Naombeni ushauri tafadhali

pondiboy

Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
81
Reaction score
29
wana jamvi mimi ni kijana nina 27 yrs, tatizo langu ni kwamba nilikuwa na girlfriend wangu ambaye tulipendana saana!!
Mpenzi wangu huyu nilikutana naye kipindi nikiwa nahitimu chuo mwaka 2011, sio siri nilimpenda na nilimuona kila kitu kwangu kwa ukweli hata yeye anajua nilimpenda naye pia!
baadhi ya ndugu zangu walimfahamu na pia ndugu zake walinifahamu!!!
kila mmoja wetu alipopata shida tulisaidiana!!! tulikuwa tukitembeleana mara kwa mara kwani yeye alikuwa iringa na mimi dar!!! mwanzoni mwa mwaka Jana nilisafiri kuja mikoa ya kanda ya ziwa!! hivyo tukawa mbali mbali zaidi kuliko ilivyokuwa awali! Tulipanga Dec mwaka Jana tungeenda kutambulishana lakini nikashindwa kwenda kutokana na majukumu niliyonayo huku nilipo! ulizuka ugomvi mkubwa! mpenzi wangu yule alinikatia mawasiliano!
hapo nilijitahidi saana kutafuta suluhu lakini nilishindwa. mwisho ikawa ni january mwishoni mwaka huu akaniambia nitafite mwanamke mwingine! alijaribu kunihesabia yale tuliyotofautiana toka tunaanza mahusiano! nilihuzunika saana toka hapo hapokei simu wala kujibu msg zangu. najihisi kuchanganyikiwa sielewi nifanye nini, nimekata tamaa ya maisha! naomba kama kuna mtu anaweza kunisaidia kisaikolojia ani-pm
 
Pole sana kijana ila usijaribu kusema umekata tamaa ya maisha kwa ajili yake kwani maisha yako yapo mikononi mwako mwenyewe
 
Usikate tamaa ya maisha sababu ya demu, jikaze wewe mtoto wa kiume

Je ukikutana na chalenji za kimaisha si ndio utajinyonga

Changamka wewe acha kulia lia
 
pole kaka, hawa wanawake wanabadilika kulingana na mazingira. co be strong in any circumsitances
 
Ukiona mpenzi uliyenaye anakufanya ulie kila siku,jiulize huyo uliyenaye ni mpenzi au ni bomu la machozi!
 
mtoto wakiume kukata tamaa kisa mwanamke ni uzembe

mitoto ya kike ipo mingi hivyo wewe unataka kufa kisa mmoja ambaye amekutosa..

grow some balls and move on with your life..damit!!
 
mtoto wakiume kukata tamaa kisa mwanamke ni uzembe

mitoto ya kike ipo mingi hivyo wewe unataka kufa kisa mmoja ambaye amekutosa..

grow some balls and move on with your life..damit!!
Mbaya zaidi wewe umeshapoteza maisha, yeye anaendelea kula bata
 
naombeni mnielewe ndugu zangu! mnajua hayo mengine ni nature yanakuja automatically, najitahidi kukaa na marafiki, kuwa busy lakini nashindwa kumsahau kila mara namkumbuka
 
Jikaze mkuu, usiuze timu nakuomba

Kinachokusumbua mazoea tu, baada ya muda utasahau
 
pondiboy niskilize vizuri, hayo maisha au hicho kipengele kama si wote basi ni % kubwa ya watu wanakipita, (binafsi yashanikuta) unachotakiwa kuamini ni kua huyo hakutakiwa kua mke wako na ukilazimisha yanaweza kukukuta zaidi ya hayo, usikubali hisia zako zikutawale utapotea, kuna wanawake warembo na tabia unazozipenda waiting for you, 27yrs unakata tamaa? Ni shida kumsahau kwa sasa ila inawezekana tena simple sana, hatua ya kwanza uwe busy, fanya mazoezi, usikae pekeako na ikibidi kua pekeako kama mda wakulala hamia jf soma thread, changia....
 
Last edited by a moderator:
Nyie ndio mnatabirika

Dada yangu wanawake katika mia unaweza kupata wawil wenye true love
Wanasema kabisa bora nife mapema kwa kua na maisha mazuri kuliko kufa kikongwe na maisha magumu
Wanawake ndo mnatufanya tuibe na kufingwa jela ili kuwalidhisha
Mf kajala masanja
 
Kuachwa kuachwaaaaa...
.kuachwa ni shughuli pevuu..aaaaah.

Mbaya zaiiidi kwa yule uliyempenda.
Wewe unakonda,yeye ananenepa

Kwa mawazoooo....Kwa mawazoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…