Jumakwamba
New Member
- May 18, 2024
- 2
- 7
Habari, mimi nimeoa nina mke na nimezaa nae watoto wa nne, mke wangu ni mzaliwa wa Tanga, kuna mistake ambayo nilifanya nilijikuta natoka nje ya ndoa yangu na kuanzisha mahusiano na binti mwingine (mchepuko) ambae ni mzaliwa wa kondoa (mrangi) na huyu mchepuko pia nimezaa nae watoto wawili. Mke wangu amegundua kuwa nimechepuka na nimezaa nje ya ndoa yangu, furaha imetoweka ndani ya nyumba na mke wangu anataka nimpe talaka tuachane. Kiukweli nashindwa kumuacha mke wangu kwasababu ni mwanamke mwenye kujielewa sana, mpambanaji na pia ndie nilieanza nae tangu sina kitu mpaka Leo hii mungu kajaalia nina maisha mazuri
Niliteleza kuchepuka na kuanzisha mahusiano na huyu mwanamke mwingine wa kirangi na kuzaa nae
Kitu sahihi ambacho nimewaza au naona ni sahihi ili kunusuru ndoa yangu ni kuachana na huu mchepuko ili nibaki na mke wangu tulee watoto wetu kwasababu huyu mchepuko kwanza hana akili ya maisha anachojua ni starehe na kupenda vitu vya thamani ambavyo havina maana katika maisha yani hawazi maendeleo yoyote zaidi ya starehe na kuvaa nguo mpya tu
Nimewaza niwajengee watoto niliozaa na huyu mchepuko kisha nimpe msingi afungue biashara ili hiyo biashara atakayofungua ndio iwe inapatikana pesa ya kulisha watoto, na nimepanga kuwakatia Bima ya afya watoto ili iwasaidie pindi wakiumwa kwa maana mimi nibakie na jukumu la kuhakikisha tu watotoe wanasoma na kulipiwa Ada shule.
Sihitaji connection yoyote na huyu mchepuko ili niweze kukaa na mke wangu kwa amani na yeye nimuache na maisha yake.
Naomba kujua, nikimfungulia biashara ili iwe inasaidia kulisha watoto niweze kuepeka suala la kutoa pesa za kila siku za matumizi ya watoto ni sahihi au si sahihi?! Naomba ushauri wenu na mawazo yenu nini sahihi nikifanye maana naona tayar nishachanganya Unga na cement kwenye maji mpaka sasahivi, nishauri chochote ambacho unahisi kitanisaidia