwa kwa kupindisha sheria, masikini hata akiiba kuku kwa umasikin wake anafungwa miaka 17, anayeiba ma bilion anakula bata mtaani.

  Bendera ipo nusu mlingoti na chochote cha weza kutokea ili Mungu kuonyesha hasira zake juu ya viongoz wabadhirifu sio jeshi, vifaru, ndege za kivita zitamzuwia Mungu kuja kufanya mabadiliko ktk serikali ya Tanzania, ni lazima serikal ijuwe hakuna siri ktk Mungu huyu ambaye ni Mungu wa wote wenye mwili tajiri na masikini.

  Huu ni wakati Rais kuchukua na kufanya maamuz magumu kuokoa kizazi hiki na serikali ijayo, hatuna budi watanzania kujiweka tayari for any change to come, hakuna litakaloshindikana as long as watanzania tutasimama as 1 kusema ukwel na kufanya kaz kwa bidii.

  Mungu ibariki Tanzania Mungu wabarik wa Tanzania.

  Amen!
   
 2. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona wewe ni Nabii. Sema basi wazi tukuelewe.
   
 3. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Ni kweli, nguvu yetu ni umoja na kuthubutu, bendera i nusu mlingoti, ni maombolezo na msiba mkubwa.

  Ni wakati wa kufungua minyororo mikononi na miguuni mwetu, na vitambaa vyeusi machoni mwetu, utandu uliotanda akili zetu, frkra na imani zetu!

  Nani ni adui yetu? Je, ni kweli ccm kama tunavyoaminishwa? Siamini katika hilo, ila nachoamini adui yetu wa kwanza ni nafsi zetu wenyewe, nafsi zilizosaliti mantiki iliyomo ndaniye, na kupokea unafiki na kufanya iwe imani yetu. Ndicho wanachoamini wanasiasa wetu, kufuga manyigu na kutarajia kulina asali, uliona wapi? Kama hujamtambua adui yako, basi umeshashindwa vita tayari!

  UMOJA NA KUTHUBUTU ndio nguvu yetu. Bendera i nusu mlingoti!

  Mungu wetu anaita!
   
 4. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  cha kusikitisha zaidi hata elimu mkombozi wa wanyonge nayo imekuwa ni ya matabaka sasa watoto wa maskini kusoma chuo kikuu ni ndoto kipaumbele ni sayansi na ualimu,kwa kawaida sio wote wenye wito wa kusomea vitu hivyo ila wataenda kwa shida ya mkopo na si vinginevyo hiyo sayansi mtoto wa shule za kata hata bunsen burner hajawahi itia machoni,maabara ni kitendawili kwake leo anaambiwa aende sayansi inaumiza sana,watoto wetu mwaka huu wataomba ualimu watake wasitake.Cha kufurahisha serikali inadai haina pesa wakati mafisadi wanatafuna pesa,je hao mafisadi wanatoa wapi hizo pesa wanazotafuna kila uchao au wanaishi nchi jirani?this is terrible
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  Acha bendera ipepee nusu mlingoti, leo ndio yalikuwa mazishi rasmi ya CCM pale Jangwani
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,583
  Trophy Points: 280
  Mkuu Tumaini, bendera ni moja vitambulisho vya taifa letu hivyo huitendei haki kuiita "Mbendera", hiyo siyo bendera ya CCM wala sio bendera ya JK ni bendera ya taifa, ni bendera yetu hata CDM kikiwa chama tawala, hata Dr wa ukweli akiwa rais, bado bendera ndio hiyo, kwa nini uiite mbendera?!.
   
 7. K

  Kayinga junior Senior Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nikweli bendera ya muungano kamba yimechoka
   
 8. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  HIVI UMEGUNDUA KWA NINI BENDERA YETU INAFANANA NA ILE YA SOUTH AFRICA? HALAFU HATA WIMBO wa Taifa mungu Inariki africa unafanana na ule wa sauth africa!
   
Loading...