Naona binti yangu amekua, sasa kwa kumkomesha nimeamua nifanye hivi

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,203
85,311
Kwa kipindi cha likizo ya wiki moja, niliona kidogo pameku na mabadiliko kwa huyu mwanangu wa kike mkubwa.

Na hasa kikichokua kinanikera ni tabia yake ya kupenda kuingia chumbani kwetu (hata kama tunapumzika na mamayao), kisha anaanza kujiremba na akitumia dressing table ya mamayao.

Sasa hali hii ya kuingia chumbani kwetu kila anapojiskia ilikua inanikwaza sana, na sikupenda kumkataza kuingia kwasababu nilihisi kama nitamkwaza.

Sasa badala yake juzi niliamua kupitia pale kwenye vyuma chakavu na nikanunua 1" square pipe na flat bar kwa jumla ya shilingi 9,000.
Kisha nikanunua kioo kikiwa kwenye frame ya aluminum kwa shilingi 15,000.

Basi jana kwakua sikua na kazi pale ofisini, ndipo nikaamua nimtengenezee huyu mwali wangu dressing table kama hivi ili pindi watakapo funga shule na akirudi nyumbani tusije tukapata usumbufu tena.

Screenshot_2020-09-12-15-40-07-95.jpg
Screenshot_2020-09-12-15-40-46-81.jpg
Screenshot_2020-09-12-15-41-49-65.jpg
Screenshot_2020-09-12-15-41-55-84.jpg
 
Back
Top Bottom