Naombeni ushauri wa kisheria juu ya hichi kiwanja ili kiuzike

Charlie chaplin

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
336
311
nini kinapaswa kifanyike inapotokea hali kama hii baada ya mirathi.
  1. document yaani orijino ya offer ya kupata hati ya kiwanja kutoonekana
  2. ila copy zipo za hiyo offer na watoto wa marehemu wanataka kuuza hicho kiwanja je? sheria inashauri nini kifanyike kama hawa warithi hawana orijino documents. na wanataka kuuza kiwanja cha urithi
 
Duuh sasa itakuwaje mkuu hapo kwenye haya mambo ya kisheria kwa maana haki inatakiwa itendeke

nimeleta jukwaani ili wadau wa sheria watoe mawazo yao maana ni watu wengi sana kwenye jamii wakifiwa hii hali huwatokea na kushindwa kupata haki
 
nini kinapaswa kifanyike inapotokea hali kama hii baada ya mirathi.
  1. document yaani orijino ya offer ya kupata hati ya kiwanja kutoonekana
  2. ila copy zipo za hiyo offer na watoto wa marehemu wanataka kuuza hicho kiwanja je? sheria inashauri nini kifanyike kama hawa warithi hawana orijino documents. na wanataka kuuza kiwanja cha urithi

Ndugu, cha kufanya hapo hao warithi (watoto wa marehemu kama ulivyosema) watoe taarifa kutuo cha polisi kuhusu kupotea kwa hizo nyaraka (offer). Baada ya hapo wakatoe tangazo kwenye gazeti la serikali (government gazette) kuhusu upotevu huo. Mwisho baada ya yote hayo waende kwa Msajili wa viwanja awapatia title deed (hati ya kiwanja).
Hapo sasa wataweza uza eneo lao kisheria bila bughdha au mushkeli wowote.
 
Mirathi inatosha;

Kama orijino offer hazionekani hilo linaelezeka mana ni marehemu anajua alipoziweka, Kwa hiyo msimamizi wa mirathi aende mahakamani aombe hati ya kupatiwa hati kupitia kopi za offer, akishapewa anaenda arithi wilaya kufuatilia utaratibu wa hati.

Kama wewe muomba ushauri ndio mnunuzi, nakushauri muende mahakamni wote, wewe na msimamizi wa mirathi na warithi wote iandikwe hati ya wao kukubali kukuuzia hicho kiwanja kwa kutumia kopi ya ofa kwa maelezo kuwa original hazionekani ndio utoe hela.

Fungua inbox yako pia kuna sms nimekuandikia
 
Ndugu, cha kufanya hapo hao warithi (watoto wa marehemu kama ulivyosema) watoe taarifa kutuo cha polisi kuhusu kupotea kwa hizo nyaraka (offer). Baada ya hapo wakatoe tangazo kwenye gazeti la serikali (government gazette) kuhusu upotevu huo. Mwisho baada ya yote hayo waende kwa Msajili wa viwanja awapatia title deed (hati ya kiwanja).
Hapo sasa wataweza uza eneo lao kisheria bila bughdha au mushkeli wowote.

asante sana mkuu. je jina la hati wakati wa mauziano halitaleta shida kwa kua ni jina la mzazi wao marehemu? je huchukua muda gani baada ya kupublish kwenye government gazzette mpaka msajili atakapotoa deed?
 
Jina la hati halitaleta matatizo hata kama hawataamua kubadilisha. kwa vile wao ni warithi tu na si wamiliki wa mali bora jina la hati libaki kuwa la marehemu, wala halitaleta shida. Baada ya tangazo kutolewa kwenye gazeti la serikali na maombi kupelekwa kwa msajili, hati hutolewa ndani ya mda usiozidi siku tisini
 
Waende ofisi ya ardhi ya sehemu husika ili afisa ardhi aweze kupitia jalada la kiwanja husika na kucertify hiyo nakala ya hati kuwa ni original......
 
Back
Top Bottom