Naona giza mwaka 2020

Mamy K

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
3,042
10,704
Habari zenu wakuu

Kwa kweli Mimi ni miongoni mwa watu wasioipenda CCM, natamani nilale niamke nikute 2020 imefika nishiriki kuiondoa madarakani kwa sanduku la kura.

Ila kinachoniumiza ni mwenendo wa upinzani wa nchi yetu, naumia, Nikiangalia kulia namuona Bwana Lipumba anavyotumia nguvu zake zote kuibomoa CUF, na inavyoonekana anafanikiwa.

Nikirudi kushoto huku CDM Mara mavoice note ya mwenyekiti na kashfa nyingine lukuki,
Nikichungulia ACT siwaelewi, nawaona kama tawi la chama tawala.

Jamani kwa upinzani huu tutaitoa CCM madarakani? Naumia jibu likija kuwa hatuwezi, Huyu Mzinza kanifika hapaaaaa, simpendiii.

Au ndo Yale ya waliopo hatuwataki na wanaotaka tuwape hatuwaamini. Nimechoka mwili na roho, natamani kuhama nchi na Sina pa kwenda.
 
Upinzani wa Tanzania ni dhaifu mno.

Hauna mbinu, hauna sera, hauna ajenda, hauna dira, hauna mwelekeo, na hauna mipango yoyote ile ya maana.

Kazi yao ni kulialia na kuishauri CCM!

Upinzani Tanzania hauko tayari kushika hatamu za madaraka.
 
Mkuu 2020 tukiibashiri kwa kutumia maudhui ya kisiasa ya sasa kwa upinzani hali sio nzuri.

Ni vyema walitambue hili naamini miaka miwili ni mingi watajipanga.
 
Upinzani wa Tanzania ni dhaifu mno.

Hauna mbinu, hauna sera, hauna ajenda, hauna dira, hauna mwelekeo, na hauna mipango yoyote ile ya maana.

Kazi yao ni kulialia na kuishauri CCM!

Upinzani Tanzania hauko tayari kushika hatamu za madaraka.
Na kuongezea tu ni kuwa hakuna RASLIMALI WATU. In short ni VITEGA UCHUMI vya watu ( RUZUKU, MICHANGO & MISAADA ) siyo vyama
 
Haujataka kutafuta ukweli mkuu, mpaka sasa hiyo VN inaonyesha ni yakutengeneza

Kama bado upo Upinzani jua upo mikono salama, kama unaelekea kwenye Nzi wa kijani tambua uzeeni utakuwa mchawi.
 
  • Thanks
Reactions: 247
kukiangusha cha tawala sahau asee upinzani wenyew ni dhaifu hawana hata la maana walifanyalo sidhani kwa mwenendo huku CCM mbele kwa mbeleee
 
Upinzani wa sasa umegeuka ccm
ya zamani.Na ccm ya sasa kubali ukatae
ndo upinzani wa zamani tena enzi ya
Dr.
 
Upinzani wa Tanzania ni dhaifu mno.

Hauna mbinu, hauna sera, hauna ajenda, hauna dira, hauna mwelekeo, na hauna mipango yoyote ile ya maana.

Kazi yao ni kulialia na kuishauri CCM!

Upinzani Tanzania hauko tayari kushika hatamu za madaraka.
Ni kweli mkuu.

Wapinzani:
1. Mara wanaupinga ufisadi mara wanawakaribisha mafisadi na kuwapenda.
2. Miaka nenda miaka rudi wanakaripia wizi wa madini, leo wanawatetea wezi wa madini.
N.k.

Mind boggling. Not ready for prime time.
 
Back
Top Bottom