Naombwa kujuzwa hili kuhusu NACTE

God knows

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
276
173
Leo hii nimepitia Central Admission System ya NACTE.

Nimekutana na kitu hiki:

Welcome to Central Admission System for Certificate,Diploma,Higher Diploma and Bachelor Degree for Ordinary Diploma Holders

The System allows you to apply for Admission into Further and Higher Education for academic year 2016/2017.


Available Application Categories:-
- Admission into Certificate/Diploma and Higher Diploma
- Admission into Bachelor Degree Programmes :- Deadline 31/05/2016


Kwa tangazo hili, inamaanisha kwamba NACTE wameanza kudahili wanafunzi wa Certificate, Diploma and Higher Diploma.

Naomba kuuliza kama je, ni vyuo vyote ambavyo vinatoa Certificate, Diploma and Higher Diploma ambavyo unaweza kuombea kupitia NACTE au ni vile vyuo ambavyo vipo under NACTE tu?

Nauliza hivi kwa sababu nimewapigia NACTE kwa namba zao tofauti 5 bila mafanikio.

Baada ya hapo nikawapigia TCU nikajibiwa kwamba ni vyuo vyote Tanzania whether vipo chini ya NACTE au TCU. Aliyenijibu kutoka TCU sina imani naye kwa sababu alikuwa anababaika wakati namuuliza maswali. Inaonekana kama hana taarifa sahihi.

Wadau mliopo kwenye Admissions Offices vyuo mbali mbali au yeyote mwenye uelewa wa hili, tafadhari naomba taarifa sahihi.

Nazihitaji taarifa hizi mno lakini nimekosa kwa kuzipata.
 
Vyuo Vyote Mkuu! Hata Vya Zanzibar! Chuo Hakiwez Kutoa Cert! Dip! Au High Dip! Bila Kuingizwa Nacte.
 
Hili suala limekuwa na utata,kuna watu watapoteza fursa za kusoma vyuo vikuu mwaka huu,wengi walizoea kuwa TCU ndiyo inahusika kudaili vyuo vikuu sasa kuna nacte!Nina wasiwasi na watu wanaojiendeleza kukosa fursa mwaka huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom