Naombeni ushauri, nimepigwa na butwaa

Naombeni ushauri, nimepigwa na butwaa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,702
Reaction score
57,187
Habarini za mihangahiko wakubwa zangu najua wengi ni wakubwa kwangu waliomo humu ndani kwa hiyo naombeni mnisaidie Hili suala linalolisumbua sana akilini katika haya maisha kiasi cha kunipa stress.

Nawasihi mnipe ushauri ambao utanisaidia ndugu yenu na wala msichukulie kama ni ishu nyepesi kiukweli imeniumiza sana Inaweza kukutokea na wewe.

Ipo hivi mwanzoni kipindi nasoma huko Singida Mwenge secondary kisha nikapiga chuo flani cha sanaa nikapata kazi mbeya tayari nilianzaga uhusiano na binti flani wa kinyaturu jina lake Maria alikua mrembo sema tulikuja kugombana nae na hii ni mda mfupi baada ya kumchukua toka kwao na kwa kuwa kwao maisha hayakuwa mazuri mama ake alimkubalia tu aje Mbeya nimtafutie kazi pia niishi naye na kumleta mbeya nilipokuwa napiga kazi ishu yenyewe tuliokwaruzana.

ilikuwa hivi nilimtafutia kazi ndio lakini kuna siku alinikamata namchepuko wangu flani wa chuo flan pale mbeya akaniuliza kwann unanifanyia hivi John kwangu hupat nini kiukweli nilimjibu vibaya nilimwambia "kwanza we nshakutaftia kazi ukiamua kapange chumba chako mwanamke mwenyewe mshamba na haupendezi " huyo maria alilia sana yaani sijui kwanini nilijitoa ufahami nikamjibu hivyo kana kwamba nilikuwa sina mapenz naye bali kumchezea.

Ni matatizo ya dunia nilifanya kosa. Tukaendelea kuwa wapenzi lakini kuna ishu nyingine tena ikatokea na hii msala ulikuwa kwake nilikamata simu yake anachat na wanaume wengine na charting zipo katika mkao wa kimahusiano ye alinijib shortcut kwamba anachat nao hajawah ku sex nao me nikaona huyu ananiletea za mazoea ya kiniaje kwani me boya niamin kwamba awe na mahusiano na mtu alafu asigegedwe nikaamua ku mshit nikamwacha Mbeya me nikaja Dar nikahamia kikazi na nikavunja mawasiliano naye ingawa kuna kipindi tulishawahi hadi na kuwa na mipango ya ndoa nadhani tulivoachana ye aliumia zaidi kwasababu mimi nilishakuwa wa mjini hapa Tanzania napenda kujichanganya nikaamua kushit mipango yote na mawasiliano na ndugu zao kimsingi nilibadilisha line.

Sasa nimekuja Dar kwenye kazi zangu za sanaa bahati nzuri nikapata office ipo mjini nikapata na mdada mzuri tu na yeye ni mwanafunzi wa chuoni semister ya mwisho ametokea kunizimikia sana na kama unavojua umri unaenda na Dar starehe nyingi kwa huyu mtoto wa chuo nilikuwa nipo mbioni nafanya mipango ya kutambulishana ndoa na kaharusi sio mbaya tungefanya hata mwakani lakini huyu msichana wa mwanzo Maria amebadilika sana kimtizamo amekuwa na akili sana ya maisha toka nimwache kwenye kazi yake Mbeya.

Maria week kama mbili ziizopita amenitafuta kwa jamaa yangu flani akapewa namba akatoka Mbeya a kaja mpaka Dar na ndege, alinitumia meseji kuwa nipo Dar tukutane sehem nikaona sio mbaya labda ana ujumbe mzito nilivokutana nae amenipa maneno kuntu na ya uchungu sana kiasi kwamba nimepagawa huruma imenishika moyo umekuwa mzito amenambiaa tafadhal John me wewe toka zamani tunapendana sa kwann tumeachana kwa sababu hazina msingi.. Maria ye umri wake ni kama tupo sawa huyu wa chuo nimempita miaka minne

Kiukweli alafu huyu Maria amekuwa mzuri sana siku hizi anavaa vizuri anafanya biashara zake amekuwa na maendeleo ananiambia anachotaka me na ye tufunge ndoa akanambia binadamu hajakamilika kuna vingi tuna weka mistake tusamehane akanambia ukweli alikuwa na mahusiano na wanaume kama wawili pale mbeya na mmoja ni rafiki yangu mfanyabiashara pale Mbeya basi baada ya kukiri makosa yake akaniambia tusamehane yote alafu tufanye mipango ya harusi na kwamba binadamu ni kiumbe dhaifu na kwamba wote ukicheki tulikosea hivyo basi ana haki ya kusamehewa na anachoangalia mbele kwa sasa ni mimi and yeye tujenge familia bora yenye maendeleo akanipa simu niongee na mama yake mama ake akanisihii kuwa tuache utoto tumeshakuwa wakubwa tusamehane.Dondoo zile za maria na mamake zimeniumiza sana kihisia nimejikuta nalia karibia ucku kucha .

Lakini dah me sina time nipo busy tayari na huyu msichana wangu mpya ambaye yupo college hapa Dar mtoto ni wa kichaga mama ake mkubwa anayeishi nae kawalea malezi mazuri. Kwa kuwa na moyo mmoja basii nishaamuaga kuwa na mpenzi mmoja sasa nashindwa kuamua nichague yupo na ndipo lilipo hitaji langu la msaada wenu wa huku Dar hatuna muda mrefu naye ananipenda sema pia mtoto wa huku Dar naye ananiheshim sana yupo kwa wazaz wake ugali dona maisha yanandelea.

Naogopa huyu wa Dar ni tamuumiza sanasana anamiamni namsaidia vitu vingi chuo naanzaje kumuacha Maria ndani ya moyo wangu ni jina kubwa kuzid lowaza. Natetemeka kila nikikumbuka Saut yake akiniambia kuwa ye ni mtu mzuri na maalum kwa ndoa yangu nisikosee na ukicheki Maria yuko bomba siku hizi kazi yake inampatia hela ni anapenda mafanikio.
Ifahamike kuwa sio kweli ninachokipendea kwa maria ni pesa bali ni jinsi ana vo hustle kutwa kuzitafuta, hata hivo pesa aliyonayo sio kubwa sana ila kwa muda mfupi alioanza kazi na hasa ukiangalia ni mtoto wa kike kwa kwel ana hitaji pongezi.. Kama huku Dar ningepata mwanamke wa ajabu (sifa zao unazijua) nisingejiuliza mara mbili ningemchukua mtoto maria jumla ila ugumu ni kuwa hata huyu mtoto wa Dar anajitahid kunipenda na kunionyesha ana iman asilimia Mia kuwa akimaliza shule lzm nimuoe japo mipango yote sikuwah kumwmbia dadake naye tunaheshimiana nae anasema tufunge harus mapema atatusapot kimtindo Naombeni kujua yupi hapo ni mke wangu sahihi. Maria ana leta hizi mambo najikuta nmuonea huruma hili jambo linatengeneza history kubwa ya mapenzi lazima iwe history nzuri yenye faida ila naogopa kumuumiza mmoja wao mawazo mpaka najikuta nimekuwa mlevyi nakunywa pombe nyingi.

Sio sinema wala sio ndoto bali nimeshindwa kuamua na kama mnavojua suala la ndoa sio la kujaribu na hitaji kuweka akili na hisia sawa ili nisibugi
 
Maria. Maria ooohh Maria. Nipo na mawazo Sana saa hii Maria Mke wangu Mwema anaumwa. Tulia kwanza nitakushauri tuu kwa kutumia KVL and KIL
 
Ulipokuwa unaamua wala hukuuliz yamekufika utosini ndio unatujia sasa
 
Yeah baba ni balaa hapo kuamua but fata moto wako unapokutuma hata kama utamuumiza mmoja
 
Mimi naona Maria humpendi ndio maana ulimtendea ulotenda na bado unasema maria kakuchanganya kwa kuwa siku hizi kapendeza na Ana pesa! Wewe inaonekana unatafuta maslahi na sio mpenzi. Acha ulevi jitafakari Mara mbili wala hilo sio swala la kukufanya ulewe
 
Utoto wewe ndio unamaamuzi sio sisi wakukuchagulia mke
 
Tayari ushaseme unampenda sana mwana college wako sasa tukushauri nini wakati maria unamuonea tu huruma lakini humpendi? Inamaana tukikushauri urudi kwa maria siku huruma itaisha utamuumiza tena mnyaturu wa watu we fuata Maisha yako upendavyo usituletee ngonjera hapa
 
Chaguo ni lako


Kama kweli unaomba ushauri na unamaanisha,

1. Futa mtazamo wa pesa za maria, mpende maria kama maria kwani maria anakupenda pia.

2. Muoe Maria haraka iwezekanavyo.

3. Huyu mwanachuo usimwambie kitu, punguza mawasiliano taratibu sana na muweke wazi maria juu ya mwanachuo.

Ndoa njema na usichepuke kamwe.


Kumbuka kuleta mrejesho.


Ahsante
 
  • Thanks
Reactions: Art
Kama kweli unaomba ushauri na unamaanisha,

1. Futa mtazamo wa pesa za maria, mpende maria kama maria kwani maria anakupenda pia.

2. Muoe Maria haraka iwezekanavyo.

3. Huyu mwanachuo usimwambie kitu, punguza mawasiliano taratibu sana na muweke wazi maria juu ya mwanachuo.

Ndoa njema na usichepuke kamwe.


Kumbuka kuleta mrejesho.


Ahsante
 
Umeona eee, huyu jamaa aitaka pesa ya maria
 
Acha uongo we hujatulia, utaendelea kuwaumiza na hata huyo wa chuo anataka msaada wako tu, akimaliza chuo ataamua kuolewa na amtakaye
 
Back
Top Bottom