Naombeni ushauri....!!!

C

cashmoney

Member
Joined
Dec 14, 2011
Messages
90
Likes
3
Points
0
C

cashmoney

Member
Joined Dec 14, 2011
90 3 0
Habari wakuu..!!
Kifupi nina shida na uhitaji wa kupata mtaji wa kuendesha biashara yangu (operating capital). Nina kampuni changa ya microcredit activities (utoaji wa huduma za mikopo) ambayo nimeisajili na kuianzisha tangu mwaka 2011. Mwaka 2012 nilitarajia kuanza kutoa huduma lakini mambo hayakwenda kama nilivyotarajia kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu na imenichukua takribani mwaka sasa nimejaribu kuhangaika kupata mtaji niendelee na biashara hii. Nina ka nyumba ka urithi (ingawa mzazi bado yupo hai) ambacho Bi mkubwa (mama) alinishauri either nikaombee mkopo benki, ktk taasisi za kifedha au kwa mtu binafsi au kuiuza nipate mtaji, lakini nimejaribu kufuatilia njia hizo hadi sasa bilabila. Ktk taasisi za kifedha na mabenki wameniambia inatakiwa uzoefu wa kuendesha biashara hiyo usiopungua miezi sita hadi mwaka. Kuna threads ktk jukwaa la matangazo madogomadogo nilipost humu JF tangu miezi sita iliyopita kuhusu kuuza nyumba hiyo lakini sijafanikiwa kupata mteja hadi leo (hata wa kwenda kuiona tu sijampata). Mda unavyozidi kwenda akili inazidi kunipelekesha nikiwazua namna ya kufanikisha lengo langu. Nimeshachoma meli moto (nimeachana na kazi zangu za kuajiliwa tangu mwaka juzi) lakini changamoto ni nyingi mno. Ufupi naombeni ushauri nifanyeje kufanikisha mpango huu maana mwaka ndo huu unakatika na sijui hata niweke mikakati gani kwa ajili ya mwakani.
Natanguliza shukrani.
 
chaUkucha

chaUkucha

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
3,242
Likes
334
Points
180
chaUkucha

chaUkucha

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
3,242 334 180
iyo ni nyumba ya familia na sio urithi kama ulivyosema unaweza kuitumia kuombea mkopo bank.
 
C

cashmoney

Member
Joined
Dec 14, 2011
Messages
90
Likes
3
Points
0
C

cashmoney

Member
Joined Dec 14, 2011
90 3 0
iyo ni nyumba ya familia na sio urithi kama ulivyosema unaweza kuitumia kuombea mkopo bank.
Ni nyumba yangu ya urithi na si ya familia kama unavyong'ang'ania. Na kuhusu kuombea mkopo bank kwangu ktk hali niliyonayo kibiashara ni ngumu kama nilivyoeleza hapo juu, kuwa kampuni yangu yenyewe ni ya kutoa mikopo na sina experience ya operations za kutoa huduma, nimeshajaribu bank zote wameniambia niwe na experience isiyopungua miezi sita au mwaka ya utoaji huduma maana kwa sasa ndo naanza (start up).
 
Tembele

Tembele

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Messages
1,144
Likes
20
Points
135
Tembele

Tembele

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2011
1,144 20 135
Hongera kwa kuwa na Mawazo ya kujitegemea.

1. Biashara yako ina vibali vyote halali?

2. Unaweza kuandika andiko linoonyesha kuwa ukipewa fedha itaweza kurudi. (Kwamba mradi utarudisha pesa)

3. Unataka Hiyo pesa kwa ulipe kwa utaratibu upi, kwa mwezi ama?

4. Una mdhamini ama dhamana kwa hiyo pesa unayotaka kukopeshwa?

Nijibu hapo then I will see the best way we can assist.
 
M

masagati

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
412
Likes
101
Points
60
M

masagati

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
412 101 60
Changamoto ndiyo kipimo cha akili komaa na wazo lako ukishinda changa moto ndiyo umeshinda mtihani wa maisha.
kuwa mwangalifu na majibu yako wengine wanapima akili yako ili pengine akupe msaada wewe unajibu vibaya wote watakupuuza mfano :umesema UNANG'ANG'ANIA
 
C

cashmoney

Member
Joined
Dec 14, 2011
Messages
90
Likes
3
Points
0
C

cashmoney

Member
Joined Dec 14, 2011
90 3 0
Hongera kwa kuwa na Mawazo ya kujitegemea.

1. Biashara yako ina vibali vyote halali?

2. Unaweza kuandika andiko linoonyesha kuwa ukipewa fedha itaweza kurudi. (Kwamba mradi utarudisha pesa)

3. Unataka Hiyo pesa kwa ulipe kwa utaratibu upi, kwa mwezi ama?

4. Una mdhamini ama dhamana kwa hiyo pesa unayotaka kukopeshwa?

Nijibu hapo then I will see the best way we can assist.
1. ndio biashara ina vibali vyote
2. ndio naweza andika
3. nitakuwa natoa mikopo kwa wafanyakazi ambao muajiri wao atakuwa tayari kuwadhamini ili marejesho yatoke ktk makato ya mishahara yao. mikopo itatolewa kuanzia kipindi cha mwezi mmoja hadi miezi 12.
4. nitaweka nyumba kama dhamana
 
C

Changamoto2015

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2012
Messages
759
Likes
47
Points
45
C

Changamoto2015

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2012
759 47 45
Umesema vema mkuu! Huyu jamaa inabidi achunge sana asiingiwe na hasira katika utoaji wa majibu yake wakati anaulizwa.
Changamoto ndiyo kipimo cha akili komaa na wazo lako ukishinda changa moto ndiyo umeshinda mtihani wa maisha.
kuwa mwangalifu na majibu yako wengine wanapima akili yako ili pengine akupe msaada wewe unajibu vibaya wote watakupuuza mfano :umesema UNANG'ANG'ANIA
 
V

VeroEretico

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Messages
305
Likes
182
Points
60
V

VeroEretico

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2013
305 182 60
1. ndio biashara ina vibali vyote
2. ndio naweza andika
3. nitakuwa natoa mikopo kwa wafanyakazi ambao muajiri wao atakuwa tayari kuwadhamini ili marejesho yatoke ktk makato ya mishahara yao. mikopo itatolewa kuanzia kipindi cha mwezi mmoja hadi miezi 12.
4. nitaweka nyumba kama dhamana
Mkuu ni mtaji kiasi gani unahitajika ili kuanzisha hii biashara
 
Forum statistics

Threads 1,252,277
Members 482,061
Posts 29,802,493