Mungu ni muweza wa yote, fanya maombi ya kufunga omba sana na Mungu atafungua milango,soma Yeremia 33.3, Yeremia 29.11, hakuna jambo linaloshindikana kwake Mungu, atakusaidia tu mdogo wangu. Pia waweza kwenda sehemu ya ibada unakoabudu mwambie kiongozi wako kama ni Mchungaji, Padre au Shekhe, atakutangaza pale uapoabudia wapo watu wenye mioyo ya huruma, upendo na utoaji watakusaidia, pole ila Mungu yupo pamoja na wewe na utafaulu na siku moja utakuwa kazini ukipokea mshahara wako, hayo ni majaribu tu, yatapita, pia sikiliza wimbo wa Upendo Kilahiro usemao " HILO NALO LITAPITA"