Naona future nzuri kwa Lazaro Nyarando, Mbunge wa Singida Kaskazini

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
"SIASA HAINA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU".
"SIASA HAINA MWENYEWE"

Mbunge wa Singida Kaskazini, Mh Lazaro Nyarandu amekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kipindi cha awamu ya nne ya Mh Jakaya Kikwete. Aidha, hajabahatika kurudi kwenye Baraza la Mawaziri kipindi hiki cha awamu ya tano, awamu ya Dk John Pombe Magufuli.

Tukio la ajali ya wanafunzi wa shule ya Vicent Lucky ya jijini Arusha iliyopelekea vifo vya wanafunzi 33 na walimu 2 imemfanya Mh Nyarandu kupambana sana kuhakikisha majeruhi wanaenda kutibia Marekani kupitia mtandao wake wa marafiki alio nao huko ambao pia wapo hapa nchini kwa ajili yan utalii.

Mh Nyarandu ameonekana mstari wa mbele sana kuhakikisha anawalink majeruhi hawa, serikali ya Tz na hao wafadhiri ili kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda kupatiwa matibabu nchini marekani kwa kiwango cha hali ya juu sana. hiki siyo kitu kidogo kwa mwanasiasa kufanya jitihada hizi.

Namwombea mema Mh Lazaro Nyarandu
 
Juhudi zake ni nzuri ila kitendo cha kukaa kila dakika anawapost wale watoto Instagram sidhani kama ni vizuri!
Wameshaenda kwenye matibabu tena na wazazi wao tuwaache wapumzike wapate tiba huku tukiwaombea kwa Mola awape ahueni!
Sasa kila dakika yeye anashinda install..mara ooooh sasa Hivi ndio wanaanza operations, Mara wamemaliza, Mara wameanza mazoezi etc...

Sijui lengo lake ni nini?
 
Unatafuta watu wa kukusaidia kufukua makaburi!?

Subiri awamu ya Mkulu mwingine sio hii.
 
"SIASA HAINA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU".
"SIASA HAINA MWENYEWE"

Mbunge wa Singida Kaskazini, Mh Lazaro Nyarandu amekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kipindi cha awamu ya nne ya Mh Jakaya Kikwete. Aidha, hajabahatika kurudi kwenye Baraza la Mawaziri kipindi hiki cha awamu ya tano, awamu ya Dk John Pombe Magufuli.

Tukio la ajali ya wanafunzi wa shule ya Vicent Lucky ya jijini Arusha iliyopelekea vifo vya wanafunzi 33 na walimu 2 imemfanya Mh Nyarandu kupambana sana kuhakikisha majeruhi wanaenda kutibia Marekani kupitia mtandao wake wa marafiki alio nao huko ambao pia wapo hapa nchini kwa ajili yan utalii.

Mh Nyarandu ameonekana mstari wa mbele sana kuhakikisha anawalink majeruhi hawa, serikali ya Tz na hao wafadhiri ili kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda kupatiwa matibabu nchini marekani kwa kiwango cha hali ya juu sana. hiki siyo kitu kidogo kwa mwanasiasa kufanya jitihada hizi.

Namwombea mema Mh Lazaro Nyarandu

Angalia dada Mange asije iona hii thread!!
 
Acheni kusahahau mambo mapema, Jamaaa hafai hata kuwa mwenyekiti wa Kijiji, kumbukeni akiwa waziri wa maliasili Jinsi Twiga, Nyati nk walivyokuwa wakisafirishwa hai, Kumbukeni Uwindaji wa kidharimu wa wale Waarabu mpaka Mchugaji Msigwa akatoa Clip ya kutisha. Hafai kabisa hata kuwa wa kitongoji. Hao Wamarekani wanaomfadhili ndio wale wale waliokuwa wakipiga dili za wanyama wetu.
 
"SIASA HAINA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU".
"SIASA HAINA MWENYEWE"

Mbunge wa Singida Kaskazini, Mh Lazaro Nyarandu amekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kipindi cha awamu ya nne ya Mh Jakaya Kikwete. Aidha, hajabahatika kurudi kwenye Baraza la Mawaziri kipindi hiki cha awamu ya tano, awamu ya Dk John Pombe Magufuli.

Tukio la ajali ya wanafunzi wa shule ya Vicent Lucky ya jijini Arusha iliyopelekea vifo vya wanafunzi 33 na walimu 2 imemfanya Mh Nyarandu kupambana sana kuhakikisha majeruhi wanaenda kutibia Marekani kupitia mtandao wake wa marafiki alio nao huko ambao pia wapo hapa nchini kwa ajili yan utalii.

Mh Nyarandu ameonekana mstari wa mbele sana kuhakikisha anawalink majeruhi hawa, serikali ya Tz na hao wafadhiri ili kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda kupatiwa matibabu nchini marekani kwa kiwango cha hali ya juu sana. hiki siyo kitu kidogo kwa mwanasiasa kufanya jitihada hizi.

Namwombea mema Mh Lazaro Nyarandu

Lakini mbona kuna wagonjwa kibao walio majeruhi na wasio majeruhi kwa nini hakuwasaidia kuwapeleka huko Marekani walao hata kwenda India? Kukodisha ndege kubwa kama ile, je Lazaro hakuona kuwa angeokoa wengi kwa kuwapeleka India na wangepata matibabu yaleyale? Hivi hakuna kilichojificha ktk msaada huo? Kama ni moyo wake basi Mungu ampe nguvu na mwangaza wa kuwaona wagonjwa wengine walioko huku Songea,Sumbawanga, Bukoba nk
 
Mimi ni miongoni mwa watu wasiomkubali huyu mtu anaitwa Lazaro Nyarandu, ila mtu kama kafanya kitu cha maana ebu tujaribu kumpa haki yake hata kama kafanya mabaya mangapi. ahukumiwe kwa mabaya aliyoyafanya sawa lkn pia apewe sifa panapostahili kama kafanya jambo jema. kama kafanya kujineemesha kisiasa mimi sijui, sana sana naangalia jambo alilolifanya. Kama kuna wagonjwa au wahitaji wengine wanahitaji huduma kama hii, tukumbuke kila mtu ana bahati yake, hapa ndio kapata nafasi ya kutenda ambalo kiila mtu mwenye akili timamu hana budi kumpongeza.
 
Back
Top Bottom