wana mtoto mmoja wa kuzaa na mwingine wa ndugu ambaye ni yatima ila wanalingana kiumri na wote wanaishi nao.
Hapa sister haongei kitu zaidi ya imetosha, na huyo bwana amesafiri jana tu
na pia hataki kumwuuliza maana anasema kuuliza si utatuzi maana kwa mtu mwenye akili anajua alkua anayafanya hayo kwa sababu gani! Yeye anasem tu imetosha
mama d;
ahsante kwa maelezo na poleni sana kwa yaliyotokea, ni kweli inauma sana na kati ya vitu vinavyouma sana ktk maisha na kuweza kusababisha mtu afanye maamuzi magumu, ambayo kwa baadaye yanaweza yakawa na matokeo mabaya au mazuri ni suala zima la mapenzi. Ukweli ni kwamba huyo mme amemkosea sana dada na ni haki dada kuumia kiasi hicho, sasa nini nafasi yangu mie ktk hili;
dada achukue muda ili akae na kuongea na ndugu na marafiki makini ambao anawaamini na anaweza akashare nao personal issues kama hili na asikie wao wanamshauri vipi. Ktk hili naomba kusisitiza, kamwe asimshirikishe ndugu au rafiki ambaye ndoa ilishamshinda au ambaye ana always negative idea about marriage, ndiyo maana nimesema ndugu na rafiki makini.
Then, apate muda yeye binafsi na kuweza kutafakari maisha yake na mume wake, akumbuke pia ups and downs ktk maisha bila kusahau malezi ya watoto (hili lina umuhimu sana ktk ndoa, na si rahisi sana mara zote kuwa na malezi mema kwa malezi ya upande mmoja. Yawezekana huyo mme akaonekana hana msaada economically, lkn i can assure you kwamba ana mchango mkubwa sana ktk malezi ya watoto na heshima ya hapo nyumbani na familia kwa ujumla.
Dada kabla hajaamua kumshirikisha hao watu makini, hana budi aongee na mme wake. Kumbuka, hapa hekima na uvumilivu inahitajika sana kwa pande zote (dada na mme wake) ili waweze kuongea na kuona kama kweli mme anaonyesha kujutia yale yaliyotokea na nini inaweza ikawa nafasi yake kwa maisha yao kama mme na mke. Nasisitiza hili la kuongea wawili ni muhimu sana, kwani sisi kama binadamu tuna mapungufu mbalimbali na hivyo tuna nafasi ya kuweza kuongea ili kuyapatia muafaka. Ktk hili dada inabidi ajaribu kupunguza hasira na kuwa tayari kuongea na mme wake. Dada asiishie tu kusema basi tu, basi tu! Dada inabidi aongee na mme wake.
Nb: Mwishoni, dada atapaswa kufanya maamuzi yeye mwenyewe hasa baada ya kuwa na maongezi na mme wake na wale ndugu na marafiki makini. Kwanini afanye maamuzi yeye mwenyewe, ni kwasababu madhara ya hayo maamuzi atakayoyafanya yatakuwa kwake siku zote. Na kumbuka, maisha ya ndoa ni zaidi ya uwezo wa kiuchumi.
Poleni sana na zaidi mtangulizeni mungu ili aweze kuwaongoza ktk kulipatia hilo suala ufumbuzi. Mama d, jaribu kuwa karibu na dada ktk hali hiyo ili uweze kumsaidia.
Rdi.
wana mtoto mmoja wa kuzaa na mwingine wa ndugu ambaye ni yatima ila wanalingana kiumri na wote wanaishi nao.
hapa sister haongei kitu zaidi ya imetosha, na huyo bwana amesafiri jana tu
na pia hataki kumwuuliza maana anasema kuuliza si utatuzi maana kwa mtu mwenye akili anajua alkua anayafanya hayo kwa sababu gani! yeye anasem tu imetosha
Mama D.... Nimejisikia vibaya utadhani mimi ndie niliefanyiwa..... Inauma. Inaumaaa mno, lakini hata hivo sishangai.... Usitegemee hata siku moja kua doing everything right and to perfection maana yake ndio kwamba mwanaume hatatoka nje. Lah! Nafurahi kama dadako kaona imetosha na yeye ndie alieamua kama yatosha. Ingekua ni mwanamke ambae tu katereza huko na akatoka nje... that would have been at least understandable... But dating a woman wa kale for more than six years! Dah!
Ukweli unabaki kua huyo mume yupo na mkewe sababu anamhitaji na sio kumpenda... na saa ingine hata hicho kitendo cha kuingiza kipato kidogo ni tu ile kujiendekeza tokana na ukweli kua kabweteka tokana na the way anakua treated na the wife on top of that kuendelea kujengewa heshima ya mume, baba na mtoto (kwa wazazi na nduguze); Naamini kwamba ingekua the other way round huyo mume angekua alisha muacha siku nyingi mkewe ili awe na huyo mpenzi wake wa kale.
Cha ajabu ni kwamba... NDIO ni mda mrefu.... Lakini sijui ni kwanini Mapenzi ya wizi ni mazuri na hudumu. Amini usiamini anaweza aachane hapo na mkewe na huyo hawara wa mda woote huo wakashindwa kua pamoja saa ingine hata mwaka tu! Hata hivo niachane na shemejio...
Mama D... Ni muhimu ujue kua dadako ana hali mbaya saan emotionally na psychologically hasa tokana na the fact kua she is holding it inside. Atakua bado in shock, hajielewi... thou anatambua kilicho tokea na kukubali... bado akili na moyo hujaregister ipasavo. Saiz itahitajika awe na mtu wa karibu na kum - consol.... I feel for her and wish her all the Best kwa lolote atalo amua.
Ukweli unabaki kua huyo mume yupo na mkewe sababu anamhitaji na sio kumpenda...