Naombeni ushauri tafadhali!

Naombeni ushauri tafadhali!

Gogobaby

Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
55
Reaction score
3
Nna boyfriend wangu nampenda sana tatzo ni kwamba siku hizi simuelewi kabisaa kwani amekua busy kupita kiasi inafikia kipindi wiki nzima yeye hanitafuti kwenye simu mpaka nimuanze mimi nikipiga simu hapokei badae akinipigia ananambia kitufe cha kupokelea kimeharibika na hivi sasa mwezi umepita sasa sijaonana nae.Nashindwa kumuelewa kama ni aje
 
Mwezi hamjaonana mnakaa jirani? Maana isije ikawa yeye yupo Tabora we upo Musoma.

Kama mpo jirani/mji mmoja labda kwake we ni rafiki tu kama washkaji zake sio boyfriend ile ya upenzi.
 
Shogaaa kusoma hujui, na picha pia huoni?......zinduka mwana kwetu
 
Muombe uonane naye akueleze sababu za yeye kuwa kimya namna hiyo. Kichwa ni yako ukitaka kunyoa au kusuka.
 
Kwa nini unajiita Gogobaby?
Labda unalalaga kama gogo kwa nini asisepe?
 
Last edited by a moderator:
Watoto wa dot.com siku hizi mnashida sana, sijui ni uvivu wa kufikiri au ni maisha yamewabadilisha? enzi zetu ukikuta mtu anaomba ushauri unasoma mara mbili mbili hujui cha kushauri jinsi ishu ilivyo taiti.. siku hizi hujanunuliwa pipi unakuja kuomba ushauri khaa! kweli dunia inabadilika
 
Nna boyfriend wangu nampenda sana tatzo ni kwamba siku hizi simuelewi kabisaa kwani amekua busy kupita kiasi inafikia kipindi wiki nzima yeye hanitafuti kwenye simu mpaka nimuanze mimi nikipiga simu hapokei badae akinipigia ananambia kitufe cha kupokelea kimeharibika na hivi sasa mwezi umepita sasa sijaonana nae.Nashindwa kumuelewa kama ni aje

Unauliza sukari kwenye duka la vifaa vya ujenzi? Umeshapoea hapo kifupi huna mtu.
 
Muombe uonane naye akueleze sababu za yeye kuwa kimya namna hiyo. Kichwa ni yako ukitaka kunyoa au kusuka.
si ameshamwambia kibatan cha simu kibovu sasa amueleze nini tena?
 
anafanya kazi gan? mpo umbali gani? Simu yake ushawahi kuiona sku za karbuni?
 
Yuko manispaa, umbali sio mkuubwa unapanda hata bajaj dakka 10 tu cjaiona cm yake tangu msimu wa ckukuu za mwaka mpya
 
Njoo huku ucheze mwenyewe kama unahisi huko unachezewa:a s 114:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom