Naombeni ushauri: Msichana wangu ana mchepuko

Naombeni ushauri: Msichana wangu ana mchepuko

lucky lefty

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
491
Reaction score
454
Habarini wakuu,

Nina msichana wangu mmoja tulianza nae mahusiano toka 2013, katika maisha ya mapenzi baina yetu kuna kipindi cha kati hapo tukagombana, ikabidi kila mmoja akaendelea na ishu zake.

Sasa yeye mwenzangu katika kipindi hicho tulichoachana akatoka na lijamaa huko akapewa kibendi, Mungu akamjaalia akajifungua mtoto wa kiume. Katika kipindi chote toka alipopata ujauzito jamaa aliyempa kibendi alikataa kuhudumia mpaka mtoto alipozaliwa.

Mara baada ya kujifungua huyu msichana akaanzisha tena mahusiano na jamaa aliyemtoa usichana (huyu siye aliyempa kibendi), katika mahusiano yao sijui kilichoendelea lakini niliskia waliachana.

Katika shida shida za utawala huu wa mjomba magu huyu msichana akanitafuta last year and tuka reconcile so akawamsichana wangu tena. Tatizo lilikuja alipotaka nimuoe, mimi sikuwa na tatizo sema kama mtu ninaejielewa ikabidi nifanye uchunguzi (sikutaka kuingia kichwakichwa kwenye ishu za ndoa) kama hana mchepuko huko alipo na ndio hapo nilipojua anatoka na lijamaa lake la zamani.

Ushahidi nilikuwa nao wa kutosha kuanzia messages hadi baadhi ya siku huwa anaenda kulala kwa mchizi, sasa nilipo mconfront kama najua anamchepuko na najua huwa analala kwa mchizi baadhi ya siku msichana alinijia juu kwa maneno mengi akataka tuachane, tatizo sikuwa na nia ya kumuacha ilikuwa tuongee tuyamalize lakini mwenzangu akawa analazimisha tuachane, sasa katika marumbano mimi nikaona isiwe tabu tukapigana chini.

Sasa cha kushangaza jioni yake baada ya kuachana akanitumia message kuniomba msamaha kwa alivyokuwa ananijibu na hataki tuachane kwa hasira, nikamwambia nimemsamehe.

Sasa hapa nipo dilema maana msichana nampenda na yeye ana feelings nasema hivi kwa sababu tunakaa mikoa jirani na kila nikiwa na shida naye nikimpigia aje kesho jua lazima atatia maguu gheto, sijawahi kumwambia aje akazingua au akagoma au akaleta kisingizio cha kutokuja.

Na hata kesho nikimwambia aje huku nilipo atakuja ingawa tumeachana, tatizo hataki kukiri makosa yake na hataki hata kusikia ushahidi niliokuwa nao.

Naombeni ushauri wakuu nimpotezee kimoja au niwe mvumilivu nishee na mchizi?
 
Kama kazalishwa na hilo jamaa na bado yuko nae bora umuache2

wanawake huwa hawasahau waliowatoa bikra na waliowazalisha
Na wewe haupo kati ya hizo
 
Saa nyingine ukisema usikilize moyo tu kuna vitu unakuwa unakubaliana navyo ila madhara yake yanaonekana baadae

Binafsi naona mwanamke anayeweza kutoka kwako akaenda kulala kwa mwanaume mwingine hafai...kama una nia ya kumuoa muoe ila lolote litakalotokea katika ndoa yenu hutatakiwa kumlaumu sana since alishakuonesha true colours zake tangu huku

Kama ningekuwa mimi ningeachana na mtu wa design hiyo...
 
wewe jamaa ni kilaza sana,yaani wenzako tunavyowasulubu hao wanawake tutakavyo wewe unakuja kututia aibu humu na pumba zako,eti nampenda,unampenda malaya,how does it come?
nilichokigundua jamaa hauna hela,fanya kazi kwa bidii upate pesa hizo shida za moyo wako zitabakia historia!
 
Hiv unajua kuwashwa washwa alikokusema baba mwenye nyumba bas wewe na huyo dada mnawashwa washwa
 
Back
Top Bottom